Natoa uzoefu kidogo na nilichojifunza kuhusu kuishi ughaibuni, naongelea Marekani ninapopajua zaidi!
Waafrica wengi sana regardless anatoka nchi gani wanapata shida sana ya kuadapt mazingira ya nchi zilizoendelea kwa sababu moja tu kuu "emotional attachment" na nchi tulizotoka. Yani tunashindwa kukubali psychologically kwamba hatupo tena nyumbani na maisha ni popote tufanye maisha kama vile ndio ushanunua kiwanja na kujenga hapo ndio kwako, yani kama unabyohamia Mbeya, Songea, Kigoma, Kibosho mk, panakua ndio kwako hadi mambo yatakapobadilika, tunaamini ipo siku tutarudi nyumbani permanently na tunatakiwa kuwekeza huko ili tusijeaibika, tuwe na sehemu ya kuishi na pia tuwaonyeshe tuliowacha nyumbani kwamba tupo nje na tumeshafanikiwa (kuwakoga) yani wanaotujua waone kwamba tupo tofauti sasa.
Matokeo ya hii emotion tunajikuta tunapiga kazi sana na kutuma sana miamala nyumbani "tufanyiwe" kitu na tunaowaamini, unakuta mtu katuma pesa 10yrs anajenga nyumba ya kuishi na haijakamilika, huku US anateseka ile mbaya, yani hana maisha ng'ambo wala nyumbani. Ni kazi mchana na usiku iwe profession au mpiga box wote hali moja. Hii inafanya tuumize credits zetu na kujikuta tuna madeni makubwa, hatuna assets zaidi ya gari ughaibuni, credits zikiwa mbovu tunapata mikopo ya riba kubwa sana na hatuna motivation ya kulipa kwa wakati kwa kuwa tunaamini muda utafika tutaondoka (who cares). So unakuta mtu kakaa miaka 15 hana nyumba Marekani na nyumbani haijakamilika kwa kuwa anayemsaidia pia anampiga na kuinflate sana costs na hii kama huyo msaidizi ana nia njema, otherwise hata msingi hutaukuta.
Huko US ukiwa na credits nzuri una access ya resources za kutosha kila mahali na kila biashara inakuita ikuwezeshe na kwa riba ndogo sn wakati mwingine hata 0%. Ukiwa na 700+ credits kwa mfano unaweza kuchukua mkopo wa Small business authority (serikali) wa hadi $5m kwa kuwa na business plan na 10% downpayment, ukipata mzigo kama huo ni biashara gani utashindwa kufanya duniani?? Hapo hujagusa opportunities zingine maelfu za serikali ya federal, State, angel funders, ushindani, ubunifu, minority, za makanisa na dini zingine, marafiki, wawezeshaji wasiotaka kujulikana, zote hizi zinazokutafuta kila siku.
Maelezo mengi sana na nitarudi na personal experiences, sijitoi kwenye hali hiyo na nimeshtuka late sana baada ya kutoil sawasawa!