Kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa matumaini ya kupata msaada wa elimu

Inaendelea....

Baada siku nilipokuwa likizo na kuwepo Mwanza ziliisha na nikaondoka kurudi kazini mgodini nikaa mgodini kwa miezi miwili na baadae nikapata ujumbe wa kuitwa dar japo sikuambiwa kuwa ni Nani haswa ananihitaji, niliomba ruhusa kazini kuwa naenda Singida Kuna shida kidogo home niliondoka kwenda Mwanza nikapanda ndege Hadi dar nilifikia Hoteli fulani nikachukua room nikalala.

Usiku huohuo saa 6 nikapigiwa simu namba ile ile ilioniomba kuja dar na kadri ya maelezo ya ujumbe nikaombwa kufika Kunduchi bila kukosa mda huo usiku, Basi niliamka nikatoka na beg langu nikaaga hotelini kuwa kesho Nina safari hivyo ninaetakiwa kusafiria nae ameniomba kwenda nikatafuta usafiri wa tax Hadi Kunduchi, nimefika nikapokelewa sehemu nikaulizwa baadhi ya maswali na swali la mwisho ilikuwa ni Kuna mtu yeyote unaweza kumuaga mda huu nikasema ndio.

Hivyo nilipata wasaa Kama masaa 3 ya kubaki na simu yangu kuaga kazini kwangu na mtu wangu wa karibu na Mambo mengine baadae nikamkabidhi simu yangu mhusika nikapotea.
"Mungu ni wa upendo"

Itaendeleaa.....
 
Inaendelea baada ya mda sana nikawa na kazi yangu mpya nikamshukuru Mungu na maisha yanaendelea na kuzurura mikoa na wilaya mbalimbali nchini baadae nikapata nafasi ya kwenda kusoma nje masters na kurudi kuendelea kutumikia nchi yangu hata Sasa naendelea.

Changamoto:

Ndugu zangu katika maisha Kuna Mambo mengi sana Kuna changamoto nyingi sana nakumbana nazo kwenye maisha hasa zingine zinatokea kwa watu ambao usingeweza kufikiria ama kuwaza kuwa huyu niliemsaidia hiki au kile anaweza kunipitisha au kunisema kwa ubaya kiasi hiki! Ila yote kwa yote huwa namuachia Mungu na kuendelea kujifunza zaidi,
Kuna mahazi nahangaika kumpa mtu ufadhili wa masomo lakini natumia mda wangu na hela zangu kusema kuwa nirudishe fadhila zangu kwa Mungu lakini mtu anaenda kuishia kula Bata tu chuoni kusoma hasomi anatoka na matokeo ovyo na wengine kufel kabisa.

Nimesadia mabinti watano Kati ya hao wawili walipigwa mimba wakaacha shule mmoja yeye aliamua kunisikiliza yeye nimemtafutia na scholarship nje ya nchi yeye ananitia moyo kila hatua wengine wawili wapo nchini nao kidogo wanapambana.

Cha ajabu Sasa watoto wa ndugu zangu ambao nilisema nitamweleza nguvu kubwa kwao wao hata shule ya msingi hawamalizi Sasa najikuta namlilia Mungu afanye Jambo kwao Ila imekuwa ngumu sana.

Itaendeleaa.....
 
Inaendelea....

Changamoto katika mahusiano:

Hapa wakuu naombeni ushauri wapi nakosea, Ila pia naomba ushauri wako usijikite kuzungumzia ngono na Wala sipo hapa kujadili maswala ya ngono nipo hapa kujifunza Nini nifanye kwenye relationship.

Kama miaka 5 Nyuma nilipata mdada ambae ni mwalimu wa sec tulikubaliana kufunga ndoa nae na nilifanya kila kitu ambacho wato hujitoa kwenye mahusiano kasoro sex tu, tukapanga mipango mingi sana nikatamani akaongeze shule pia lakini nikamwomba tufunge ndoa kwanza na baadae aende chuo Kama mke wa mtu na nitampangishia Nyumba nzima iwe rahisi hata nikitaka kwenda kumsalimia Basi nijiachie.

Huyu mwanamke nilimpenda sana nae Kama alikuwa ananipenda sana japo siwezi kujua ndani ya moyo wake sana, Hadi mahali nilitoa na nikamvalisha na Pete ya uchumba kabisa Tena kanisani.

Huyu mwanamke kabla ya tarehe ya ndoa akawa ameonekana na mimba Tena bila hata kuficha alipoitwa na mchungaji akasema ni ya kijana wa kanisani hapo ambae pia ni mwl mwenzake hivyo anaomba asamehewe amekosea nimuoe tu huyo mtoto atampa jamaa akikuwa 😳😳😳😳🏃🏃 hapa ikawa ngumu kuelewa hata kidogo, niliamua kwenda kurudisha magari yangu na kuchukua Pete yangu nikaenda kuiuza .

Itaendeleaa......
 
Endelea mkuu.

Hata hivyo nimejufunza mengi kwenye simulizi yako.
 
Daah pole sana mkuu.
Kwa Changamoto unayopitia.
Jipe moyo, utayashinda
 
Hapo kwenye mahusiano 🚶🤦

Pole Kaka...Ila maisha yako ni muujiza unaotembea.
Kama Mungu alivyokupigania juko nyuma usichoke kumlilia akuonekanie kwenye mahusiano yako.

Most of the time, mambo ya mahusiano hua yanatutoaga kwenye reli na kusahau vile Mungu alivyotutendea mwishoni utajikuta unahangaika peke yako.
 
Na kingine Tabora schools walimu wengi ni waaminifu... cheers to Tabora schools by m-warsaw mmoja🥰
 
Hapo kwenye mahusiano 🚶🤦

Pole Kaka...Ila maisha yako ni muujiza unaotembea.
Kama Mungu alivyokupigania juko nyuma usichoke kumlilia akuonekanie kwenye mahusiano yako.

Most of the time, mambo ya mahusiano hua yanatutoaga kwenye reli na kusahau vile Mungu alivyotutendea mwishoni utajikuta unahangaika peke yako.
Ameen! Katika maisha yangu nilishamua moja Hata Kama nipitie Moto kwa namna gani sipo tayari kugeuka nyuma maana nimetoka mbali Sana na ninakoelekea ni karibu mno.
 
Thats the faith Baba...Mungu akutangulie
Ameen! Katika maisha yangu nilishamua moja Hata Kama nipitie Moto kwa namna gani sipo tayari kugeuka nyuma maana nimetoka mbali Sana na ninakoelekea ni karibu mno.
 
Inaendelea....

Changamoto katika mahusiano:

Hapa wakuu naombeni ushauri wapi nakosea, Ila pia naomba ushauri wako usijikite kuzungumzia ngono na Wala sipo hapa kujadili maswala ya ngono nipo hapa kujifunza Nini nifanye kwenye relationship.

Kama miaka 5 Nyuma nilipata mdada ambae ni mwalimu wa sec tulikubaliana kufunga ndoa nae na nilifanya kila kitu ambacho wato hujitoa kwenye mahusiano kasoro sex tu, tukapanga mipango mingi sana nikatamani akaongeze shule pia lakini nikamwomba tufunge ndoa kwanza na baadae aende chuo Kama mke wa mtu na nitampangishia Nyumba nzima iwe rahisi hata nikitaka kwenda kumsalimia Basi nijiachie.

Huyu mwanamke nilimpenda sana nae Kama alikuwa ananipenda sana japo siwezi kujua ndani ya moyo wake sana, Hadi mahali nilitoa na nikamvalisha na Pete ya uchumba kabisa Tena kanisani.

Huyu mwanamke kabla ya tarehe ya ndoa akawa ameonekana na mimba Tena bila hata kuficha alipoitwa na mchungaji akasema ni ya kijana wa kanisani hapo ambae pia ni mwl mwenzake hivyo anaomba asamehewe amekosea nimuoe tu huyo mtoto atampa jamaa akikuwa 😳😳😳😳🏃🏃 hapa ikawa ngumu kuelewa hata kidogo, niliamua kwenda kurudisha magari yangu na kuchukua Pete yangu nikaenda kuiuza .

Itaendeleaa......
Pole mkuu. Hizi changamoto tunazipitia wanaume wengi sana japo haziwezi kufanana 100%. Maliza kwanza stori kisha nitatoa ushauri wangu kulingana na experience niliyo nayo na hawa viumbe.
 
Inaendelea.....

Baada ya kurudisha mahari yangu na kuchukua Pete yangu, nilikaa Kama miezi 6 hivi nikapata mdada mmoja huko Arusha mmeru Fulani hivi akiwa ndio kamaliza chuo tukaongea akaniomba kwanza nimtafutie japo kazi ili hata maandalizi ya harusi na nini isiwe tabu kunisumbua Mimi kugharamia shughuli zote, Basi kwangu nikaona ni bonge la wazo na kwa sababu ya connection mjini Kama mnavyojua Tena ni kitendo Cha kuagiza tu huyu kesho aje kazini na kupata kazi fasta tu week mtu huyo job.

Kufika job week mbili baadae simu hazipokelewi Mara visingizio vingi sana,kosa kubwa hakujua kuwa kwenye hiyo ofsi hiyo manager ni rafiki yangu tumekulia wote pori tumechunga sana na kuogelea kwenye maji machafu, nikampigia mshikaji simu kwani Kuna Nini huko akaniambia usijali nimpe kazi ya kufuatilia ilichukua siku tatu akanasa kila kitu Hadi kutumiwa video yupo bar anakunywa aisee nusu nizimie yaani, nikapanda Gari Hadi huko nikafika hotelini nikamwita kaja nikamhoji akagoma Tena na kilio na kusema anasingiziwa tu daah nikamwonyesha kila kitu kabaki mdomo wazi ni vilio Tena kuomba msamaha.

Daahh endelea Mkuu nimesoma mwanzo mwisho aiseee huu n muujiza mkuu na nimejifunza vtu vingi sana kwanza uvumilivu, Heshima kumuheshimu kila mtuu na kikubwa zaid n kumtanguliza M/Mungu kwa kila kitu unachokifanya endelea mkuuu tafazal
 
Back
Top Bottom