Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Sehemu ya 2
Tulienda dar es salaam na usafiri binafsi wa baba mkubwa nakufika, ambapo alikuwa akiishi kurasini karibu kabisa na mizani. Miasha ndani ya jiji ya dar hayakuwa mazuri sana maana joto lilikuwepo na mbu kwa wingi, haswa ukizingatia arusha hali ya hewa haswa ukanda wa sakina una baridi kwa kweli. Ndani ya wiki mbili 2 niliugua Malaria na kwa wakati huo dawa iliyokuwa ikitumika sana ni chloroquine. Ila dada zangu wao hawakuugua Malaria.

Tulikaa dar na baba mkubwa akatutaftia shule huko moshi ambayo ni ya bweni yaani kulala ili tusijihisi upweke pale nyumbani. Hivyo tulienda kusoma shule moja inaitwa Moshi Academy maeneo ya ushirika kibosho. ( Kwa watu wa moshi watakubaliana nami ushirika na kcmc zote zipo ndani ya kibosho).

Kwa maisha ya pale shule tulisoma na mimi nilifaulu ijapokuwa nilipata wakati mgumu sana haswa kwenye kubadili mtaala maana ukumbuke pale arusha shule tulisoma kwa mfumo wa Cambridge na sio huu wa Tanzania. Nilimaliza darasa la 7 mwaka 1998 nikawaacha wadogo zangu shule ambao nao walilia sana kuwa hawawezi kusoma hapo kama sipo. Lakini walibaki kusoma hapo hapo. Mimi nakumbuka baada ya hapo baba mkubwa alinipeleka tabora kwa shemeji yake ambaye alikuwa akikaa maeneo ya bachu. Nilifika tabora na nilifanyiwa mpango wa kujiunga na Tabora boys.

Nilianza kidato cha kwanza mwaka 1999 na mwaka huo ndio ulikuwa ni kama mwanzo wa mateso yangu. Baba mkubwa alikuwa amechukua mikopo hivyo mambo hayakuenda vizuri na duka lile la vitambaa pale kilombero lilokuwa la mzee aliliuza pamoja na ile nyumba iliyokuwa halali yangu kwa kisingizio cha elimu yetu ni kipaumbele kumbe alitumia kulipa madeni yake. Hivyo mambo yalianza kwenda kombo mimi nikiwa busy na shule baba mkubwa mambo yalizidi kuyumba sana baada ya hapo mke wake ambaye alikuwa ni mwenyeji wa tabora maeneo ya isikizya alimwambia sisi ndio chanzo cha mikosi na mabalaa yanayomkumba hivyo atuache turudi kwa bibi kijijini.

Baba mkubwa alijaribu kukaza shingo akiwa na nia thabiti ya kutusaidia ila shinikizo la mwanamke ukizingatia na hali inazidi kudorora kiuchumi, rasmi mrija wa misaada ulikata kwangu na kwa wadogo zangu, mimi pale nilipokuwa nikikaa nilihama mwenyewe kwasababu ya manyanyaso, kipindi hiko maji tabora yalikuwa ya shida hivyo unaeza tumwa kwenda kisimani unachota maji na baiskeli ukirudi unaambiwa uende upeleke mchele wa vitumbua mashineni hapo hujala chochote.

Ukirudi unaambiwa uwashe moto na kwenda kutafta kuni za kupikia ukirudi unakuta wameshakula wamekuachia ugali kidogo na kisamvu cha karanga. Ukishakula hapo ndio basi tena mpaka kesho tena. Mi kiujumla hayo maisha yalinishinda yamanyanyaso haswa ukizingatia sikuyazoea kabisa, nikaomba kuondoka kurudi nyumbani, nilipandishwa basi la nbs na kurudi dar. Dar napo nikapokelewa mzobe mzobe kwa kisingizio kwamba nimewatukana mama zangu wadogo na mkwe wa baba mkubwa hivyo nikafungashiwa virago na kupandishwa basi la ngorika kurudi moshi ambapo ntaenda kijijini Rombo kwa bibi.

Kweli nilifika mida ya 8 mchana njia panda ya himo nikashushiwa hapo na mizigo yangu. Nilikaa sana nikimsubiri mtu wa kuja kunipokea ndipo kijana mmoja ndugu naye alipokuja na kurudi na mimi mlimani. Kule nilikutana na wadogo zangu na kwa kweli walifurahi sana kuniona nami pia nilifurahi sana kuwaona faraja zilirejea mioyoni yetu kwa muda huo.

Maisha ndani ya Rombo hayakuwa mazuri, bali yalikuwa ni ya shubiri kukata majani ya ng'ombe, kutafta kuni, kusafisha hori la ng'ombe na fimbo kwa wingi sana yaani ukifanya kosa dogo ni fimbo haswa! Tulikosa mtetezi na ni kama tulitengwa na hilo lilikuwa linaonekana wazi wazi maana hata kuku akichinjwa sisi tutaishia kupewa vikwaru kwaru yaani miguu, kichwa au kibawa kile ambacho hakina nyama. Na hata wakipika nyama basi wengine wanafichiwa katikati ya wali na pale juu inawekwa moja au mbili kama geresha.

Mwaka 2000 niliamua kwenda tarakea kwa shangazi alipoolewa nikakaa huko ili nijaribu kufungua ukurasa mpya wa masha yangu!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Mwaka 1999 kuna Bus la Nbs na Tabora boys unaenda na kurudi home, maana yake Tabora Boys ilikuwa Day School au siyo
 
Sehemu ya 10
Tulienda mpaka ipuli ambako ni nyumbani kwa shemeji yake na madelagawisa ambaye ndio alituuzia mchongo. Tukazihesabu hela na zilikuwa milioni 40 kasoro. Mpoladuhu akasema maisha yanaitaji roho ngumu sana, kama tungekata tamaa tungezipata wapi hizi hela?
Tuligawana pale watu wanne na yule muuza ramani wa 5, ila yeye hakupata sawa na sisi.
Kesho yake nilirudi home nikiwa nimejaa tele nikaamua kupanga chumba kingine siku hiyo hiyo maeneo ya kanyenye jirani na mwika. Na kile pia nilibaki nacho hivyo nilikuwa navyo viwili. Nyakati hizi naikasema hakuna kufeli tena, nilimdanganya mwanamke nimetoka machimbo hivyo nikampa hela ya biashara namimi narudi machimbo.
Nilikaa wiki nikarudi Rombo nyumbani kwenda kuweka mambo sawa. Baada ya hapo nikapitia Arusha kuwasilimu kina mroso na palangyo, ambako nilipata taarifa ya kuwa wote waliuwawa kule stendi ya mboya moshi. Ilinishtua sana na mdogo wake na palangyo akazidi kuniambia arusha saivi hapafai kabisa polisi wamechachamaa sana.
Namimi nikaamua nijirudie zangu tabora. Ile kufika tu Mpoladuhu ananiambia hatulali tunaunganisha usinge kuna ramani. Nilikuwa najihisi mchovu lakini hamna namna. Safari ya usinge ilianza, tulifika kaliua nakulala pale tukiwa na gari hilux double cabin nyeusi. Kesho yake asubuhi tukaondoka na kuelekea usinge, ambako tulikutana na wadau wawili ambao walikuwa wanatupa mchongo wa hela. Kwa muhtasari mchongo ulikuwa kwenda kumwibia maarabu mmoja hapo mwanga ana mabiashara na mabasi hivyo tulitakiwa kuwa timu ya kutosha maana hautakuwa mchongo rahisi hata kidogo. Tuliondoka usinge na kwenda mpaka nguruka ambako huko tuliungana na genge lingine na kuwa jumla yetu 8. Hapo hapo usinge tulilala siku mbili kwaajili ya kujiboost kwa wazee. Hatukuwa na silaha yoyote ila tayari location ya kwenda kupata kupata silaha ilikuwepo. Gari mbili ziliongozana hilux na hiyo nyingine rav4 nyeusi. Tuliingua kigoma na kwenda kuweka kambi yetu maeneo ya mwanga kilimahewa. Mpango ulifanyika wa kupata silaha maeneo ya kitongoni, ambapo zilipatikana bunduki 8 yaani kila mtu yakwake, kati ya hizo kuna pistol na hizi smg pamoja na risasi zake. Wale ambao walitukodisha walikuwa sharti lao nao wawe sehemu ya tukio maana wao pia wanataka hela. Hivyo tukawaunga jumla yetu 10 mwarabu kazi anayo. Tuliondoka na kwenda location * kwaajili ya kuhifadhi zana za kazi na kisha kuondoka na kwenda kuoga tena dawa kwa wataalam kwaajili ya kujilinda.
Siku ya tukio ilifika na kulikuwa na mvua na radi za mngurumo balaa, tukajongea site kuendelea kuangalia hali ikoje tukaona ni mizigo inaingia na kutoka maana walikuwa na sheli pia. Ilipofika mida ya kukaribia kufunga gari moja iliangalia uelekeo wa magharibi na nyingine mashariki pale tulishuka maana tulikuwa tushajipanga 5 waliingia site na sisi 5 tulibaki nje, hapo ni milio ya risasi nakwakweli wale tuliokuwa nao walikuwa majambazi haswa hakuna maswali mengi unakula chuma ni hela zitolewe waarabu nao hawakuwa nyuma kuna wawili walianza kurudisha mapigo na hapo mji ukachangamka sasa wawili waliongezeka ndani kutoa msaada na hela zilianzwa kukusanywa vizuri, polisi nao tayari walikuwa alert na hilo tukio kutokana na milio heavy hawakusogea eneo la tukio tulivyoanza kuondoka kila gari ilishika uelekeo wake mimi nilikuwa kwenye rav4 tulienda kuwakuta mapai lake Tanganyika tukarushiana risasi kidogo, dereva akaenda mitaa ya buzeba ili polisi wasirushe risasi. Ila mpaka hapo roho mkononi, tukaendelea kufukuzana huku nao wakitufukuza kuelekea road block zao. Shughuli yetu ilienda kukwamia bangwe na ndipo tulianza mashambulizi tena. Katika rusha nikurushie tunazidi kupunguwa huku polisi wakisisitiza tujisalimishe. Tukaambizana sasa kila akimbie ashike njia yake kujinusuru. Mimi nikakimbilia kule makaburini na ndio ikawa pona yangu giza lishaingia wale niliokuwa nao wote waliuwawa onspot pale na mapolisi wote 4.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Duh, dunia hii jamani dah
 
Mwaka 1999 kuna Bus la Nbs na Tabora boys unaenda na kurudi home, maana yake Tabora Boys ilikuwa Day School au siyo
It's the brain work to find fault, mistake,error, negative,danger etc so no wonder.

So Kama amedanganya si uachane naye ama akuhakikishie Kama Ni ukweli itaongeza namba yoyote kwa maisha yako,ama kipato chako?

Na je story una uhakika gani Kama Ni ya kutunga ama uwongo ama ukweli,tangiapo ikiwa ukweli,uwongo ama kutunga wewe itakusaidia Nini ama kupunguza nini. Is there anything you wanna trade with this story?
 
It's the brain work to find fault, mistake,error, negative,danger etc so no wonder.
So Kama amedanganya si uachane naye ama akuhakikishie Kama Ni ukweli itaongeza namba yoyote kwa maisha yako,ama kipato chako??
Na je story una uhakika gani Kama Ni ya kutunga ama uwongo ama ukweli,tangiapo ikiwa ukweli,uwongo ama kutunga wewe itakusaidia Nini ama kupunguza nini. Is there anything you wanna trade with this story?
Dude, why all of these? I was just wondering if NBS company was existing with such a name and Tabora boys School was a day school by then,je kuna tatizo kwenye hilo mkuu?
 
Dude, why all of these? I was just wondering if NBS company was existing with such a name and Tabora boys School was a day school by then,je kuna tatizo kwenye hilo mkuu?
Mtu hawezi andika yote sahihi. Kuna kampuni zipo tokea zamani mno. Mie nimejitambua nayaona mabasi ya Zachary Peter,kimotco nimempanda so no wonder.mie sio wewe Bali Ni Aina ya ubongo tulio nao hata mie ninao Ila sio your personality. Yaani ndio nature ya ubongo wetu yaani kila binadamu
 
Sehemu ya 9

Nikaona Arusha hali ishakuwa mbaya uzulumati ndio jadi na ili uweze kusurvive basi yakupasa uwe mbabe haswa!

Nikarudi Rombo kupumzisha akili ila sikukaa sana nikaenda kwa bibi Marangu ambako ndio nilikaa mwezi mzima huku nikitafakari hatua inayofuata mbele.

Nikaondoka na kwenda kuanza maisha mapya huko Tabora, ambapo nilipanga chumba maeneo ya Isevya.

Kule nilianza kujishughulisha na nguo za mtumba, ambapo nilikuwa naagiza mzigo Dar ukifika mimi nasambaza madukani. Huko nilibahatika kupata mwanamke tukawa tunaishi naye pika pakua.

Niliifanya biashara hiyo ila haikudumu maana ilikuwa ni ya mikopo sana. Hivyo nilifilisika rasmi na back to square one. Nyumbani kule dogo anasumbua maana ndio yuko form 4 na hapa pia mwanamke kazi hataki anajua kupokea tu na umri wangu ulikuwa bado. Kichwa kilikuwa kinawaka moto kurudi nyumbani naona jau. Nikaamua kuingia kwenye biashara ya ganagana( daladala baiskeli).

Nikafainya kwa muda wa kama wiki moja, nilipata ruti ya kutoka mjini kwenda Cheyo kama nne hivi. Sasa huwa kuna kamlima fulani kupandisha, miguu iliuma nikalala ndani siku 2 na kazi hiyo nikasema hainifai.

Nikaingia kupiga vibarua vya kushusha cement na saidia fundi na penyewe pakuwa pagumu sana kwangu.

Siku moja nilienda Mwinyi Mchichani kwenye bar x kufurahi huko nikakutana na Mpoladuhu ambaye tulianza kupeana michongo ya hapa na pale.

Nyakati hizo zilikuwa ni za majira ya asali huko Sikonge na Kaliua. Mpoladuhu akaniambia twende Kaliua, ambako huko tulipanda gari na kuelekea kilomita 90 Ugala huko mpakani mwa Tabora na Katavi.

Shughuli iliyotupeleka huko ni urinaji wa asali kinyemela huko Ugala na kurudi mpaka hifadhi ya Lumbe. Yeye alikuwa ni mtaalam wa urinaji na tulifanikiwa kupata madumu 5. Lakini hayakuzaa matunda kwani tulikamatwa na game na kunyang'anywa yote na kichapo juu!

Tukarudi mjini na tukaamua kuunda genge letu tukamuongeza Kinehe na Madelagawisa ambao tutashirikiana katika maisha. Hivyo kila mmoja hapo ameshawahi kuwa katika matukio kadha wa kadha.

Tuliondoka na kwenda katika milima ya Izimbili ambako huko tulijifua kwa dawa na kula viapo mfano ukidakwa basi kufa mwenyewe, kugawana pasu kwa pasu, kutokuzungukana n.k. Kule mbuzi mnyama alichinjwa na madawa mengine na tulipigwa kila mtu chale mwilini za kinga. Kwasababu wasukumu ukiwaibia mara nyingi wanakimbiliaga kuloga hivyo tuliona tujizaetiti mapema.

Katika kutest mitambo na kujiweka sawia na kazi tukaamua twende tukawatembelee huko Cheyo kwanza.
Tulienda mitaa ya Cheyo A, ila tulighairi na kwenda Uzunguni ambako tulipata taarifa za mstaafu mmoja. Hapo hatukuwa na silaha ni mapanga tu hivyo usiku tulimvamia na kuvunja mlango maana hakukuwa na uzio katika hiyo nyumba. Tulizama ndani na bila kupoteza wakati tulianza kuwapa kichapo, lakini wapi mstaafu mwanaume hataji hela zilipo na mwanamke pia hataji wote wamekaza.

Piga na mabapa ya mapanga mpaka mstaafu akazimia ila mwanamke aligoma katakata kutaja hela zilipo. Walikuwa wawili tu nyumbani mume na mke. Hivyo tukaanza kupekuwa huku na huko pesa hazionekani tukirudi kwa mwanamke anasema hajui zilipo.

Muda unazidi kwenda na hapo uzalendo umeanza kutushinda. Mpoladuhu kwa hasira alinyanyua meza kumpiga nayo yule mke wa mstaafu, na ndipo kila mtu akastaajabu. Meza ya mbao kwa chini imegongewa mbao nyingine na kwa ndani ndipo hela zinapokaa.

Bila kupoteza muda tuliivunja na kutoa maburungutu ya hela na kutia kwenye mfuko wa rambo na kutokomea zetu tukimwacha akiangua kilio kikali sana.

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Wewe una matukio zaidi ya Umughaka na wenzake kina Gabby
 
Sehemu ya 11
Nilikaa pale makuburini, na muda uliyoyoma sana nikaamua kusubiri muda uzidi kusonga maana niliona hapa ndio salama yangu.

Kausingizi kalinipitia kidogo nikaja kuamshwa na wanga waliokuja kufanya yao makaburini, wao hawajiona ila mimi nimewaona. Nikaamka kuwafata ili kujua natokaje tokaje hapa, naona wao pia wananikimbia kwa hofu sijui walihisi mfu kafufuka au vp.

Nikaendelea kujibana na vituko viliendelea nikaona busara nisisumbue tena watu nkaja kamatwa hivo nilijiongeza kusubiri adhana ilie ili niende uelekeo huo huo. Macho nayo yalikuwa mazito ila adhana niliisikia nami nilifata uelekeo huo huo mpaka Masjid pale nikajiziguzisha maeneo yale na kwakuwa mabomba yapo nilinawa. Mida ya sala ilivyoisha nikiwa na hang hang mitaa hiyo kwa kutosomeka nilisikia stori watu wanapiga. Yameuawa wote, mengine yamekatwa, yule muarabu haingiliki wale wameyakanyaga. Nikajua hapa kishanuka

Kulipambazuka na stori kubwa town ilikuwa ni hiyo ukipita vijiweni au stendi watu wanasimuliana. Hapo sina hata ndururu (sina hela) nikawaza naondokaje huu mkoa wa Kigoma.

Nikaenda stendi kuzengea zengea nikamwona konda ananichangamkia, nikamuuliza unaenda wapi jomba? Akasema Kasulu! Nikamwambia namimi naenda huko huko ila sina nauli msaada namimi ntapiga debe, akasema sawa kwanza fanya usafi ufagie ndani ya gari hilo utoe taka zote ukamwage.

Nikafanya kama nilivoambiwa, gari lilikuwa kwenye kilo abiria walivyojaa likaondoka njiani mambo yalikuwa mengi sana ila nilifika Kasulu na kuanza kufanya kazi za day worker sokoni.

Na kulala ilikuwa ni kambi popote nilikaa kama wiki mbili kisha nikaondoka na kwenda kibondo maeneo Twabagondozi ambako huko napenyewe ni vibarua vya mtaani tu.

Huko nilibahatika kupata rafiki anaitwa Ulokoze, huyu naye tulizoeana na katika kupiga soga za hapa na pale aliniambia mishe kuu kwa huku nikuteka magari au mabasi utaweza?

Nikawaza nikaona hizo mishe ni ndogo ndogo sana nikamwambia hamna za hela ndefuu? Akasema labda wewe utupe sisi uzoefu wetu ni huku Kibondo mpaka Kasulu. Nikamuuliza silaha ipo? Akasema hana ila kuna mtu anayo nikitaka inapatikana. Nikamwambia basi hamna shida tuliachana na baada ya siku 3 alinifata na kuniambia wanaenda chimbo, yaani kutesa rizki za watu. Mi nikamwambia hizo za pesa ndogo achana nazo naendelea kusoma mazingira. Wao walienda na walifanikiwa kweli kutesa rizki.

Alivyorudi nikamwambia anifanyie mpango wa silaha kuna chimbo naenda namimi kutesa rizki. Tulienda nae nikachukua silaha na kuondoka jioni nikampitia nikamwambie twende kuna hela za kutosha, tulipofika mitaa ya Kanyamhela yeye alikuwa anaendesha pikipiki mimi nyuma amenipakia nilimpiga na kitako cha bunduki kwa nguvu pikipiki iliyumba tukaanguka wote chini, nikamsogeza pembeni ya barabara na kurudi kule kule kwake nikamvamia mkewe nakuwapora hela zote ambazo zilikuwa kama milioni 1 na chenchi kidogo.

Mimi nikaamua sasa kukimbia na ile silaha niliitupa. Hapo ni usiku ukumbuke.

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Good afternoon brothers and sisters 👋

Based on a true story!
Mimi nafanya kuiwasilisha kwenu, hivo fuatana nami mpaka mwisho.

Mimi naitwa Alphonse ni kijana niliezaliwa miaka 36 iliyopita yaani 1986 huko mkoani Kilimanjaro katika hospital ya KCMC. Kwetu tupo watatu mimi na dada zangu wawili, wa kwanza Anna alizaliwa 1988 na mwingine Agness alizaliwa 1992. Baba ni mchaga wa rombo useri na mama ni mchaga wa marangu kirua. Baba alikuwa mfanyabiashara mkubwa hapa jijini Arusha wa vitambaa maeneo ya kilombero na mama yeye alikuwa mtumishi yaani mwalimu katika shule ya Arusha Secondary School kifupi Arusha sec. Tulikuwa tukiishi sakina maeneo ya silentini ndipo wazazi walipojenga.

Maisha yetu kwa kweli yalikuwa mazuri sana hapakuwahi kuwa na shida nyumbani upendo ulitawala na ndugu walitupenda sana na kila tukifunga shule basi bibi wa huko kijijini wa pande zote kila mmoja alikuwa anang'ang'ania tukakae kwake. Shule tulisoma nzuri mimi nakumbuka nilisoma st. Constantine iliyopo Arusha, shuleni tulienda kwa school bus na kurudi kwa school bus. Hata shuleni kulikuwa na tour za kwenda mbuga za wanyama mbali mbali na vivutio vingine nchini.

Kwa kweli shida sikuwahi kuzijua maana nyumbani tulikuwa hatuli maharage na dagaa maana mama alikuwa na vidonda vya tumbo. Nakumbuka hata nguo nlikuwa nafuliwa na dada wa kazi ambaye alikuwa mwenyeji wa Singida. Asubuhi ilikuwa lazima tule cornflex na maziwa. Nilikuwa mtoto wa geti kali hata kucheza ni ndani kwa ndani tu.
Mwaka 1995 nakumbuka nikiwa shule alikuja mjomba shule hivyo niliitwa ofisini kwa mwalimu mkuu nakuambiwa nirudi nyumbani. Tuliondoka na mjomba kwenye gari aina pegeout mpaka nyumbani ambapo kulikuwa na watu wengi tayari, sikujua nini kinaendelea kwa hiyo mimi na wadogo zangu tulikuwa na mjomba muda wote, ndipo baadae alipokuja baba mkubwa na kutuambia baba na mama hawapo tena! Mdogo wangu aliuliza wamesafiri watarudi lini? Alijibiwa hawatarudi tena na sasa ninyi ni jukumu letu.

Mimi sikuielewa na hakuna ambaye pia alielewa tukazidi kuhoji na tuliambiwa tu wameenda mbinguni kwa Mungu. Bado kwetu kuamini na kuelewa ilikuwa ngumu lakini tulienda kuzika Rombo na huko tulilia sana ila mdogo wetu wa mwisho Agness yeye wala hakulia ni kama alikuwa haelewi kinachoendelea. Mazishi yalikamilika hakuna aliyekuwa na nawasi wasi sana ila ndio hivo tulishabaki yatima bila kujijua.

Kilichobaki hapo ni mgawanyo wa mali na kwa mila zetu mimi ndio nilimikishwa mali zote za Mzee ikiwemo mashamba huko Rombo na nyumba hapo sakina. Na huko Rombo pia mzee alijenga nyumba yake. Kule kwa mama kirua pia napo mzee alimjengea mama mkwe wake nyumba.

Basi baba mkubwa ambaye alikuwa akiishi dar kwa wakati huo alisema angetuchukua tukaishi kwake huko dar na kwamba angetusomesha mpaka tutakapokuwa. Ile nyumba baba mkubwa alisema isiuzwe bali waishi ndugu zetu nayeye pia akiwa anakuja arusha aweze kufikia huko.

Sikuwahi kujua kuhusu hati ya nyumba, mafao yoyote ya mama maana alikuwa mtumishi na wala kujua kama mzee alikuwa na hela benki au akiba yoyote. Mzee alikuwa na magari 3 pegeout ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kupeleka abiria namanga, defender 110 ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kubeba abiria kutoka mererani kaza moyo kupitia mbuguni mpaka arusha mjini na staut nyeupe ambayo ndio alikuwa akiiendesha yeye katika shughuli zake ilikuwa ikimsaidia sana. Ila baba na mama walipata ajali ndani ya hiyo staut maeneo ya mto nduruma na umauti kuwafika hapo hapo!

Pegeout alibaki nayo mjomba akiendelea na ruti za namanga na ile defender 110 baba mkubwa aliipeleka kijijini ikafanye kazi ya kubeba maziwa na kuleta moshi mjini. Statut ilibaki imekaa juu maye na ilichinjwa ikauzwa.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatilia mkasa huu wa maisha ya kweli unaosisimua na kutoa machozi.
Kwanini mnaleta vistori vya kipumbavu ambavyo havina kichwa wala miguu, eti itaendelea nani alikulamisha uilete huku. Shenz.
 
Back
Top Bottom