Basi katika kuwaza sana nilion njia pekee ni kwenda dar wakati bado nasubiria matokeo Basi nikatafute kibarua Cha kufanya, Basi nikaenda kwa mkuu nikaomba kwanza anipe hata namna ya kuonana na yule mzee alienitoa kwenye kibanda kushona viatu lakini na mkuu hakuweza kunipa na akasema yeye aliambiwa tu anipokee na mpaka hapa yule msaada wake ndio uliisha hapa, nililia nikamwambia naomba hata mawasiliano tu Mimi nimshukuru tu lakini hakuweza kunipa na Hadi leo sijui huyo mzee yupo wapi, basi nilimuaga mkuu akanipa na tuakiba za pesa zangu zote na zingine ambazo alitumiwa Ila hakuniambia Ila siku hiyo kanikabidhi zote nikaenda na kwa yule mama nikamwambia mama Mimi naondoka nae akanipa kafungu fulani kazuri na kaniandikia barua kanipeleka kwa RTO nikatandikiwa barua ya kupewa msaada wa kusafiria bure hii Hadi leo barua hii ninayo Kama kumbukumbu yangu.
Nilienda kituo Cha tren nikapanda baada ya kuonyesha kibarua changu huyoo mpaka dar nikafika sehemu nilipokuwa nashona viatu nikamkuta jamaa yangu yupo nikafurahi sana kumwona tukasalimiana baadae nikaenda kulala gongo la mboto guest kesho yake mapema nikashuka Pugu mnadani kwa mbele panaitwa mwambisi hapa ni kile kipindi bado watu hawajahamishwa huko kulikuwa na mzee mmoja wa kinyaturu huko Mwambisi tulifahamiana wakati nashona viatu akanipa maelekezo akaniambia ukiona maisha yanakuwa magumu naomba uje tubanane hapahapa.
Nilifika yule mzee akanipokea vizuri kabisa kwa furaha nikajitambulisha akawa amenifahamu vizuri na maisha yakaanza ya kukata mkaa na kwenda kuuza Pugu kajiungeni huko na Goms mwisho wa lami.
Katika kukata mkaa kwangu nilikutana na watu wengi sana na tukafahamiana nikawa mwenyeji mno na nikapata fedha nyingi tu, matokeo ya form 4 yalitoka siku yanatangazwa nipo zangu Buguruni narudi zangu Goms nasikia kwenye Gari matokeo matokeo mie nikawa nahamu ya kutaka kujua Nini kinaendelea nikapita kwa binamu yangu kwa Mara ya kwanza tangu niondoke hapo kwa kutoroka Basi nikamkuta binamu yupo karudi job nikamwambia binamu unajua nilikuwa shuleni, Wala hakuchukulia uzito sana duuh mood yote ikaisha kabisa nikaondoka kwenda kwa mzee mmoja alikuwa jirani yake na ni mtu wa home nikamwambia yote lakini ombi langu naomba unifanyie mpango nijue matokeo yangu ya kidato Cha nne mzee akasema usijali mwanangu kesho nikienda job nitakuambia.
Siku ikafika kesho yaani Nina Moto vibaya mzee kaja kwanza kacheka kaniambia we kweli mwanaume, nikamwambia Basi niambie tu, mzee kauvuta mkeka akaniambia Tabora boys mna one ya 7 zipo kadhaa na wewe umo nikamwambia unanitania akasema ni kweli Basi nikafurahi Hadi machozi siku hiyo ilikuwa ni ijumaa nikasepa Hadi church kukesha kabisa kwa maombi.
Itaendeleaa.........