Sehemu ya 10
Tulienda mpaka ipuli ambako ni nyumbani kwa shemeji yake na madelagawisa ambaye ndio alituuzia mchongo. Tukazihesabu hela na zilikuwa milioni 40 kasoro. Mpoladuhu akasema maisha yanaitaji roho ngumu sana, kama tungekata tamaa tungezipata wapi hizi hela?
Tuligawana pale watu wanne na yule muuza ramani wa 5, ila yeye hakupata sawa na sisi.
Kesho yake nilirudi home nikiwa nimejaa tele nikaamua kupanga chumba kingine siku hiyo hiyo maeneo ya kanyenye jirani na mwika. Na kile pia nilibaki nacho hivyo nilikuwa navyo viwili. Nyakati hizi naikasema hakuna kufeli tena, nilimdanganya mwanamke nimetoka machimbo hivyo nikampa hela ya biashara namimi narudi machimbo.
Nilikaa wiki nikarudi Rombo nyumbani kwenda kuweka mambo sawa. Baada ya hapo nikapitia Arusha kuwasilimu kina mroso na palangyo, ambako nilipata taarifa ya kuwa wote waliuwawa kule stendi ya mboya moshi. Ilinishtua sana na mdogo wake na palangyo akazidi kuniambia arusha saivi hapafai kabisa polisi wamechachamaa sana.
Namimi nikaamua nijirudie zangu tabora. Ile kufika tu Mpoladuhu ananiambia hatulali tunaunganisha usinge kuna ramani. Nilikuwa najihisi mchovu lakini hamna namna. Safari ya usinge ilianza, tulifika kaliua nakulala pale tukiwa na gari hilux double cabin nyeusi. Kesho yake asubuhi tukaondoka na kuelekea usinge, ambako tulikutana na wadau wawili ambao walikuwa wanatupa mchongo wa hela. Kwa muhtasari mchongo ulikuwa kwenda kumwibia maarabu mmoja hapo mwanga ana mabiashara na mabasi hivyo tulitakiwa kuwa timu ya kutosha maana hautakuwa mchongo rahisi hata kidogo. Tuliondoka usinge na kwenda mpaka nguruka ambako huko tuliungana na genge lingine na kuwa jumla yetu 8. Hapo hapo usinge tulilala siku mbili kwaajili ya kujiboost kwa wazee. Hatukuwa na silaha yoyote ila tayari location ya kwenda kupata kupata silaha ilikuwepo. Gari mbili ziliongozana hilux na hiyo nyingine rav4 nyeusi. Tuliingua kigoma na kwenda kuweka kambi yetu maeneo ya mwanga kilimahewa. Mpango ulifanyika wa kupata silaha maeneo ya kitongoni, ambapo zilipatikana bunduki 8 yaani kila mtu yakwake, kati ya hizo kuna pistol na hizi smg pamoja na risasi zake. Wale ambao walitukodisha walikuwa sharti lao nao wawe sehemu ya tukio maana wao pia wanataka hela. Hivyo tukawaunga jumla yetu 10 mwarabu kazi anayo. Tuliondoka na kwenda location * kwaajili ya kuhifadhi zana za kazi na kisha kuondoka na kwenda kuoga tena dawa kwa wataalam kwaajili ya kujilinda.
Siku ya tukio ilifika na kulikuwa na mvua na radi za mngurumo balaa, tukajongea site kuendelea kuangalia hali ikoje tukaona ni mizigo inaingia na kutoka maana walikuwa na sheli pia. Ilipofika mida ya kukaribia kufunga gari moja iliangalia uelekeo wa magharibi na nyingine mashariki pale tulishuka maana tulikuwa tushajipanga 5 waliingia site na sisi 5 tulibaki nje, hapo ni milio ya risasi nakwakweli wale tuliokuwa nao walikuwa majambazi haswa hakuna maswali mengi unakula chuma ni hela zitolewe waarabu nao hawakuwa nyuma kuna wawili walianza kurudisha mapigo na hapo mji ukachangamka sasa wawili waliongezeka ndani kutoa msaada na hela zilianzwa kukusanywa vizuri, polisi nao tayari walikuwa alert na hilo tukio kutokana na milio heavy hawakusogea eneo la tukio tulivyoanza kuondoka kila gari ilishika uelekeo wake mimi nilikuwa kwenye rav4 tulienda kuwakuta mapai lake Tanganyika tukarushiana risasi kidogo, dereva akaenda mitaa ya buzeba ili polisi wasirushe risasi. Ila mpaka hapo roho mkononi, tukaendelea kufukuzana huku nao wakitufukuza kuelekea road block zao. Shughuli yetu ilienda kukwamia bangwe na ndipo tulianza mashambulizi tena. Katika rusha nikurushie tunazidi kupunguwa huku polisi wakisisitiza tujisalimishe. Tukaambizana sasa kila akimbie ashike njia yake kujinusuru. Mimi nikakimbilia kule makaburini na ndio ikawa pona yangu giza lishaingia wale niliokuwa nao wote waliuwawa onspot pale na mapolisi wote 4.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.