Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

inaonesha humu kuna kundi kubwa la wale waliokodiwa mabasi kwenda sheikh amri abeid.
 
Mkuu taratibu, twende kwa mpango maana siwezi kuamini kwamba Mbatia anaweza washinda Lipumba na Dr.Slaa kwa kutia nia halafu ukasema afadhali watakuwa wamezungumza facts!..FACTS zipi hadi washindwe na huyo Mbatia atakuwa amesema nini. Ukishindwa ina maana hukuweza kuwaridhisha wananchi kwisha..

Kifupi, Hali ya Usalama nchini ni tete na usitazame tu magaidi (terrorists) Kina Al - Shabab, wapo magaidi wa ndani kama umesahau wakimbizi wa Rwanda na Burundi awamu ya kwanza ya JK. Majambazi wa kupora na kuiba majumbani all are terrorist. Kuna maswala ya Zanzibar na Bara, Waislaam na Wakristu akipitishwa rais mzigo, mkuu wangu itakula kwetu.

Mimi simpambi lakini ndivyo navyoona hadi sasa hivi watu watatu, Yeye, Mwigulu na Makongoro wana ukomavu katika baadhi ya sehemu. Makongoro ni CCM Asilia, sijui kama ataweza badilisha watu walokwisha batizwa Ubepari, Mwigulu kaandaliwa vema na Membe anayo experience zaidi yao wote sehemu nyeti ktk kutazama uwezo na sifa za mgombea Urais.

Binafsi yangu leo, bora mtu anayezungumzia mambo ya ndani na sheria kuliko yule anaye ahidi Maendeleo wakati kisha pangiwa anafanya nukuu tu. Nani baina yao aloahidi nje ya Mipango ya maendeleo tulokwisha pangiwa hadi 2025 nakala hii HAPA Je, huyo muweka nia wa CCM ataandika yake kinyume cha kupangiwa?.Atapata wapi fedha za kuanzisha miradi hiyo kama sio kodi juu zaidi kwa wananchi..
 
Mkuu, kwa taarifa tu Tanzania huwa tunachagua mtu(rais) atakayewakilisha chama huwa hatuchagui chama kama UK. Sasa kama mtiania huyo hana anachopanga kuanza nacho kama alivyo Membe kuna haja gani ya kumfikiria kuwa rais.

Kama wagombea hawana sera na vipaumbele vyao kuna haja gani ya kuwa na watiania wengi ndani ya CCM si wangemteua mwenyekiti wao tu akawakilisha chama kupambana na mgombea kutoka UKAWA.

Tofauti na CCM UKAWA nao wana utaratibu wao wa kumpata mgombea, hata kama watakuwa na sera na ilani moja itawalazimu kuwaita wagombea watakaojitokeza waeleze vipaumbele vyao.

Mfano...ilani ya UKAWA kwenye sera iko kama ifuatavyo, 1. Elimu 2. Afya 3. Miundombinu nk, itabidi waangalie mgombea A ana vipaumbele vipi kwenye sera ya Elimu je ataanza na kujenga madarasa au yeye ataanza na mishahara ya walimu nk, je B yeye anasemaje kwenye sera ya Miundombinu anaona kipi muhimu kujenga reli au barabara na ana mipango gani. Kwa hiyo hata kama chama kina sera na ilani yake lazima kiangalie kitafit most na mgombea yupi.
 
Unachokosea mkuu wangu ni kusema tanzania tunachagua MTU ukasahau kwamba huyo mtu hupangiwa ILANI na chama chake. Hivyo vipaumbele vyake ni porojo tupu maana masikini hana kupanga jambo hupangiwa.

Kwa hiyo unachanganya kutazama mazuri yanayokufaa tu wakati hutazami hali halisi ya vyama na sababu za kufukuzwa watu wasiofuata misimamo ya chama. Kweli sisi huchagua MTU na sio chama kwa hiyo Membe hatafuti kura yako bali ameweka nia ili kupata hizo saini za wafadhili wake. Tofauti na mfumo wa nchi nyingine wagombea wote tayari wana uhakika wa wadhamini toka mikoa yao ama sehemu walokwisha pitia, kwa hiyo hatua ya pili ni kupita ngazi za chama tu na kuna vigezo vyake sio swala la Sera wala vipaumbele ila nani anauzika?.

Hivyo mgombea huchaguliwa kwa sababu anakubalika na wananchi kwa sura na tabia zake maana kumbuka JK alikataa hata midahalo na Dr.Slaa na bado akashinda!. Kwa hiyo yeyote atakaye simama kwa jina la CCM ndiye atakaye tangaza SERA na ILANI ya chama dhidi ya Upinzani kwa kutoa ahadi tu, lakini leo huko ndani watashindania nani atakuwa mwakilishi mzuri wa CCM kwa kufuata vigezo vya Wadanganyika kama mnavyotaka hadi sasa ambavyo ni UNAFIKI, Atakaye kuwa MNAFIKI zaidi ndiye atakaye shinda, watu kama Muhongo na Lowassa!.
 
Mkandara

Sikiliza vipaumbele vya January Makamba sikumsikia Membe akitaja hata kimoja.

1. kukuza kipato cha uchumi cha mtu mmoja mmoja.
2. huduma bora za uhakika za kijamii
3. utawala bora, utawala wa haki
4. usimamizi wa uchumi ma benki, TRA, na mashirika ya umma nk.
5. kudumisha amani
 
Ccm hakuna jipya watu ni wale wale sera zilezile tusitarajie manadiliko yoyote kutoka kwa hawa jamaa, tubadilishe tuweke chama kingine kwani sio dhambi.. Tanzania miaka 50 hakuna mabadilko ya maana rasilimali zinaisha nchi inageuka jangwa na bado nchi masikin...
 
Tofauti na CCM UKAWA nao wana utaratibu wao wa kumpata mgombea, hata kama watakuwa na sera na ilani moja itawalazimu kuwaita wagombea watakaojitokeza waeleze vipaumbele vyao.
Hapo kwenye RED ndicho pia wanachofanya CCM! Utafika wakati wote hawa wataitwa mbele ya vikao vya CCM kuelezea vipaumbele vyao... kimsingi, wakati wa kutangaza nia hawalazimiki kufanya hivyo! Pale inatosha kabisa kuitisha tu Press Conference ukatangaza nia, biashara inaisha na kusubiria hatua nyingine!
 
UKAWA tunaheshimu hadhi ya cheo cha rais sio CCM ambao wamekifanya kama sehemu ya kujifunzia siasa hadi watoto wa shule wa miaka 20 nao wametangaza.


Wanaeshimu urais wapi! democrasia changa na mfumo wa kidictatar na kifalme unaowanyanyasa nafsi, kibabu kimengangani tangaza nia uone.
 


ccm futa membe futa lowasa,hawafai wapenda bifu za kijinga,wapenda mitandao na urafiki usio na tija kwa masikini, hawajiamini ndo maana wanaweka watu wa kuwapamba hadi kwenye mitandao.
 
baada ya ccm kukataza watangaza nia kushiriki mdahalo ndo nikaelewa kuwa membe ndo chaguo la ccm.wanajua udhaifu wake ndo maana walijua ataaibika

mkuu mdahalo upo kwa watangazani nawaurumia wengine maana vigezo vilivyo wekwa ni aibu.mfn

1,hotuba inayoeleweka
2,nusu ya takwimu za hotuba yako zitoke kichani sio kukopy hadi kumta,
3 muda masaa 3
4,mtiririko uaoeleweka sio kurudi hoja na maneno,
yaani acha kabisa iko burudani

 
Atakuzaje? Nini maana ya huduma bora ama utawala bora ikiwa hazisemi sheria gani atazipitisha. Ndio hayo ya Cyberbill badala ya kutaja specific crimes, sheria inasema matumizi mabatya ya Mitandao.. Ni yapi hayo? oooh hapo tena utawasikia sijui Bulling! kwani walishindwa nini kuandika Bulling katika mitandao ndio crime! badala yake tunaona sheria inayotaka kumlinda Lowassa na mafisadi isiwe kigezo cha kuwabomoa.

Labda nikwambie ukweli, January Makamba nilimpenda kwa sababu ya exposure yake lakini ilipofika swala la kodi za simu, mara kaingia katika hii Cyberbill ili kumlinda Lowassa kiana huku tukiaminishwa ni team tofauti inanipa picha kwamba pengine he bet his chances as plan B itakavyokuwa japo EL anataka yeye tu na kama sio yeye basi hakuna mwingine..

Kwa hiyo, hii habari ya kutangaza sijui nitafanya hivi ama vile wakati unaomba nia ni kujaribu kuleta siasa za nchi za magharibi ambako rais ana wajibu mkubwa wa kujitofautisha katika Vipaumbele vyake akionyesha fedha zitatoka wapi na atakata mambo gani kutokana na bajeti inayotegemewa na wataalam wa mambo hayo wakayajadili.
 


mkuu nimekubali! Ktk siku ambayo nimeingia humu na kukuta logic sms ni hii yako,nadhani kuna kitu cha ziada unacho kichwani,hivyo ndivyo ilitakiwa kuwa,mpaka sasa nimemuona 1, ambaye amekuja na style yake wengine ni viraza tu kukopi na kupest hadi sumu,nikisema
magufuli anawazidi wote, watu wanabisha,asante sana kwa ufafanuzi huo.
 
baada ya ccm kukataza watangaza nia kushiriki mdahalo ndo nikaelewa kuwa membe ndo chaguo la ccm.wanajua udhaifu wake ndo maana walijua ataaibika

mkuu mdahalo upo kwa watangazani nawaurumia wengine maana vigezo vilivyo wekwa ni aibu.mfn

1,hotuba inayoeleweka
2,nusu ya takwimu za hotuba yako zitoke kichani sio kukopy hadi kumta,
3 muda masaa 3
4,mtiririko uaoeleweka sio kurudi hoja na maneno,
yaani acha kabisa iko burudani

 
Healing of the nation and party needs to be part of the process. Hatuchagui mwenyekiti wa chama kama watia nia wengine walivyosema katika vipaumbele vyao
 
Ndugu yetu Bernard Membe ameanza safari ya matumaini

Source:Mzee Mchopa -M/kiti wa CCM mkoa Lindi 7/06/2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…