Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re- examination, Makam Mwenyekiti Bara John Heche.

Mhe. Lissu: Ulionyeshwa video ukaulizwa kama ni wewe na kama hayo maneno yanaelekea kuwa ni ya kwako na ukasema hukumbuki kutoa hotuba ya aina hiyo.

Heche: Sikumbuki kutoa hotuba hiyo, wametumia akili mnemba kuitengeneza.

Mhe. Lissu: Fafanua Akili Mnemba

Watu kicheko😂😂😂😂

Heche: Akili Mnemba ndio Artificial Intelligence (AI)

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu magari manne ya bei mbaya ukasema una magari mawili, fafanua.

Heche: Nilimaanisha nina Prado na Hilux ambazo ndo huwa nazitumia, hiki ndo nilichomaanisha.

Mhe. Lissu: Unakumbuka kuhusu kukamatwa kwako nje ya Mahakama na kuwa unapelekwa Tarime, Uliulizwa ulienda Kenya? Ukasema nilizuliwa, fafanua.

Heche: Nilizuiliwa na immigration kwenye mpaka wa Sirari.

Mhe. Lissu: Unakumbuka uliulizwa na mawakili wa Serikali kuhusu wewe kukutana nao Oysterbay Police na walisema kwamba 70% ya waliokamatwa walikutaja wewe kuwa unahusika na kuratibu wewe hizo vurugu, ukasema hujui , fafanua.

Heche: Nilikuwa ndani tangu tarehe 22 Oktoba 2025 kwa vyovyote vile siwezi kuhusika na yaliyotokea Oktoba 29, 2025.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu matibabu yangu hasa kuhusu matibabu nje ya nchi, ulijibu kwamba wakili wa Serikali alikuwa sahihi nusu na sio sahihi nusu, Fafanua

Heche: Kuna mazingira ambayo Mbunge anaweza asifuate utaratibu wa kawaida, mfano mazingira kama ya dharula.

Mhe. Lissu: Uliulizwa ni lazima Mbunge mpaka apate referral kwenda nje ya nchi? Ukasema sio lazima apate refferal

Heche: Mbunge akiwa mahututi sio lazima apewe referral

Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji muda umeisha hivi sasa ni saa kumi na moja tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji huyu John Heche ndio shahidi wangu wa mwisho kwa ambao ni raia, Kwahiyo kesho tutamaliza sio zaidi ya lisaa kwahiyo naomba kesho mashahidi wengine kesho waje ili niongee nao kujua namna tunavyoenda na ushahidi uliobaki.

Watu kicheko😂😂😂😂😂😂

Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi, shahidi bado hujamaliza kutoa ushahidi wako.

Imepigwa High Cooooouuuuuurrrrrtttt

Majaji wanatoka

Tukutane kesho saa tatu kamili asubuhi✌️

TUKUTANE KESHO ASUBUHI MAHAKAMANI.
Mh Lissu amefukia mashimo vizuri sana. MaCCM yalidhani yatachekewa. Mapuuzi makubwa! Bunch of twits!
 
Sema na taarifa zake za kibenki kuweka wazi kinyume na sheria.
Yes. Ndo nimesema hapo kitendo cha yeye kukana kumfahamu Salman ndo kumepelekea ongezeko la maswali mpk kuanikwa taarifa zake za kibenki kinyume na sheria.
Kwani angekiri tu kuwa anamfaham kungekuwa na shida gani?
Au kwa kuwa sijui sheria?
 
Ahsante, Manyanza weka simu full charge tuwaone Mashahidi makamanda wa TAL!
 
Kosa alilofanya Heche katika siku mbili za meanzo za kufanyiwa cross examination, alijaribu kuwa Muungwana, lao amebadilika, aneamua kwenda na Katuga vile anavyokuja matokeo yake ni Katuga kupaliwa, alichosnza nacho Heche leo ndiyo kile alikifanya Brenda Rupia
Katika mashahidi waliozingua ni Brenda Rupia. Hata Heche ashukuru Mshitakiwa jana kusema shahidi amechoka kesi ikaahirishwa, na inaonekana baada ya hapo alienda kutulizwa na kupewa maarifa zaidi. Jana Heche alibanwa vibaya na ndo maana leo baadhi ya maswali mengi amesema hajui.

Alichotaka kuharibu leo ni kumpanikia wakili wa Serikali mchana kabla ya mapumziko.mshitakiwa ana maarifa mengi ila ni kama hajawapa vijana wake na baadhi ya viongozi wake ukiacha Mnyika.
 
Lissu akitaka mashahidi wake ambao sio raia mahakamani watu wote wanacheka mpaka majaji, shida nini?

😂😂
Mimi nimecheka sababu naamini wakitokea kwenye witness stand, wanaenda kuiacha uchi serikali, vyombo vyao na wao binafsi.
Hivyo kicheko changu baada ya Lissu kuwataka mashahidi wake ni kumaanisha "hawawezi kwenda katu"!
 
Wanafiki nyie tunawajua tabia yenu, mnyika alifanya kazi nzuri ndio, mbona hamkumsifia siku ile mnamsifia leo?

Sio wewe uliyeshikia bango elimu ya mnyika ile siku?

Unataka nikutafsirie unachojaribu kufanya hapa? Manipulation za kitoto.

Ukweli ni kwamba mlikuwa mmemkamia Heche, and so far mpaka hapa hajawapa mnachotaka, you are all dissapointed, mnaokoteza vi kitu kitu kumdiscredit.

Mimi sijawai kuwa mnafiki
Tafuta ule John Mnyika akifanyiwa Dodoso
Nilimsifia tangu ile siku ✍️
 
Ila tusimlaumu Heche, ht ungekuwa kwa maswali ya Katuga ungechemka tu...
Wala nisingechemka, angechemka katuga na kujiona fala yeye pamoja na lectures wake wa MU kina Kinemo 😹😹
 
Baada ya kucheka cheka mkumbuke kununa kupo mbele ya Safari 🤔

Nassoro Katuga siku kafunga Ushahidi kwa mtu wa 16 au 17 napo mlicheka na kuimba halleluyaaah

Lkn kikafata kilio 😭😭

Nasasa endeleeni kucheka
sana maumivu yupo njiani
kwenu✍️
 
Heche hata interview zake za kwenye tv huwa anapenda aongee yeye tu huwa hapendi challenge, sasa hapo akae akijua ni Mahakamani sio sehemu ya kubwata

hamkutegemea hali ingekuwa hivi, mlishajiaminisha kuwa mnajua sheria kuliko wengine, kama mnajiamini kwann mnakataa video yenu ya east africa?
Video yetu na nani?
Sasa Katuga anajua sheria au wewe kipofu?

Kwa maswali yasiyo na kichwa wala miguu we umemuona anajua? 😹😹😹

Ndiomana tunachelewa kupata katiba mpya sababu ya wajinga kama nyie..!!
 
Mimi nimecheka sababu naamini wakitokea kwenye witness stand, wanaenda kuiacha uchi serikali, vyombo vyao na wao binafsi.
Hivyo kicheko changu baada ya Lissu kuwataka mashahidi wake ni kumaanisha "hawawezi kwenda katu"!
Kasheshe hapo!

Waje kwa kweli ili siku nyingine wakitaka kumfungulia mtu kesi waonane na wanasheria kwanza washauriwe vizuri.
 
Na wasipokuja, Lissu atadai kanyimwa haki yake ya kujitetea.
Majaji watatoa hukumu dhidi yake bila ya kuwasikiliza mashahidi wake?
 
Yes. Ndo nimesema hapo kitendo cha yeye kukana kumfahamu Salman ndo kumepelekea ongezeko la maswali mpk kuanikwa taarifa zake za kibenki kinyume na sheria.
Kwani angekiri tu kuwa anamfaham kungekuwa na shida gani?
Au kwa kuwa sijui sheria?
Chukulia nimemtuma mdogo wangu akuwekee pesa kwenye akounti yako 10m kama tulivyokubaliana then mdogo wangu aka andiko Jina lake moja ya Salman.
Wewe unanijulisha kuwa umeona 10m kutoka kwa Salman nakujibu ndiyo imetoka kwangu.
Baada ya miaka miwili unaulizwa kama unamfahamu Salman unajibu kuwa unamfahamu?
 
Back
Top Bottom