Mjusi Sharobalo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2025
- 8,306
- 14,632
Ni kweli kabisa ukijichanganya wnakupasua 😀😀😀Tena muwahi mapema huku hata makopo siku hizi kuna masela wamejiwekea makoloni yako sio unaokotaokota tu

Basi mavuta bangi hayo....yana bahati yanamiliki gamba la nje, kikinuka bongo yanasepa...Bongo yangeishia kuwa machizi and nobody care!Itakuwa hivyo 🤣
Wana passport za ulaya wote wawili
Rubani alikuwa mjinga.Naomba urudie kusoma uzi rafiki,huyu hakuwa msomi huyu ni rubani..."Fikiria kaweka gari bond ili alipie masomo ina maana alikuwa hajui hiyo coz inahitaji sh ngapi?...ni sawa leo wewe utake kusoma MBA uambiwe course yote ni 10M halafu wewe ukaweke bond gari uchukue 5M nini kitatokea?lazima kikurambe......Au walimroga jamani?
Ukizidi umri wa miaka 35 bado unafanya shughuli zako za kimaisha nchi zilizoendelea, kama huna changamoto yoyote ya kimaisha nakushauri rudi Tz kusalimia tu.Nikibahatika kwenda mamtoni nitarudi nikiwa mtu wa makamo uzima ukiwepo,
Uko sahihi. Kenya kugumu mno kupata pesa. Kule hakuna huruma kabisa.Unakujuwa vizuri Kenya? Kuna mzungu daktari alimfata mke wake mkenya, baada ya kukimbia na watoto wake, kaishia kuwa mlevi wa mataputapu, Hana kazi na mke kamkimbia!...maana yangu Kenya ni kugumu mno mno kiutafutaji, ndo maana wakija nje wanafanya kazi kama punda!...msoto wa Kenya sio poa!
Anaefuga njiwa mtu wa bangi sanaBasi mavuta bangi hayo....yana bahati yanamiliki gamba la nje, kikinuka bongo yanasepa...Bongo yangeishia kuwa machizi and nobody care!
Hv kikeke alistaafu ndipo akarudi huku,Ukizidi umri wa miaka 35 bado unafanya shughuli zako za kimaisha nchi zilizoendelea, kama huna changamoto yoyote ya kimaisha nakushauri rudi Tz kusalimia tu.
Hizi familia zetu za kiafrika ni kwikwi asee, zikiona mmojawapo kaenda kiwanja wanahisi unaenda kuokota hela barabarani, kumbe msoto wake ni afadhali aliyeko bongo..mindset ya ovyo kweliNdio mana watu wengi wanakataa kurudi nyumbani baada ya kuishi ulaya kwa.muda mrefu inawezekana ushirikina uliingia hapa kummaliza kuna jamaa mwingine maeneo ya Tanga huko ni kama huyu alikuwa rubani marekani kosa lake alirudi home na ndoto ya kubadili maisha ya wanakijiji we acha tu akaenda tena ulaya ghafla akaeusi tena kijijini akawa mgonjwa na uchizi juu mwisho wake akawa mwizi mpaka kifo africa tuna tatizo kubwa sana tuache kurogana...
Hahahahhahaa...abroad kutoa nyegez bei ghali sana🤣🤣🤣Anaefuga njiwa mtu wa bangi sana
Mwingine yeye na machangudoa ni kama alikuwa na upwiru wa kufa mtu miaka yote aliokuwa ulaya
Si unaona anavyokuwa frustrates hapa? Nafikiri mkataba wake uliisha.Hv kikeke alistaafu ndipo akarudi huku,
Kweli kabisa kiongozi
Mhmm sio kweli , kuna watanzania maelfu wapo kenya na wana maendeleo makubwa sanaUko sahihi. Kenya kugumu mno kupata pesa. Kule hakuna huruma kabisa.
Mkuu hayo maelfu ulihesabu lini?Mhmm sio kweli , kuna watanzania maelfu wapo kenya na wana maendeleo makubwa sana
Wapo kibao mombasa na Nairobi hasa watu wa kilimanjaro ni matajiri wa kubwa mno kenyaMkuu hayo maelfu ulihesabu lini?
Wapo waliofanikiwa ila haiondoi ukweli kuwa Kenya pagumu mno.Wapo kibao mombasa na Nairobi hasa watu wa kilimanjaro ni matajiri wa kubwa mno kenya
Hii ni hadithi ya maumivu ya ndugu Samuel Mawato, mkazi wa Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, nchini Kenya.
Samuel hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa muokota makopo. Kwa miaka 15 aliyoshi Marekani, ambako alisomea urubani na baadaye kufanya kazi kwa muda mfupi katika shirika kubwa la ndege la American Airlines, hakuwahi kufikiria kwamba maisha yake yangeishia kuokota makopo.
Kabla ya kwenda Marekani, Samuel alikuwa akifanya kazi kama mhudumu wa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi. Hata hivyo, ndoto yake kubwa ilikuwa kuwa rubani. Kwa jitihada na maombi, hatimaye mwaka 1998 alipata fursa adimu ya ufadhili wa masomo ya urubani nchini Marekani kupitia Kanisa la Methodist.
Alijiunga na chuo mashuhuri cha ATP Flight School kampasi ya Arizona. Kwa miaka miwili alijifunza urubani na kupata leseni ya awali ya kurusha ndege binafsi (Private Pilot License – PPL). Aliendelea na mafunzo na baada ya miaka miwili zaidi akapata leseni ya kurusha ndege za kibiashara (Commercial Pilot License – CPL).
Baadaye alipata kazi kama rubani msaidizi (First Officer) katika shirika la American Airlines. Alioa mwanamke wa kizungu na kuanzisha familia. Walifanikiwa kupata watoto wawili katika ndoa yao: wa kike na wa kiume.
Mambo yalianza kubadilika baada ya Samuel kutaka kurudi Kenya na kutumia ujuzi wake kusaidia taifa lake. Walitofautiana na mkewe ambaye hakuwa tayari kuhamia Kenya. Alimtaka Samuel waendelee kuishi Marekani. Lakini Samuel aliona kubaki Marekani ni usaliti kwa jamii yake na kanisa lililomsomesha.
Mvutano huo ulisababisha ndoa yao kupasuka. Mkewe akabaki Marekani na watoto, Samuel akarudi Kenya. Baada ya miaka 15 ya kukaa ughaibuni, Samuel aliamini kurejea kwake Kenya kungekuwa mwanzo wa maisha bora na yenye matumaini. Alipoingia Kenya, akaoa mke mwingine.
Hata hivyo, mambo hayakuwa kama alivyotarajia. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA), rubani aliye somea nje ya nchi hutakiwa kufanya refresher training na kutimiza angalau 200 flight hours ili leseni yake itambulike na kuruhusiwa kurusha ndege kibiashara. Samuel alikuwa ameanza kupungukiwa na fedha, hivyo akachukua mkopo kuweka gari yake rehani ili apate fedha za kushiriki mafunzo hayo.
Fedha alizopata hazikutosha kulipia masaa yaliyohitajika. Zikaisha kabla hajamaliza mafunzo. Benki aliyokopa ikataifisha gari yake baada ya kushindwa kufanya marejesho. Hivyo akapoteza gari na mafunzo hakumaliza. Akiwa katika mtanziko, mkewe (yule aliyemuoa Kenya) akamtoroka.
Maisha yakaanza kuwa magumu. Miaka 15 aliyokuwa Marekani ilitosha kumpotezea baadhi ya marafiki na jamaa. Aliporudi, hawakuwa tena karibu naye kama zamani. Alipojaribu kuwaomba msaada, wengi walimkwepa. Hapo ndipo maisha yakazidi kuwa magumu kwake.
Hatimaye ikamlazimu kufanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani. Alianza kwa kuendesha toroli, lakini kadri umri ulivyosonga ndivyo nguvu zilivyomuishia. Hatimaye akaamua kujikita katika shughuli ya kuokota makopo. Na sasa ameanzisha kikundi kiitwacho Responsible Citizen Initiatives kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa mazingira Kilifi.
Leo akiwa na umri wa miaka 64, Samuel anajikongoja taratibu mitaa ya Mtwapa huko Kilifi akiokota makopo kama shughuli pekee inayoendesha maisha yake. Bado anakumbuka jinsi alivokuwa na imani kwamba uzoefu wake wa ng’ambo ungefungua milango baada ya kurejea nyumbani. Lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia.
Hana mawasiliano na mkewe wa Marekani wala watoto wao wawili kwa miaka mingi sasa. Anajua kwamba wanae kwa sasa ni watu wazima na huenda hata akikutana nao wasimtambue, lakini hajakata tamaa.
Katika umri wa uzee, mwili kudhoofu na maisha ya upweke, bado Samuel analo tumaini. Anaamini siku moja Mungu atampa nafasi ya kukutana na watoto wake, walau awaone tu na kuwakumbatia kabla hajafa. Hilo ndilo ombi lake kubwa kwa sasa.
Je nini maoni yako? Samuel alikosea kurudi Kenya? Samuel hakujipa muda wa kupata taarifa sahihi kabla ya kurudi? Watu wenye vipawa vikubwa na akili nyingi wameshindwa kustawi Afrika kutikana na mifumo mibovu?
Source: Facebook page ya Godlisten Malisa
Sio kweli. Huyo jamaa ni upumbavu wake mwenyewe tu.Huyu ni mwanaume wa nne wa kikenya kukumbwa na dhoruba na wanawake wa kizungu, wanawake wa kizungu au wazungu kwa ujumla vichwa vyao vina mushkeli sio kidogo, anaweza kuamka asubuhi akadai talaka na hujamkosea, anachukua mkwanja unaachwa hapo...kibaya zaidi wanapenda ndoa kuzitunza sasa !...ukiwa nae sahau kuwekeza Africa, maana anakuwa ana monitor account yako, ..siku yakikukuta sasa ndo kama hivi, huna chochote Africa!
Yaan ni mwendo wa ngiri mkia juu, full kukukwepa....Tena wanafurahia kishenzi🤣🤣Ha haaaa haaaa hao hao ndio wa kwanza kusema jamaa hakujipanga
Waache wamba wafurahishe mtaa ,kama nawaona hapo itakuwa ni slang za kiswahi_English siku nzimaAnaefuga njiwa mtu wa bangi sana
Mwingine yeye na machangudoa ni kama alikuwa na upwiru wa kufa mtu miaka yote aliokuwa ulaya
Kenya ni pagumu sana kama haujanyooka , ila sisi tuliowahi fanya biashara huko tunajua Urahisi wake Monetary doctorWapo waliofanikiwa ila haiondoi ukweli kuwa Kenya pagumu mno.
Kwa upumbavu wa huyu jamaa muanze kumbebesha mizigo sherani kwa ujinga wa huyuHii ni hadithi ya maumivu ya ndugu Samuel Mawato, mkazi wa Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, nchini Kenya.