TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
- Thread starter
- #41
Daaaahh. Inasikitisha sana.Huyo alikosea mwenyewe. Inaonekana alitaka show off kwa wakenya wenzake kwa sababu huko Marekani kila mtu yuko bize na hawajali urubani wako. Mbaya zaidi hakufanya utafiti akirudi ataanzia wapi.
Hii stori IMENIKUMBUSHA ndugu yetu mmoja mwanariadha mkubwa miaka ya 90 hadi mwanzoni mwa 2000. Huyu jamaa alikuwa anafadhiliwa na SAMSUNG na hata baadae akikaribia kustaafu riadha alipata ajira ya kudumu makao makuu ya Samsung, Korea. Akaushtusha umma kwa kuamua kuacha kazi Samsung kwa alichodai Korea kuna baridi sana pia yuko mbali na familia yake. Ikumbukwe Samsung ilikuwa inalipia tiketi ya kwenda na kurudi kwa ajili ya mke wake na watoto wao wawili mara tatu kwa mwaka.
Jamaa akarudi Arusha. Mwanzoni alikuwa kama mfalme kwasababu ya pesa. Ila kadiri muda ulivyoenda pesa pia ikawa inakata. Alivyofikia level ya kuanza kutembea kwa mguu mke naye akaanza kumsaliti kwa kutembea na rafiki wa jamaa. Jamaa alidhoofika kuanzia kiuchumi hadi kisaikolojia kwa sababu haikuwa siri tena kwamba anachapiwa. Mwaka 2009 tulimpoteza mtu wetu kwa kifo cha ghafla.
Ninadhani ukienda nchi kama Marekani yenye utulivu halafu maisha yakakunyookea endelea na maisha hukohuko. Labda kama umeenda DRC, Afrika ya kati au nchi nyingine ya kishenzi ukabahatisha pesa ni sawa kurudi nyumbani.
Kufanya maamuzi kihisia zaidi, unataka tu kurudi nyumbani, unasahau mazingira huko nyumbani yakoje? Umejiandaaje?