Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Membe anatangaza nia sasa UKAWA wanapigwa vipi hapo? wakati mwingine jitendeeni haki akili zenu kuliko kujishabiisha na vinyesi namna hii.....

Yaani wewe unatia kinyaa Sana bora uendelee kushinda kule kwenye jukwaa la mashosti wenzio...

Hahaaaaa
Yaani umenichekesha
 
Binafsi nimevutiwa sana na hotuba ya Membe. Hakika CCM ina hazina ya viongozi.
 
Tangu waanze kutangaza nia membe Leo ameharibu.
1.hajaeleza dira dhidi ni historia yake.
2.kutukana wapinzani wakati hajapitishwa bado na cc .
3.Ameshindwa kuwa na Hoja sahihi zaidi ya kueleza tambo za rushwa bila kuzifahamu sheria za rushwa .
4.Kuivua nguo serikali wakati yeye ni mmoja wapo.
5.Kueleza habari za kaburi la nyerere wakati makongoro analala juu ya kaburi la baba yake.
5.Amefeli kuelezea kwanini awe yeye na si mwingine.
6.Pia amejishushia hadhi pale aliposema kawa kiongozi wa CCM tangu enzi za nyerere,Mwinyi,Mkapa ila hakuwahi kuwa hata balozi wa CCM wa nyumba kumi means viongozi wa awamu tatu hawakumuamini .Busara angekaa kimya angetangazia nia chumbani akiwa yeye na mke wake.
Kweli amekosa washauri wa kumweleza cha kusema ? na waandishi wa hotuba mlishindwa kumwandikia ya msingi zaidi ya Ngoma za kimwela?,
Ndio maana Nasema Leo mh membe umetia aibu kweli hotuba ya kuwania urais uzungumzie "Ukiwa rais utakataza pombe kwa wanaume wanaowanywea watu" Kweli membe uko serious hata Huyo shemeji hawezi kukubeba kwa style hii .Hotuba yako haukuipanga ktk mtindo wa nini cha kufanya kwa Tanzania ijayo ndo maana ulikuwa ukisema nani kama membe watu kimya.
Tunakushauri kaa pembeni maana huwezi kujenga Hoja zenye mantiki na mashiko.
Ahsante
Twalb zubeir
FBI .
 
Hotuba ya vijembe bila kutueleza atalifanyia nini taifa Kweli membe haingii hata robo kwa mwigulu.
 
Kutoka CCM kati ya wote walokwisha tia NIA mimi namkubali Membe kutokana na jinsi navyomfahamu akiwa ubalozini Canada, yeye na marehemu Aziz hakika walikuwa mfano bora wa Ubalozi unatakiwa kushirikiana na wananchi kiasi gani. Tukimuita Kichwa toka enzi hizo.. Lakini binadamu hubadilika sijui baada ya kuwa waziri ameonyesha mapungufu gani ya dhahiri kiasi kwamba kila mtu anapingana na uwezo wake.
 
Membe ni mtu hatari sana! Amepania kuyashughulikia baadi ya makundi na kuwabeza ukawa,huyu akipata madaraka ataleta mpasuko zaidi na vurugu zisizoisha,eee mungu epushia mbali.....
 
Leo ndio nimezidi kuamini Membe hafai kabisa.... Jamaa ni mweupe ile mbaya
 
Hahahaa...eti nimeongea na Mwl Nyerere kabulini kwake akanambia nafaa, jamaa hovyo kabisa.
 
baada ya ccm kukataza watangaza nia kushiriki mdahalo ndo nikaelewa kuwa Membe ndo chaguo la ccm.wanajua udhaifu wake ndo maana walijua ataaibika
 
PPM

Mkuu sema hutaki wewe, maana sisi wengine kama Watanzania na sio UKAWA lazima tujiandae na mtu yeyote atakaye chaguliwa kwa kura nyingi. Sifa na Mapungufu ya kila mgombea ni lazima tuyazungumzie maana hayakwepeki. Mtu akisha weka nia fahamu ya kwamba kuna uwezekano akawa ndiye rais wako.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: PPM
Mimi ninachofurahi, ni jinsi CCM wenyewe kwa wenyewe mnavyoambiana ukweli.

Hakuna wa kutuzuia Magogoni. Ukawa mbele
 
Back
Top Bottom