Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,508
Mapungufu ni mengi, kwanza kaonekana hakujipanga in the first place, kama hakujipanga kwa speech muhimu kama hii unategemea ajipange akiwa ikulu?Ebu twendeni taratibu na swala hli, Tutazame upande wa pili wa shilingi. Kwa nini watu mnafikiri Membe hafai? Ana mapungufu gani kama kiongozi na kwa nini watu mnafikiri Mwigulu amefanya vizuri kuliko Membe katika kuweka nia!. NIA ni kitu gani?
Hivi kati ya wagombea wote wa CCM kuna mmoja ambaye nyie mnafikiri ni bora zaidi ya wengine? na kwa nini?
Kama umesikiliza Membe hajataja vipaumbele vyake tofauti na watiania wengine kama Wassira, Mwigulu nk waliokuwa wanataja kama ni vitano au vinne, mfano hakuzungumzia chochote kuhusu elimu, afya, maji nk.
Technical errors, sehemu kama hiyo hakutakiwa kuuabudu ushirikina waziwazi hadi kaita mzee wa kufanya zindiko kwenye mkutano, vile vile tumemsikia akisema alikwenda kwenye kaburi la Nyerere na kuongea naye, really?
Pili hatunzi kumbukumbu vizuri, kasema atagombea uchaguzi wa 2010, pia kasema tangu uhuru wapinzani wamekuwa wakishindwa uchaguzi wengine wameshindwa mara tano, hii ni kuonesha hakuwa anajua alichokusudia kukisema.
Tatu, personal attacks, kwa mtu mwenye diplomasia kama yeye hakutakiwa aende too personal.
Nne, pale alikuwa anatangaza nia alitakiwa kuwaomba wana CCM wampe ridhaa na sio kupambana na UKAWA kwa vile Ukawa sio wajumbe wa NEC ya CCM, alitakiwa kuelewa kwa kipindi hiki maadui (competitors) wake sio UKAWA ni watiania wa CCM ambao leo wanafika 22.
Amejikita kwenye eneo moja la ushirikiano wa Tanzania na nchi za nje huku masuala yanayowagusa wananchi wa kawaida akiyapa nafasi ndogo au kuyaacha kabisa.