Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Huyo alikosea mwenyewe. Inaonekana alitaka show off kwa wakenya wenzake kwa sababu huko Marekani kila mtu yuko bize na hawajali urubani wako. Mbaya zaidi hakufanya utafiti akirudi ataanzia wapi.

Hii stori IMENIKUMBUSHA ndugu yetu mmoja mwanariadha mkubwa miaka ya 90 hadi mwanzoni mwa 2000. Huyu jamaa alikuwa anafadhiliwa na SAMSUNG na hata baadae akikaribia kustaafu riadha alipata ajira ya kudumu makao makuu ya Samsung, Korea. Akaushtusha umma kwa kuamua kuacha kazi Samsung kwa alichodai Korea kuna baridi sana pia yuko mbali na familia yake. Ikumbukwe Samsung ilikuwa inalipia tiketi ya kwenda na kurudi kwa ajili ya mke wake na watoto wao wawili mara tatu kwa mwaka.

Jamaa akarudi Arusha. Mwanzoni alikuwa kama mfalme kwasababu ya pesa. Ila kadiri muda ulivyoenda pesa pia ikawa inakata. Alivyofikia level ya kuanza kutembea kwa mguu mke naye akaanza kumsaliti kwa kutembea na rafiki wa jamaa. Jamaa alidhoofika kuanzia kiuchumi hadi kisaikolojia kwa sababu haikuwa siri tena kwamba anachapiwa. Mwaka 2009 tulimpoteza mtu wetu kwa kifo cha ghafla.

Ninadhani ukienda nchi kama Marekani yenye utulivu halafu maisha yakakunyookea endelea na maisha hukohuko. Labda kama umeenda DRC, Afrika ya kati au nchi nyingine ya kishenzi ukabahatisha pesa ni sawa kurudi nyumbani.
Daahh 😄

Inahuzunisha lakini imebidi nicheke
 
Naomba urudie kusoma uzi rafiki,huyu hakuwa msomi huyu ni rubani..."Fikiria kaweka gari bond ili alipie masomo ina maana alikuwa hajui hiyo coz inahitaji sh ngapi?...ni sawa leo wewe utake kusoma MBA uambiwe course yote ni 10M halafu wewe ukaweke bond gari uchukue 5M nini kitatokea?lazima kikurambe......Au walimroga jamani?
Hii story ina maswali mengi sana aisee, ila amepiga wrong moves nyingi. Pia kuacha mke ulaya na kuja kuoa tena huku nadhani alikosea sababu Mungu huitambua ndoa moja. Kwa wanadamu kuna kuachana ila kwake hakuna kuachana.
 
Hii story ina maswali mengi sana aisee, ila amepiga wrong moves nyingi. Pia kuacha mke ulaya na kuja kuoa tena huku nadhani alikosea sababu Mungu huitambua ndoa moja. Kwa wanadamu kuna kuachana ila kwake hakuna kuachana.
Hesabu zake zilikuwa kali sana
 
Umeongea mambo mazito sana, kiasi kwamba Umenikumbusha mambo mengi sana kuhusu maisha ,

Lakini binafsi yangu kutokana na ambayo nimewahi kuexperiance Kwa kuona kusikia na kupitia Mimi mwenyewe siwezi kuthubutu hata kidogo kumlaumu huyo Mzee

Na mara nyingi watu wengi wasicho kijua Huyo Mzee itakuwa ana sumbuliwa na issues za ancestors wao ,

Ukiwa una sumbuliwa na hayo mambo halafu ukaenda nayo against kuanguka from hero to zero ni jambo dogo sana hata uwaje , Yaani ancestors Huwa hawana masihara lazima wakufilisi na kukudhalilisha hakuna kitu utakacho weza kukifanya na ukafanikiwa, Kila unacho kifanya wanaweka barrier utajua haujui

So he's not normal,
Kabisa ndugu yangu. Maisha yana mambo mengi sana hususan kwa sisi Jamii zetu za Ki Africa
 
Kabisa ndugu yangu. Maisha yana mambo mengi sana hususan kwa sisi Jamii zetu za Ki Africa
Usicheze na jamii za Kiafrika, watu wanaogopa hata kwenda kusalimia manake wanaweza kukunasisha jumla au ukajikuta hautaki tena kusafiri na hata watoto uliowaacha huko ukawaona si lolote si chochote.
Some beliefs though but you never know.
 
Hii ni hadithi ya maumivu ya ndugu Samuel Mawato, mkazi wa Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, nchini Kenya.

Samuel hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa muokota makopo. Kwa miaka 15 aliyoshi Marekani, ambako alisomea urubani na baadaye kufanya kazi kwa muda mfupi katika shirika kubwa la ndege la American Airlines, hakuwahi kufikiria kwamba maisha yake yangeishia kuokota makopo.
Kabla ya kwenda Marekani, Samuel alikuwa akifanya kazi kama mhudumu wa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi. Hata hivyo, ndoto yake kubwa ilikuwa kuwa rubani. Kwa jitihada na maombi, hatimaye mwaka 1998 alipata fursa adimu ya ufadhili wa masomo ya urubani nchini Marekani kupitia Kanisa la Methodist.

Alijiunga na chuo mashuhuri cha ATP Flight School kampasi ya Arizona. Kwa miaka miwili alijifunza urubani na kupata leseni ya awali ya kurusha ndege binafsi (Private Pilot License – PPL). Aliendelea na mafunzo na baada ya miaka miwili zaidi akapata leseni ya kurusha ndege za kibiashara (Commercial Pilot License – CPL).

Baadaye alipata kazi kama rubani msaidizi (First Officer) katika shirika la American Airlines. Alioa mwanamke wa kizungu na kuanzisha familia. Walifanikiwa kupata watoto wawili katika ndoa yao: wa kike na wa kiume.

Mambo yalianza kubadilika baada ya Samuel kutaka kurudi Kenya na kutumia ujuzi wake kusaidia taifa lake. Walitofautiana na mkewe ambaye hakuwa tayari kuhamia Kenya. Alimtaka Samuel waendelee kuishi Marekani. Lakini Samuel aliona kubaki Marekani ni usaliti kwa jamii yake na kanisa lililomsomesha.

Mvutano huo ulisababisha ndoa yao kupasuka. Mkewe akabaki Marekani na watoto, Samuel akarudi Kenya. Baada ya miaka 15 ya kukaa ughaibuni, Samuel aliamini kurejea kwake Kenya kungekuwa mwanzo wa maisha bora na yenye matumaini. Alipoingia Kenya, akaoa mke mwingine.
Hata hivyo, mambo hayakuwa kama alivyotarajia. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA), rubani aliye somea nje ya nchi hutakiwa kufanya refresher training na kutimiza angalau 200 flight hours ili leseni yake itambulike na kuruhusiwa kurusha ndege kibiashara. Samuel alikuwa ameanza kupungukiwa na fedha, hivyo akachukua mkopo kuweka gari yake rehani ili apate fedha za kushiriki mafunzo hayo.

Fedha alizopata hazikutosha kulipia masaa yaliyohitajika. Zikaisha kabla hajamaliza mafunzo. Benki aliyokopa ikataifisha gari yake baada ya kushindwa kufanya marejesho. Hivyo akapoteza gari na mafunzo hakumaliza. Akiwa katika mtanziko, mkewe (yule aliyemuoa Kenya) akamtoroka.
Maisha yakaanza kuwa magumu. Miaka 15 aliyokuwa Marekani ilitosha kumpotezea baadhi ya marafiki na jamaa. Aliporudi, hawakuwa tena karibu naye kama zamani. Alipojaribu kuwaomba msaada, wengi walimkwepa. Hapo ndipo maisha yakazidi kuwa magumu kwake.

Hatimaye ikamlazimu kufanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani. Alianza kwa kuendesha toroli, lakini kadri umri ulivyosonga ndivyo nguvu zilivyomuishia. Hatimaye akaamua kujikita katika shughuli ya kuokota makopo. Na sasa ameanzisha kikundi kiitwacho Responsible Citizen Initiatives kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa mazingira Kilifi.

Leo akiwa na umri wa miaka 64, Samuel anajikongoja taratibu mitaa ya Mtwapa huko Kilifi akiokota makopo kama shughuli pekee inayoendesha maisha yake. Bado anakumbuka jinsi alivokuwa na imani kwamba uzoefu wake wa ng’ambo ungefungua milango baada ya kurejea nyumbani. Lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia.

Hana mawasiliano na mkewe wa Marekani wala watoto wao wawili kwa miaka mingi sasa. Anajua kwamba wanae kwa sasa ni watu wazima na huenda hata akikutana nao wasimtambue, lakini hajakata tamaa.

Katika umri wa uzee, mwili kudhoofu na maisha ya upweke, bado Samuel analo tumaini. Anaamini siku moja Mungu atampa nafasi ya kukutana na watoto wake, walau awaone tu na kuwakumbatia kabla hajafa. Hilo ndilo ombi lake kubwa kwa sasa.

Je nini maoni yako? Samuel alikosea kurudi Kenya? Samuel hakujipa muda wa kupata taarifa sahihi kabla ya kurudi? Watu wenye vipawa vikubwa na akili nyingi wameshindwa kustawi Afrika kutikana na mifumo mibovu?

Source: Facebook page ya Godlisten Malisa

Africa kinachotu cost ni UCHAWI.
 
Back
Top Bottom