Hii issue imeonyesha Tanzania hatuna media kabisa. Nchi nyingine kwa kutumia viashiria mbali mbali wangeweza kujua kinachoendelea. Unaweza kuweka waandishi fukunyuzi (wakajjicha kijasusi) area muhimu kama maeneo ya Ikulu. Hospitali ya Kitengo na sehemu nyingine na ukaja na jibu. BTW kila mtu ana theory yake. Kuna anayesema ameambiwa na waziri kuwa jamaa amefunga kwaresma na amejifungia, kuna anayesema anachapa kazi, kuna anayesema kafa, kuna anayesema ni mgonjwa. Kila mtu na lake. Jambo lililo dhahiri ni kuwa hata mawaziri wengi hawajui kinachoendelea. Inaonekana inner circle ya Magufuli ndiyo inajua na ni wachache sana na wengi ni watu wa usalama kutoka ukanda wake.