Slobodan Mirosovich
Member
- Jan 9, 2026
- 40
- 196
Ndugu zangu kamwene,
Katika ulimwengu wa madaraka, kuna wakati taasisi inabidi ijioshe ili ipate hewa ya kupumua. Nchi inapokwama kiuchumi kwa sababu ya doa la damu mfumo haulazimishi kila mtu kuwajibika maana kuna uwajibikaji hauna impact hivyo anatafutwa mtu mmoja mwenye uzito wa kubeba lawama zote.
Kilichotokea tarehe 29 Oktoba kimeacha kovu ambalo wahisani na jumuiya ya kimataifa wamekataa kulisahau wamegoma kabisa kuelewa pamoja na juhudi ya waziri mwenye dhamana kuzunguka duniani kote mpaka kwenye milango ya mkuu wa kanisa ila bado wakubwa wa dunia wamegoma kabisa, milango ya misaada imefungwa, na funguo ziko mikononi mwa watu wanaotaka kuona damu ikilipwa kwa uwajibikaji.
Kama mlivyoshuhudia kiongozi mkuu hawezi kusema nilikosea, mara zote hajakubali zaidi ya kuhamisha lawama mara walikua wakenya, mara nguvu iliyotumika ilikua inaendana kiufupi amegoma kukubali mapungufu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi yaliyotumika kipindi kile hivyo, mbinu pekee iliyobaki ni kutengeneza mazingira ya kuonyesha kuwa kulikuwa na dola ndani ya dola(State within a State).Kwamba kulikuwa na mtu mmoja mwenye nguvu aliyekuwa anatoa amri bila Mkuu kujua.
Mbuzi wa kafara ameshapatikana maana anajulikana si na wasanii tu bali nchi nzima kutokana na kujiweka kwake kimbelembele na kutumia ukaribu wake na mkuu kujitengeneza kasri ndan ya kasri na kula raha mfumo umeona huyo ndo anafaa kuwa mbuzi wa kafara. Kijana aliyeishi maisha ya anasa na kuogopwa hata na maboss wa vyombo ndiye anayepakwa mafuta ya kuwa mhusika mkuu wa tamthilia hii ya kutisha.Safari yake kutoka Katibu wa Mkuu kwenda Ubalozi wa hewa na sasa kupelekwa Wizarani, siyo bahati mbaya wala siyo uteuzi wa kawaida. Ni mchakato wa kutengwa (Isolation).
Kwa nini atolewe nyumba tukufu? Kwa sababu huwezi kumnyooshea kidole mtu aliye ndani ya kuta za mkuu itamchafua mkuu pia kwa hiyo unamtoa nje kidogo, unamvua vyeo vyake nyeti, unampeleka sehemu ya biashara na masoko ambako hana kinga ya kishushushu. Unamfanya awe raia wa kawaida mwenye cheo kikubwa, binadamu wanatabia ya kunyenyekea na kujipendekeza kwa wenye mamlaka kutolewa kwake karibu na kuwa na influence na mkuu kunamfanya apoteze thamani na umuhimu kwa waliokuwa wanamuaminia hivyo nguvu ya kujipendekeza kutoka kwa makundi fulani kama matajiri, wana siasa na watu mashuhuri kwenda kwake inaondoka automatically maana hatakua na msaada nao tena.
Hapa ndo pazito naomba mnielewe kwa umakini Tume iliyoundwa kutafuta suluhu ya doa la oktoba29 imeeleweshwa juu ya msimamo wa mkuu na kuwekwa bayana kuwa msimamo huo haubadiriki, hivyo ripoti ya kitaalamu haitakua na msaada wowote kwa mantiki hiyo ripoti ya tume inayokuja haina lengo la kutafuta ukweli mpya, bali kuhalalisha mhusika. Majibu ya Tume yataelekeza kuwa amri za nguvu kubwa zilizoleta madhara na maumivu kwa watanzania zilitolewa na Ofisi ya Katibu bila mkuu kupata taarifa sahihi wala kutoa ridhaa.Huu ndio unaitwa uongo wa Kimkakati (strategic deception)
Kwa kumfanya kijana aliyekua anapenda kuonekana kila sehemu na mkuu kuwa Kafara (Scapegoat), nchi itawaambia wahisani "Tumeshamgundua msaliti aliyesababisha mauaji, na tumemuwajibisha." Hapo ndipo mikataba itasainiwa tena na misaada itaanza kumiminika hali ni tete kwa sasa kiasi cha kuiweka hazina ya dhahabu rehani.
Kiukweli huu ni mchezo wa kikatili sana usio na huruma hata kidogo lakini pia lazima tujue kila raha inakaraha zake ukifurahia favor za mfalme jiandae ipo siku utaonja pia hasira au hila zake kama ilivyomtokea Amani wakati wa Mordekai na Esta, mtu aliyekuwa mwaminifu zaidi anageuzwa kuwa silaha ya kuisafisha Serikali. Inabidi aonekane alijichukulia sheria mkononi ili kumlinda aliyemtuma. Katika kanuni za siri msaidizi hufa ili Mfalme aishi.
Hapo wizarani ametupwa kama kituo cha kusubiri hukumu ya umma. Sababu ya kiburi na kudhani anaujua mfumo nje ndani huenda hata hajui maskini.Mara nyingi wahusika wa kafara huaminishwa kuwa wanapumzishwa kwanza. Ila ripoti ya Tume itakaposhuka, itakuwa ni pigo ambalo hataweza kurudi tena kwenye mzunguko wa ndani. Ni mchezo wa draft la kiungwana lenye maumivu makali mno.
Inasikitisha, lakini huu ndio ukweli wa chai ya nyumba tukufu .Unakunywa na Mkuu kwenye vikombe vya dhahabu mkicheka na kupanga hatima ya nchi huku ukisahau kuwa uaminifu wako huo ndio utakaotumika kama leso ya kufuta doa siku nguo ya Mkuu ikichafuka.
Hakuna upweke mkubwa kama wa mtu aliyetoa maisha yake kumlinda mwingine, kisha akaishia kutupwa nje ya ukuta ili kutosheleza kiu ya wenye hasira. Unabaki na vyeo vya picha ila moyoni unajua umegeuzwa kinga ya makosa ambayo hukuyafanya kwa niaba yako.
Kuwa mkono wa Kulia ni heshima kubwa, lakini kumbuka mkono huo ndio hukatwa kwanza ili kuokoa mwili usioze Ilimlazimu Yesu aliyekua mkono wa kulia wa Mungu asulubiwe ili binadamu waokolewa wakati mwingine wokovu unahitaji sadaka za walio karibu na utukufu.