Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

Ni kawaida tu, Mvumilieni katuga ni wakati wake wa kuwaonesha mabwana zake kuwa anaupiga mwingi.

Aiseee ukiwa upinzani unatakiwa uwe na roho ngumu kweli kweli, haya ya katuga ni tone tu.

Mahakamani ukiona judge hajasema kitu achana nalo, Japo sote tunafahamu kuwa majaji wana upande.
Unaweza nisaidia nielewe kidogo binti kiziwi

Jamuhuri walishamaliza kutoa ushahidi,

izi ma videos katuga analeta tangu jana na Bank statements si ni kama vile ushahidi mpya ?🙄

wanaruhusiwa kuleta ushahidi mpya kesi ipo kwenye progress?
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 8.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama uliwahi kutembelea East Africa Radio na kutangazia umma kwamba siyo tu CHADEMA haitoshiriki, bali uchaguzi hautofanyika.

Heche: Sikumbuki.

Nassoro Katuga: Kwa kuwa hukumbuki, upo tayari kukumbushwa kupitia nyaraka hiyo ya East Africa Radio au haupo tayari?

Heche: Msimamo wangu ni kwamba sipo tayari. Huo si uaminiko, unabambikia kesi.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi kwamba unaogopa, haupo tayari kwa sababu unajua ulichozungumza?

Heche: Sipo tayari kwa sababu documents zako ni feki.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, kwa ridhaa ya Mahakama hii, naomba nimuonyeshe document inapatikana East Africa Radio.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, upande wa Serikali haupo peke yao katika kesi hii.

Kifungu cha 177 (1 & 2) kinataka kukumbushana kwa maneno yaliyozungumzwa.

Siyo kwa Mashitaka kufanya hivyo, lakini ni shahidi mwenyewe.

Ni kwa shahidi kuomba kusoma kitu alichokisema au kukiandika kabla.

Waheshimiwa Majaji, kama upande wa Mashitaka wanataka kutumia hicho walicho nacho, watumie Kifungu cha 163.

“In writing or recorded.”

Hicho wanachokiomba hakipo, Waheshimiwa Majaji.

Nimemaliza, Waheshimiwa Majaji.

MAJAJI WANATETA.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?

Nassoro Katuga: Kinachoendelea ni cross-examination. Umuhimu wake ni Kifungu cha 164 cha Sheria ya Ushahidi.

Kinazungumza nini? Kazi ya cross-examination:

  • Kuangalia uadilifu wa shahidi.
  • Kuangalia ukweli wa shahidi.
  • Kumjua shahidi ni nani.
  • Na kumshake credibility yake.

Kifungu cha 156 (2) cha Sheria ya Ushahidi ndiyo kinaelekeza examination-in-chief lazima ijikite kwenye relevant issues.

Waheshimiwa Majaji, shahidi kasema yeye hakumbuki na hataki kukumbuka.

Kwa mujibu wa shahidi, hakuna implication ya Kifungu cha 177.

Kwenye hati ya mashitaka aliomba ajikumbushe na akapewa nyaraka.

Mshtakiwa hakuoinga kwamba electronic evidence ni document katika Sheria ya Ushahidi.

Nimemsikiliza Mshtakiwa eti akiiambia Mahakama kuwa proper provision ni 163.

Waheshimiwa, Kifungu cha 163 ni cross-examination katika statement na lazima iwe imeandikwa na yeye na lazima iwe imezungumzwa.

Sasa Waheshimiwa, sisi cross-examination yetu inatokana na nyaraka yetu ambayo tunaimiliki.

Halafu Waheshimiwa Majaji, Mahakama hii tukufu utaratibu huu imeshautolea maamuzi jana.

The Court cannot kutoa maamuzi ambayo yanajicontradict na jana.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Katuga anatawala dimba la kati
 
TUNDU LISSU ANAWAFUNDISHA SHERIA KIDOGO HAPA MAHAKAMANI.


SEHEMU YA 9.

Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, utaratibu tunaofanya ni utaratibu tunaofanya kila siku katika practice, na tunaomba tuendelee na cross-examination, Waheshimiwa.

Jaji: Naomba turejee kwenye kanuni ya cross-examination. Shahidi aendelee kuulizwa maswali ya dodoso.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, lakini mimi sijajibu.

Jaji Ndunguru: Heee, wewe ndiyo uli-object?

Lissu: Ndiyo.

Waheshimiwa Majaji, Kifungu cha 164 hakiruhusu kufanya wanachofanya.

Kifungu cha 164 kinazungumzia namna ambavyo shahidi anaweza kuwa cross-examined.

Siyo namna ya kumkumbusha shahidi document yake.

Juu ya kumkumbusha ni Kifungu cha 177, na shahidi mwenyewe ndiyo anayeiombea, siyo Wakili wa Serikali.

Waheshimiwa, vilevile Wakili wa Serikali anasema anaruhusiwa kuuliza swali lolote katika 156(3).

Hoja siyo kuuliza chochote.

Anachoombwa ni kumkumbusha ushahidi under 177.

Kama anataka kukitumia anachotaka kukitumia, lazima atumie 163.

Matumizi ya nyaraka ambazo hazijapokelewa na Mahakama.

Hawawezi kwenda kwenye 164 kwa sababu haizungumzii matumizi ya document.

Anachotaka kukifanya kimekatazwa kabisaaaaa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Kwa hiyo Lissu na Heche wanaiogopa hiyo document? Kwa hiyo anajua kabisa kuwa maneno aliyoyasema ni makosa na ndo sababu hawataki wakumbushwe. Kosa lipo ila wanacheza na sheri kuzuia isiwasilishwe.
Sitaki kabisa wanangu wasome sheria
 
Hakukataa kushinda maana alishinda kweli, lakini ilitumika nguvu ya umma kuhakikisha anatangazwa, hapo ndio tatizo lilipo. Kwanini itumike nguvu badala ya kuheshimi matokeo ya kweli ya box la kura?
Kwahiyo baada ya kutumika nguvu ya umma ndio ukawa Uchaguzi Huru na Haki? Ahahahahaha!
 
Hizi ngonjera za mahakama sio ajabu mtu asie na hatia akafungwa maana kuna janja janja za maswali na majibu kama hii ndio maana ya demokrasia bora isiwepo
Mkuu relax hayo maswali na majibu ndivo mahakama zote wanavoulizana ili kupata wanachoshtakiana.
Mahakama haipo kama siasa.
Wacha wasumbuane sisi mwishoni tutajua hukumu.
 
Ni kawaida tu, Mvumilieni katuga ni wakati wake wa kuwaonesha mabwana zake kuwa anaupiga mwingi.

Aiseee ukiwa upinzani unatakiwa uwe na roho ngumu kweli kweli, haya ya katuga ni tone tu.

Mahakamani ukiona judge hajasema kitu achana nalo, Japo sote tunafahamu kuwa majaji wana upande.

Duuuh mbona hatarii kabisaa, yaan mie najiona hapo ningeishia kuwachamba toka mawakili hadi majaji wenyewe, siwezi vumilia upuuzi.
 
Mkuu relax hayo maswali na majibu ndivo mahakama zote wanavoulizana ili kupata wanachoshtakiana.
Mahakama haipo kama siasa.
Wacha wasumbuane sisi mwishoni tutajua hukumu.
Ni mitego ya maswali hamna la maana kwa shahid in fact wanacheza na maneno ukishindwa kimekulamba hapa mjanja ndio mshindi na inaweza kuwa mwenye haki akashindwa
 
Duuuh mbona hatarii kabisaa, yaan mie najiona hapo ningeishia kuwachamba toka mawakili hadi majaji wenyewe, siwezi vumilia upuuzi.
Kuna adhabu za kuwachamba 🤣 (kuleta fujo)

Ndio maana katuga anasisitiza mahakama sio mama yako, na wenyewe wanamjibu sio mama yako pia.

Mahakamani nyie pasikieni tu (Mashahidi wa Lissu wamefanya kazi kubwa, considering walikuwa wanasubiriwa kwa hamu) Lissu mwenyewe huwa anawatania mashahidi wake kuwa mnaliona lile jopo pale? linawasubiri kwa hamu 😀
 
Unaweza nisaidia nielewe kidogo binti kiziwi

Jamuhuri walishamaliza kutoa ushahidi,

izi ma videos katuga analeta tangu jana na Bank statements si ni kama vile ushahidi mpya ?🙄

wanaruhusiwa kuleta ushahidi mpya kesi ipo kwenye progress?
Rafiki wanaojua mambo ya mahakama na sheria watakuja kukupa muongozo, binafsi nafatilia kesi na kujifunza kama wewe, Japo nafahamu clue chache zile generic

Aione Chivundu
 
TUNDU LISSU ANAWAFUNDISHA SHERIA KIDOGO HAPA MAHAKAMANI.


SEHEMU YA 9.

Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, utaratibu tunaofanya ni utaratibu tunaofanya kila siku katika practice, na tunaomba tuendelee na cross-examination, Waheshimiwa.

Jaji: Naomba turejee kwenye kanuni ya cross-examination. Shahidi aendelee kuulizwa maswali ya dodoso.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, lakini mimi sijajibu.

Jaji Ndunguru: Heee, wewe ndiyo uli-object?

Lissu: Ndiyo.

Waheshimiwa Majaji, Kifungu cha 164 hakiruhusu kufanya wanachofanya.

Kifungu cha 164 kinazungumzia namna ambavyo shahidi anaweza kuwa cross-examined.

Siyo namna ya kumkumbusha shahidi document yake.

Juu ya kumkumbusha ni Kifungu cha 177, na shahidi mwenyewe ndiyo anayeiombea, siyo Wakili wa Serikali.

Waheshimiwa, vilevile Wakili wa Serikali anasema anaruhusiwa kuuliza swali lolote katika 156(3).

Hoja siyo kuuliza chochote.

Anachoombwa ni kumkumbusha ushahidi under 177.

Kama anataka kukitumia anachotaka kukitumia, lazima atumie 163.

Matumizi ya nyaraka ambazo hazijapokelewa na Mahakama.

Hawawezi kwenda kwenye 164 kwa sababu haizungumzii matumizi ya document.

Anachotaka kukifanya kimekatazwa kabisaaaaa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Ngoja Lissu awanyooshe kmmamae zao!
 
Back
Top Bottom