Kutoka Maktaba: Profesa Assad akisifia mradi wa Bwawa la Nyerere

Kutoka Maktaba: Profesa Assad akisifia mradi wa Bwawa la Nyerere

Lumumba nilijua tu mtaenda kumfukua huyo mzee maktaba mpaka mumpate, ok leo zamu yenu kushangilia.
Sidhani kama Assad alikuwa anaongea kwa ridhaa yake. Angekataa kusifia lazima angehojiwa uraia wake au kwenda kusikojulikana kama wengine.
 
Kwahiyo hapo alishikiwa bunduki lakini kuomba mikataba ya ATCL, SGR n.k alikuwa huru? Ni muongo yule!
Mbona husemi kitu gani kilitokea alivyoomba mikataba? Si walimkatalia. Lazima atakuwa alilazimishwa kusifia hìi miradi.
 
Kwa yanayoendelea ni obvious kuna mkakati mahsusi wa kumchafua JPM!
Kumchafua kwa lipi?
Wafanyabiashara hatukutekwa?
Wafanyabiashara hatukubambikiwa kodi ikiwemo kutishwa?
Watu hawakupotezwa kwa kutofautuana mitazamo?
Tuliandika humu tangu 2016 kuwa kuna moja,mbili,tatu,misukule mkakata kuwa si kweli,hayatokei hayo.
Leo ukweli mchungu umewekwa hadharani halafu mnakuja hapa na ngonjera zenu eti "kumchafua JPM".
 
Enzi za teknolojia 'kila nyoka atatafuna mkia wake mwenyewe'..huyu babu ameshindwa kujifunza mzee mwenzake pale bungeni. Njaa ni mbaya sana.
 
Wasomi wa Udsm ni vinyonga.

Unawakumbuka akina Palamagamba Bashiru, Mwigullu Ryoba Kitila nk nk

Na wadogo zao akina Waitara Silinde Zitto, Mdee, Lisu, Matiko nk nk

Yaani ni full ubabaishaji!
Asadi hajapinga Mradi wa umeme bali anapinga ununuzi wa ndege pasipo mipango
Assad alisema hakuna/hakuona upembuzi yakinifu wa mradi wa umeme, kama hivyo ndivyo how could he come to a conclusion kuwa ulikuwa mradi mzuri? Je ubora wa huu mradi uliyeyuka baada ya yeye kutumbuliwa? Assad ni mmoja kati ya hilo genge la Kikwete ambalo limeundwa kwa sababu moja tu kutaka kutetea mradi wa Bagamoyo uwe resuscitated!!

Hakukuwa na economic justification ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo wakati huo na hakuna hivi sasa bali ni Kikwete aliyetaka kutumia URAIS wake kuendeleza sehemu alikotoka!! As to any economic justification Sasa hivi hakuna kabisa hasa ikitiliwa maanani kuwa zanzibar hivi karibuni itaanza kujenga Bandari kubwa hapo Visiwani.
 
Back
Top Bottom