Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

Ndugu wakuu naomba update ya jana.
 
Katuga, mbona km anatoka nje ya msingi was case, maana anahoji mambo binafsi ya Heche , ndivyo alivyotumwa kuja kuharibu credibility ya heche? Basi amenoaaa.
Watu tuko na Heche hadi kucheeee.
Anatembea na upepo/uzushi wa nje, inaonyesha ni kampeni halali inayojulikana
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 5.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama Mwenyekiti ambaye ni Tundu Lissu alitaka au hakutaka hotuba yake ya 03 April 2025 iwafikie umma?

Heche: Siwezi kujua.

Nassoro Katuga: Ni kweli au siyo kweli siku hiyo ya 03 April 2025 kuna mambo ya ndani yalifanyika huku waandishi wa habari wakiwa wametolewa?

Heche: Sikumbuki.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama Mwenyekiti alikuwa na uwezo au hakuwa na uwezo wa kuwaondoa waandishi wa habari katika mkutano?

Heche: Aliyewaita waandishi wa habari ni Brenda, sasa anaitaje waandishi wa habari?

Nassoro Katuga: Sasa alikuwa na uwezo au hakuwa nao?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulishuhudia au kuona Mwenyekiti akilazimishwa kuingia mbele ya waandishi wa habari?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unafahamu au hufahamu palikuwa na hotuba rasmi au hotuba aliyoandaliwa?

Heche: Sifahamu.

Nassoro Katuga: Ndugu Shahidi, mikutano ya CHADEMA huwa ina hifadhi minutes au haina minutes?

Heche: Kuna mikutano ambayo ni rasmi, vikao vya katiba, warsha na mafunzo.

Nassoro Katuga: Je, kuna minutes?

Heche: Siyo yote.

Nassoro Katuga: Nani alikuwa Mwenyekiti wa mkutano wa tarehe 03 April 2025?

Heche: Haukuwa na Mwenyekiti.

Nassoro Katuga: Nani alikuwa mzungumzaji mkuu wa mkutano?

Heche: Alikuwa Mwenyekiti.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Ndugu wakuu naomba update ya jana.
 
Asante sana mkuu. Ngoja nikaishi nayo.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6.

Nassoro Katuga: Katika huo mkutano, wewe kama wewe uliongea?

Heche: Niliongea.

Nassoro Katuga: Ni muda gani?

Heche: Kama nusu saa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisema hapa Mahakamani wewe uliongea nini siku hiyo.

Heche: Sikusema.

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia akisema tutazuia uchaguzi.

Heche: Ndiyo, nilisikia.

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia akisema tutauvuruga uchaguzi.

Heche: Ndiyo, nilisikia .

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia akisema tutahamasisha.

Heche: Ndiyo, nilisikia.

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia akisema tutakinukisha vibaya sana.

Heche: Ndiyo, nilisikia.

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia akisema Majaji ni MaCCM.

Heche: Ndiyo, nilisikia.

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia alisema Mahakamani hakuendeki.

Heche: Ndiyo, alisema.

Nassoro Katuga: Wewe kama wewe, waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisikia alisema Polisi waliingiza kura feki.

Heche: Ndiyo, alisema.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua au hujui kama Tundu Lissu anashitakiwa kwa kesi ya kutoa taarifa za uongo.

Heche: Kesi najua, ila mashitaka siyajui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa kama unajua kuwa katika hiyo kesi ya Kisutu anashitakiwa kwa kusema Majaji ni MaCCM.

Heche: Sijui ila nakubaliana nawewe kuwa majaji ni maccm.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua ushahidi wako huu unaweza kutumika katika kesi ya Kisutu.

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Je, palikuwa na Polisi ndani ya Mkutano Mkuu wa uchaguzi?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama Polisi siku ya Mkutano Mkuu waliingiza kura ili wewe ushinde.

Heche: Hakuingiza kura ili nishinde.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa sheria nchini Tanzania, nani anahusika kutangaza tarehe ya Uchaguzi Mkuu?

Heche: Ni Tume ya Uchaguzi Mkuu.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, Kikatiba Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapotekeleza majukumu yake haipaswi kuingiliwa, iwe na Serikali au mtu yeyote.

Heche: Inapaswa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua au hujui hayo yamesemwa katika Katiba Ibara ya ngapi?

Heche: Ibara ya 74.

Nassoro Katuga: 74 ngapi?

Heche: Nipe nisome yote.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa kama unajua au hujui kwamba CHADEMA inaamini demokrasia ya vyama vingi.

Heche: Sahihi kabisa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua au hujui No Reforms No Election ni msimamo wa CHADEMA.

Heche: Ni sahihi kabisa.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua au hujui kuwa CHADEMA ina haki ya kushiriki au kutoshiriki Uchaguzi Mkuu.

Heche: Ndiyo, najua.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua, mbali na CHADEMA kuwa na No Reforms No Election, kwanza kuna vyama vingapi vilivyosajiliwa?

Heche: Vingine majina tu, vyama serious ni viwili.

Nassoro Katuga: Kuna vyama vingapi vilivyosajiliwa?

Heche: Vilivyosajiliwa ni 19.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unajua au hujui hivi vyama vingine, ulitoa CHADEMA, vina misimamo yao?

Heche: Inawezekana, ila msimamo wao hautofautiani na ccm


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Nipo siti ya mbele ndugu zangu kwa ajili ya kufuatilia kwa ukaribu hii kesi ya uhaini wa mchongo. Uhaini uliohamia kwenye umiliki wa magari, miamala binafsi ya kifedha, majina ya wanafamilia, nk.

Hizo fedha na miamala ndizo walizotumia hao vichaa kuwarubuni wale vijana na kuwanunulia pombe ksha wakawahamasisha waingie road kuichoma nchi

Wewe fanya masihara lakini hapo watu hawataniii...huyo kichaa wenu kifungo kiko pale pale
 
⚖️ UPDATED CUMULATIVE ASSESSMENT

🔴 KUNYONGWA MPAKA KUFA— 98%
🟢 KUACHIWA HURU— 2%

NI VEMA APIGWE MITI KWANZA LAKINI KABLA YA KUMPIGA KITANZI

MTU KAMA HUYO KICHAA LISU INABIDI AONDOKE DUNIANI BILA CLEAN SHEET KENGE HUYO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…