Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna kitu bado hujaelewa na hujanielewa.Nikuulize kitu, unajua maana ya neno bikra?
Na kama unajua maana yake naomba unambie umetumia akili au mantiki gani kulitumia neno bikra kwa mwanaume?
Katika makuzi yako ulishawahi sikia wapi mwanaume katolewa bikra na ametolewa kwa namna gani?
Dah we jamaa umemamazwa balaa yaani inaonekana una influence kubwa sana ya kike kwenye maisha yako. Na nina wasi wasi hapo unatype huku umevaa dera.
Kwanza hapa tunajadili mada na sio mtu binafsi. Tujikite zaidi kwenye mada, kuliko hisia juu ya mchangia mada.
Issue ya bikra, nayo hujaelewa na hujanielewa. Nimeandika neno bikra kwa mwanamke na neno 'bikra' kwa mwanaume. Mantiki ni nini? Sote tunajua bikra iko kwa mwanamke tu, lakini dhana ya kimantiki kuhusu bikra ni kule mhusika kuwa mpya kabisa (naive) kuhusu kufanya ngono. Na hiyo haijarishi ni jinsia gani, na hapo ndipo nikaandika neno 'bikra' nikimzungumzia mwanaume. Yote kwa yote, logic ni ile ile, wewe mwanaume unayeweza kumhukumu msichana kuwa ameshatumika kingono kwa sababu hujamkuta na bikra, jiulize kwanza nafsini kwako pia kama wewe pia hujawahi kufanya ngono hapo kabla.