Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

. Lakini Samuel aliona kubaki Marekani ni usaliti kwa jamii yake na kanisa lililomsomesha.

Hana mawasiliano na mkewe wa Marekani wala watoto wao wawili kwa miaka mingi sasa. Anajua kwamba wanae kwa sasa ni watu wazima na huenda hata akikutana nao wasimtambue, lakini hajakata tamaa.
Yea something's not right here.

Kwanini kanisa limewekwa hapo! ! ! Bora ungesema tu wafadhili wako usitaje kanisa, msitake kufanya wa tu wa kanisani kama hawana akili timamu.

A man of GOD's hierarchy of priorities is : his GOD, his marriage, his children.

So how is you coming to be a pilot in your home country a service to GOD, your marriage, or your children? ? ?

Sorry but I think this man sacrificed all that for his own desires: he wanted a name, a status among his people.
 
Wanawake wetu hawa ukishakuwa Huna mbele wala nyuma anakukimbia mbio nyingi haangalii potential, ukiwa Huna kitu huwaoni, wanawake wa kizungu wanajua kusoma potential ya mtu, hata kama huna pesa nyingi lakini kuna potential anaiona kwako basi utakuwa naye ili ukija kutoboa mgawane mbao vizuri....Halafu kiherehere cha yeye kwenda Kenya kimemponza, mkewe aliona kabisa Kenya hatutoboi kule, mifumo migumu.
The issue is hakuwa well informed kuhusiana na mambo ya aviation nchini Kenya. Aliamini kwa ujuzi alionao huko Marekani kungempa credibility ya kuingia kwenye ajira moja kwa moja. Huyo mke wake wa kwanza mzungu inavyoonekana alimwambia afanye tathmini vizuri kuhusu mazingira ya nyumbani kabla ya kuchukua maamuzi ila uharaka na pressure aliyokuwa akiipata toka hilo kanisa lililomsomesha ndio vilimcost. Pole yake sana mzee wangu
 
Mtaji hana kivipi?kwa nini alipe ada ambayo haitoshelezi masomo si ndio kachezea mtaji hapo?alijua nani atamlipia hizo pesa zingine?
Huyu kuna kitu hakijasemwa. Marubani wengi ninkawaida ukikaa muda fulani au ukibadili aina ya ndege kuna kozi fupi unaenda. Hizi kozi fupi mashirika mengi ya ndege huwa yanawalipia. Kuna kitu hakisemwi hapa.
 
Ndiyo maana wachache walioshtuka mapema, waliwekeza fedha/assets zao kwa majina ya ndugu zao hasa Baba/Mama zao

Jambo la kujifunza hasa kwetu wote, ni kuwa na uwezo wa kuwekeza kwaajili ya Uzee wetu

Kuna watu wanahisi wataendelea kuwa Vijana miaka yao yote, kumbe ukifika 40 tu tayari unauanza Uzee kwa kasi

Mkitaka kubisha hilo, angalia ulikuwa unaenda round ngapi kwa mpenzi wako miaka 10 iliyopita, na sasa unaenda ngapi

Kama sisi Wazee wa mwaka 47, ndiyo basi tena 🙌
 
Hii ni hadithi ya maumivu ya ndugu Samuel Mawato, mkazi wa Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, nchini Kenya.

Samuel hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa muokota makopo. Kwa miaka 15 aliyoshi Marekani, ambako alisomea urubani na baadaye kufanya kazi kwa muda mfupi katika shirika kubwa la ndege la American Airlines, hakuwahi kufikiria kwamba maisha yake yangeishia kuokota makopo.
Kabla ya kwenda Marekani, Samuel alikuwa akifanya kazi kama mhudumu wa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi. Hata hivyo, ndoto yake kubwa ilikuwa kuwa rubani. Kwa jitihada na maombi, hatimaye mwaka 1998 alipata fursa adimu ya ufadhili wa masomo ya urubani nchini Marekani kupitia Kanisa la Methodist.

Alijiunga na chuo mashuhuri cha ATP Flight School kampasi ya Arizona. Kwa miaka miwili alijifunza urubani na kupata leseni ya awali ya kurusha ndege binafsi (Private Pilot License – PPL). Aliendelea na mafunzo na baada ya miaka miwili zaidi akapata leseni ya kurusha ndege za kibiashara (Commercial Pilot License – CPL).

Baadaye alipata kazi kama rubani msaidizi (First Officer) katika shirika la American Airlines. Alioa mwanamke wa kizungu na kuanzisha familia. Walifanikiwa kupata watoto wawili katika ndoa yao: wa kike na wa kiume.

Mambo yalianza kubadilika baada ya Samuel kutaka kurudi Kenya na kutumia ujuzi wake kusaidia taifa lake. Walitofautiana na mkewe ambaye hakuwa tayari kuhamia Kenya. Alimtaka Samuel waendelee kuishi Marekani. Lakini Samuel aliona kubaki Marekani ni usaliti kwa jamii yake na kanisa lililomsomesha.

Mvutano huo ulisababisha ndoa yao kupasuka. Mkewe akabaki Marekani na watoto, Samuel akarudi Kenya. Baada ya miaka 15 ya kukaa ughaibuni, Samuel aliamini kurejea kwake Kenya kungekuwa mwanzo wa maisha bora na yenye matumaini. Alipoingia Kenya, akaoa mke mwingine.
Hata hivyo, mambo hayakuwa kama alivyotarajia. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA), rubani aliye somea nje ya nchi hutakiwa kufanya refresher training na kutimiza angalau 200 flight hours ili leseni yake itambulike na kuruhusiwa kurusha ndege kibiashara. Samuel alikuwa ameanza kupungukiwa na fedha, hivyo akachukua mkopo kuweka gari yake rehani ili apate fedha za kushiriki mafunzo hayo.

Fedha alizopata hazikutosha kulipia masaa yaliyohitajika. Zikaisha kabla hajamaliza mafunzo. Benki aliyokopa ikataifisha gari yake baada ya kushindwa kufanya marejesho. Hivyo akapoteza gari na mafunzo hakumaliza. Akiwa katika mtanziko, mkewe (yule aliyemuoa Kenya) akamtoroka.
Maisha yakaanza kuwa magumu. Miaka 15 aliyokuwa Marekani ilitosha kumpotezea baadhi ya marafiki na jamaa. Aliporudi, hawakuwa tena karibu naye kama zamani. Alipojaribu kuwaomba msaada, wengi walimkwepa. Hapo ndipo maisha yakazidi kuwa magumu kwake.

Hatimaye ikamlazimu kufanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani. Alianza kwa kuendesha toroli, lakini kadri umri ulivyosonga ndivyo nguvu zilivyomuishia. Hatimaye akaamua kujikita katika shughuli ya kuokota makopo. Na sasa ameanzisha kikundi kiitwacho Responsible Citizen Initiatives kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa mazingira Kilifi.

Leo akiwa na umri wa miaka 64, Samuel anajikongoja taratibu mitaa ya Mtwapa huko Kilifi akiokota makopo kama shughuli pekee inayoendesha maisha yake. Bado anakumbuka jinsi alivokuwa na imani kwamba uzoefu wake wa ng’ambo ungefungua milango baada ya kurejea nyumbani. Lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia.

Hana mawasiliano na mkewe wa Marekani wala watoto wao wawili kwa miaka mingi sasa. Anajua kwamba wanae kwa sasa ni watu wazima na huenda hata akikutana nao wasimtambue, lakini hajakata tamaa.

Katika umri wa uzee, mwili kudhoofu na maisha ya upweke, bado Samuel analo tumaini. Anaamini siku moja Mungu atampa nafasi ya kukutana na watoto wake, walau awaone tu na kuwakumbatia kabla hajafa. Hilo ndilo ombi lake kubwa kwa sasa.

Je nini maoni yako? Samuel alikosea kurudi Kenya? Samuel hakujipa muda wa kupata taarifa sahihi kabla ya kurudi? Watu wenye vipawa vikubwa na akili nyingi wameshindwa kustawi Afrika kutikana na mifumo mibovu?

Source: Facebook page ya Godlisten Malisa

Ndio mana watu wengi wanakataa kurudi nyumbani baada ya kuishi ulaya kwa.muda mrefu inawezekana ushirikina uliingia hapa kummaliza kuna jamaa mwingine maeneo ya Tanga huko ni kama huyu alikuwa rubani marekani kosa lake alirudi home na ndoto ya kubadili maisha ya wanakijiji we acha tu akaenda tena ulaya ghafla akaeusi tena kijijini akawa mgonjwa na uchizi juu mwisho wake akawa mwizi mpaka kifo africa tuna tatizo kubwa sana tuache kurogana...
 
Back
Top Bottom