Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,413
- 4,020
inaonesha humu kuna kundi kubwa la wale waliokodiwa mabasi kwenda sheikh amri abeid.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu taratibu, twende kwa mpango maana siwezi kuamini kwamba Mbatia anaweza washinda Lipumba na Dr.Slaa kwa kutia nia halafu ukasema afadhali watakuwa wamezungumza facts!..FACTS zipi hadi washindwe na huyo Mbatia atakuwa amesema nini. Ukishindwa ina maana hukuweza kuwaridhisha wananchi kwisha..Yawezekana Dr Slaa na Prof Lipumba wasimzidi Mbatia kwa kupangilia mawazo yao vizuri wanapowasilisha hoja lakini bado hoja zao zitakuwa nzito,zenye facts na zinazoshawishi.At least hawatachanganya mambo kama Mr Bernard C. Membe kwamba wanatangaza kugombea urais mwaka 2010 au vyama vyama vimezowea kushindana na kushindwa tangu tupate uhuru mpaka sasa. Aidha ameapa kupambana na ugaidi nchini,is he serious? Hivi terrorists anawajua?Wapi wamelipua Tanzania? Huyu kama akiwa rais anaweza kuvunja rekodi za Mulugo (Waziri wa Elimu wa zamani) aliyedai kwamba Muungano wa Tanzania unatokana na Tanganyika na Zimbabwe. Hatutake tuaibike huko nje ya nchi kwamba rais wetu amechanganya mambo ktk hotuba yake flani,please!
Mkuu, kwa taarifa tu Tanzania huwa tunachagua mtu(rais) atakayewakilisha chama huwa hatuchagui chama kama UK. Sasa kama mtiania huyo hana anachopanga kuanza nacho kama alivyo Membe kuna haja gani ya kumfikiria kuwa rais.Mkuu labda nikuulize hivi. Kweli wewe unategemea Lipumba na Dr.Slaa wasimame kuweka nia kama wagombea wa UKAWA, kisha kila mmoja ajieleze tofauti na ILANI ya UKAWA watakuwa wamejenga hoja ya msingi? Yaani Mbatia akiongea vizuri kuliko Dr.Slaa au Lipumba itakupa moyo zaidi na Mbatia ama jinsi unavyowafahamu wagombea hawa nani mwenye uwezo zaidi?
Nimepitia maandishi ya mleta mada hapo juu sikuona kosa zaidi ya mtu aloweka nia tu. Kumbuka kila alozungumza kasema Vipaumbele vyake ataanza na nini wakati hakuna kati yao alosema fedha zitatoka wapi? Atakata wapi ili awezeshe wapi. Hizi zote ni porojo tupu kwa mtu asokuwa na kitu maana waswahili wengine wamejaaliwa mdomo lakini utekelezaji ni mashoga.
Mipango yote ya Maendeleo ya CCM yanategemea mikopo na mpango wa maendeleo tulopewa na IMF na Marekani Millenium sijui hadi huko 2025, kwa hiyo hakuna mjuzi pale, wote wameisha pangiwa (copy and paste) umchague Membe au Mwigulu tofauti zao ni nani kweli ataweza kusimamisha utawala wa sheria katika nchi hii ama kuleta kweli mageuzi..
Hivi kwani ni amir jeshi?au ndo anaomba agombee!Ameongea kama Amir jeshi mkuu
Unachokosea mkuu wangu ni kusema tanzania tunachagua MTU ukasahau kwamba huyo mtu hupangiwa ILANI na chama chake. Hivyo vipaumbele vyake ni porojo tupu maana masikini hana kupanga jambo hupangiwa.Mkuu, kwa taarifa tu Tanzania huwa tunachagua mtu(rais) atakayewakilisha chama huwa hatuchagui chama kama UK. Sasa kama mtiania huyo hana anachopanga kuanza nacho kama alivyo Membe kuna haja gani ya kumfikiria kuwa rais.
Kama wagombea hawana sera na vipaumbele vyao kuna haja gani ya kuwa na watiania wengi ndani ya CCM si wangemteua mwenyekiti wao tu akawakilisha chama kupambana na mgombea kutoka UKAWA.
Tofauti na CCM UKAWA nao wana utaratibu wao wa kumpata mgombea, hata kama watakuwa na sera na ilani moja itawalazimu kuwaita wagombea watakaojitokeza wajieleze vipaumbele vyao.
Mfano...ilani ya UKAWA kwenye sera iko kama ifuatavyo, 1. Elimu 2. Afya 3. Miundombinu nk, itabidi waangalie mgombea A ana vipaumbele vipi kwenye sera ya Elimu je ataanza na kujenga madarasa au yeye ataanza na mishahara ya walimu nk, je B yeye anasemaje kwenye sera ya Miundombinu anaona kipi muhimu kujenga reli au barabara na ana mipango gani. Kwa hiyo hata kama chama kina sera na ilani yake lazima kiangalie kitafit most na mgombea yupi.
Hapo kwenye RED ndicho pia wanachofanya CCM! Utafika wakati wote hawa wataitwa mbele ya vikao vya CCM kuelezea vipaumbele vyao... kimsingi, wakati wa kutangaza nia hawalazimiki kufanya hivyo! Pale inatosha kabisa kuitisha tu Press Conference ukatangaza nia, biashara inaisha na kusubiria hatua nyingine!Tofauti na CCM UKAWA nao wana utaratibu wao wa kumpata mgombea, hata kama watakuwa na sera na ilani moja itawalazimu kuwaita wagombea watakaojitokeza waeleze vipaumbele vyao.
UKAWA tunaheshimu hadhi ya cheo cha rais sio CCM ambao wamekifanya kama sehemu ya kujifunzia siasa hadi watoto wa shule wa miaka 20 nao wametangaza.
tangu waanze kutangaza nia membe leo ameharibu.
1.hajaeleza dira dhidi ni historia yake.
2.kutukana wapinzani wakati hajapitishwa bado na cc .
3.ameshindwa kuwa na hoja sahihi zaidi ya kueleza tambo za rushwa bila kuzifahamu sheria za rushwa .
4.kuivua nguo serikali wakati yeye ni mmoja wapo.
5.kueleza habari za kaburi la nyerere wakati makongoro analala juu ya kaburi la baba yake.
5.amefeli kuelezea kwanini awe yeye na si mwingine.
6.pia amejishushia hadhi pale aliposema kawa kiongozi wa ccm tangu enzi za nyerere,mwinyi,mkapa ila hakuwahi kuwa hata balozi wa ccm wa nyumba kumi means viongozi wa awamu tatu hawakumuamini .busara angekaa kimya angetangazia nia chumbani akiwa yeye na mke wake.
Kweli amekosa washauri wa kumweleza cha kusema ? Na waandishi wa hotuba mlishindwa kumwandikia ya msingi zaidi ya ngoma za kimwela?,
ndio maana nasema leo mh membe umetia aibu kweli hotuba ya kuwania urais uzungumzie "ukiwa rais utakataza pombe kwa wanaume wanaowanywea watu" kweli membe uko serious hata huyo shemeji hawezi kukubeba kwa style hii .hotuba yako haukuipanga ktk mtindo wa nini cha kufanya kwa tanzania ijayo ndo maana ulikuwa ukisema nani kama membe watu kimya.
Tunakushauri kaa pembeni maana huwezi kujenga hoja zenye mantiki na mashiko.
Ahsante
twalb zubeir
fbi .
baada ya ccm kukataza watangaza nia kushiriki mdahalo ndo nikaelewa kuwa membe ndo chaguo la ccm.wanajua udhaifu wake ndo maana walijua ataaibika
Atakuzaje? Nini maana ya huduma bora ama utawala bora ikiwa hazisemi sheria gani atazipitisha. Ndio hayo ya Cyberbill badala ya kutaja specific crimes, sheria inasema matumizi mabatya ya Mitandao.. Ni yapi hayo? oooh hapo tena utawasikia sijui Bulling! kwani walishindwa nini kuandika Bulling katika mitandao ndio crime! badala yake tunaona sheria inayotaka kumlinda Lowassa na mafisadi isiwe kigezo cha kuwabomoa.Mkandara
Sikiliza vipaumbele vya January Makamba sikumsikia Membe akitaja hata kimoja.
1. kukuza kipato cha uchumi cha mtu mmoja mmoja.
2. huduma bora za uhakika za kijamii
3. utawala bora, utawala wa haki
4. usimamizi wa uchumi ma benki, TRA, na mashirika ya umma nk.
5. kudumisha amani
kubwa zaidi watu tunadhani pale ni sehemu ya kumwaga sera wakati kimsingi pale ni sehemu ya kutangaza nia tu... Haya maneno mengi ni mbwembwe tu kwa kuwa e.l alianza kwa staili hiyo! Pale membe na wengine kama yeye hawatafuti ridhaa ya watanzania bali ridhaa kutoka kwa wana-ccm, hivyo basi, kwa hatua hii, wanakotakiwa kujimaliza ni ndani ya vikao vya ccm na sio kwenye mikutano ya kutangaza nia! Na hata hii mkikutano ya kuoneshwa live wala haikuwa na sababu lakini kv kuna mtu ameanza, hakuna aliye tayari kuachwa nyuma! Candidate awe na sera bora kuliko zote lakini, mathalani, ikiwa moja wapo ni kuvunja muungano, ccm hawawezi kukupitisha lakini kama ingekuwa ni wakati wa kutangaza sera kwa wananchi huenda sera hiyo ingekupa kura!! Wakishatoka kwenye vikao vya ccm, nikiwa na maana kwa yule atakayepitishwa kama ndie mgombea rasmi, ndipo sera zao sasa zitakuwa wazi kwa watanzania! Na kimsingi, zinakuwa sio sera zake tena bali ni sera za ccm!!
baada ya ccm kukataza watangaza nia kushiriki mdahalo ndo nikaelewa kuwa membe ndo chaguo la ccm.wanajua udhaifu wake ndo maana walijua ataaibika