Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Huyu kuna kitu hakijasemwa. Marubani wengi ninkawaida ukikaa muda fulani au ukibadili aina ya ndege kuna kozi fupi unaenda. Hizi kozi fupi mashirika mengi ya ndege huwa yanawalipia. Kuna kitu hakisemwi hapa.
Nakubaliana nawe, huwezi kupokelewa moja kwa moja kabla shirika la ndege unaloomba ajira halijawa na imani nawe katika ndege zao. Kuna uwezekano alifeli kwenye course au kuna lolote lililompelekea akashindwa kuqualify
 
Kenya ni pagumu sana kama haujanyooka , ila sisi tuliowahi fanya biashara huko tunajua Urahisi wake Monetary doctor
Naam kenya ni pagumu ila ukielewa mahitaji ya kule unaenda nao vzr sana mfn kule ukauze chips utasota sana wanataka ugali ama githeri na matumbo,, kwenye kilimo sisi tunalimaga mahindi kwa ajili ya kuuza mabichi na wakenya ndo tunawaauzia,
 
hakuwahi kufikiria kwamba maisha yake yangeishia kuokota makopo.
Hayajaishia kwenye kuokota makopo bado,tumpe muda anaweza kutoboa
Kwa jitihada na maombi,
Arudi hapa kwenye njia ya maombi ndipo alipoanzia kufanikiwa
Lakini Samuel aliona kubaki Marekani ni usaliti kwa jamii yake na kanisa lililomsomesha.
Serikali zetu hazithamini kitu kinachoitwa uzalendo alichemka sana, Kuna yule binti wa Mzee Kimiti anaongoza Mamalaka ya Mapato Uingereza huko alitaka kurudi hapa akamwambiwa atapelekwa Kigoma eti😀,

Katika umri wa uzee, mwili kudhoofu na maisha ya upweke, bado Samuel analo tumaini.
Hakika aendelee kuwa na Tumaini
 
Hii ni hadithi ya maumivu ya ndugu Samuel Mawato, mkazi wa Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, nchini Kenya.

Samuel hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa muokota makopo. Kwa miaka 15 aliyoshi Marekani, ambako alisomea urubani na baadaye kufanya kazi kwa muda mfupi katika shirika kubwa la ndege la American Airlines, hakuwahi kufikiria kwamba maisha yake yangeishia kuokota makopo.
Kabla ya kwenda Marekani, Samuel alikuwa akifanya kazi kama mhudumu wa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi. Hata hivyo, ndoto yake kubwa ilikuwa kuwa rubani. Kwa jitihada na maombi, hatimaye mwaka 1998 alipata fursa adimu ya ufadhili wa masomo ya urubani nchini Marekani kupitia Kanisa la Methodist.

Alijiunga na chuo mashuhuri cha ATP Flight School kampasi ya Arizona. Kwa miaka miwili alijifunza urubani na kupata leseni ya awali ya kurusha ndege binafsi (Private Pilot License – PPL). Aliendelea na mafunzo na baada ya miaka miwili zaidi akapata leseni ya kurusha ndege za kibiashara (Commercial Pilot License – CPL).

Baadaye alipata kazi kama rubani msaidizi (First Officer) katika shirika la American Airlines. Alioa mwanamke wa kizungu na kuanzisha familia. Walifanikiwa kupata watoto wawili katika ndoa yao: wa kike na wa kiume.

Mambo yalianza kubadilika baada ya Samuel kutaka kurudi Kenya na kutumia ujuzi wake kusaidia taifa lake. Walitofautiana na mkewe ambaye hakuwa tayari kuhamia Kenya. Alimtaka Samuel waendelee kuishi Marekani. Lakini Samuel aliona kubaki Marekani ni usaliti kwa jamii yake na kanisa lililomsomesha.

Mvutano huo ulisababisha ndoa yao kupasuka. Mkewe akabaki Marekani na watoto, Samuel akarudi Kenya. Baada ya miaka 15 ya kukaa ughaibuni, Samuel aliamini kurejea kwake Kenya kungekuwa mwanzo wa maisha bora na yenye matumaini. Alipoingia Kenya, akaoa mke mwingine.
Hata hivyo, mambo hayakuwa kama alivyotarajia. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA), rubani aliye somea nje ya nchi hutakiwa kufanya refresher training na kutimiza angalau 200 flight hours ili leseni yake itambulike na kuruhusiwa kurusha ndege kibiashara. Samuel alikuwa ameanza kupungukiwa na fedha, hivyo akachukua mkopo kuweka gari yake rehani ili apate fedha za kushiriki mafunzo hayo.

Fedha alizopata hazikutosha kulipia masaa yaliyohitajika. Zikaisha kabla hajamaliza mafunzo. Benki aliyokopa ikataifisha gari yake baada ya kushindwa kufanya marejesho. Hivyo akapoteza gari na mafunzo hakumaliza. Akiwa katika mtanziko, mkewe (yule aliyemuoa Kenya) akamtoroka.
Maisha yakaanza kuwa magumu. Miaka 15 aliyokuwa Marekani ilitosha kumpotezea baadhi ya marafiki na jamaa. Aliporudi, hawakuwa tena karibu naye kama zamani. Alipojaribu kuwaomba msaada, wengi walimkwepa. Hapo ndipo maisha yakazidi kuwa magumu kwake.

Hatimaye ikamlazimu kufanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani. Alianza kwa kuendesha toroli, lakini kadri umri ulivyosonga ndivyo nguvu zilivyomuishia. Hatimaye akaamua kujikita katika shughuli ya kuokota makopo. Na sasa ameanzisha kikundi kiitwacho Responsible Citizen Initiatives kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa mazingira Kilifi.

Leo akiwa na umri wa miaka 64, Samuel anajikongoja taratibu mitaa ya Mtwapa huko Kilifi akiokota makopo kama shughuli pekee inayoendesha maisha yake. Bado anakumbuka jinsi alivokuwa na imani kwamba uzoefu wake wa ng’ambo ungefungua milango baada ya kurejea nyumbani. Lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia.

Hana mawasiliano na mkewe wa Marekani wala watoto wao wawili kwa miaka mingi sasa. Anajua kwamba wanae kwa sasa ni watu wazima na huenda hata akikutana nao wasimtambue, lakini hajakata tamaa.

Katika umri wa uzee, mwili kudhoofu na maisha ya upweke, bado Samuel analo tumaini. Anaamini siku moja Mungu atampa nafasi ya kukutana na watoto wake, walau awaone tu na kuwakumbatia kabla hajafa. Hilo ndilo ombi lake kubwa kwa sasa.

Je nini maoni yako? Samuel alikosea kurudi Kenya? Samuel hakujipa muda wa kupata taarifa sahihi kabla ya kurudi? Watu wenye vipawa vikubwa na akili nyingi wameshindwa kustawi Afrika kutikana na mifumo mibovu?

Source: Facebook page ya Godlisten Malisa

SUBIRI KESHO YAKO MAANA HUIJUI KAMWE
 
Afrika kuna uncertainty zinazo sababishwa na system mbovu. Ndio maana ni ngumu sana diaspora kurudi Afrika.

Nchi za wenzetu kama una ujuzi, Hata upoteze kila kitu, skill yako itakubeba.

Afrika unaweza kuwa na ujuzi lakini kutokana na system mbovu, utakwama.
💯

Watu wengi hawajui madhara ya mifumo mibovu.

Na wengine wanajua madhara ya mifumo mibovu ila sababu inawapa faida hawako tayari kuizungumzia.

Kwa nchi zenye mifumo imara adui mkubwa ni afya ya akili, hata ukipoteza kila kitu so long as una sound mind, resilient ni suala la muda tu.
 
Naam kenya ni pagumu ila ukielewa mahitaji ya kule unaenda nao vzr sana mfn kule ukauze chips utasota sana wanataka ugali ama githeri na matumbo,, kwenye kilimo sisi tunalimaga mahindi kwa ajili ya kuuza mabichi na wakenya ndo tunawaauzia,
Yeah kenya ukiwaelewa una piga pesa kirahisi sana , ukifika Nairobi watu wa nyumbani kama wako kwao na wanafanya makubwa
 
Naam kenya ni pagumu ila ukielewa mahitaji ya kule unaenda nao vzr sana mfn kule ukauze chips utasota sana wanataka ugali ama githeri na matumbo,, kwenye kilimo sisi tunalimaga mahindi kwa ajili ya kuuza mabichi na wakenya ndo tunawaauzia,
Hivi biashara za bidhaa za mage,,,, Tk mpaka sasa zinatamba mkuu?
 
zipo mkuu, kama mahindi mabati na mafuta ya taa ni chapu tuu....
Dah nimekumbuka mbali 😅 hii kitu imenifanya nimekua na maraki kibao kipande cha huko , nasikia miru,,, ni dili la pesa ndefu hicho kipande
 
Yeah kenya ukiwaelewa una piga pesa kirahisi sana , ukifika Nairobi watu wa nyumbani kama wako kwao na wanafanya makubwa
Ewaaah hata code za uvaaji inabidi uende na wanavyotaka mfn kule jinzi, makoti yake ni bull bull sasa wewe fika kule kalete creativity ya vitenge uone 😂

Na ni watu poa wakijua umetoka chini ya mlima wanasema ndugu zenu kutoka nyeri hapo....

Ila hiyo TK ulivyoandka ni una uzoefu aseeh na huko
 
Ila wakenya ni mafighter sana, wakifika abroad hakuna kucheka na kima, ni kazi kazi...tatizo lao wanapenda kuoa wazungu, shida mzungu Kila unachoingiza kinahesabika kama cha familia! Huwezi kuinvest kwenu, na likija balaa la divorce wafwaa!... Kwa wazungu tu hapo ndo weakness ya wakenya!
Nawajua wakenya watatu mmoja kaowa mganda mmoja Mkenya mwenziwe na mwengine mwanamke kaolewa na mnaigeria. Kitu nilichojifunza kwa hao watatu wanaachlia income yao yote kwa wenza wao sijui wamejisahau vipi. Wakenya wa abroad niliowaona wengi wao wanapenda waafrika wenzao sio kama watanzania.
 
Back
Top Bottom