Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Ingekuwa vizuri mngekuwa mnatupia na audio za watangaza nia as membe if someone have.
 
Na mashaka na wale aliowatuma kuuliza kama anakubalika au la?

Hata mimi niliwazia hili mkuu, nikawa najadili na mwenzangu tuliyekua tunaangalia nae je ni kweli?
Au jamaa walimuongopea tu kwa kuogopa.............!
Hata hivyo nilitegemea makubwa kuliko nilichokiona.
 
Membe ni mtia nia aliewa disappoint wapambe wake kuliko timu zingine zote ... hotuba ya matambiko na mizimu mwanzo mwisho ...

Sijui team yake huko waliko sasa wana hali gani maana kama mimi tu kanidissapoint vile, vipi wale wenyewe?
 
Sijui team yake huko waliko sasa wana hali gani maana kama mimi tu kanidissapoint vile, vipi wale wenyewe?

Huyu sifa kubwa iliyomfanya autake urais ni kwakuwa ni waziri wa mambo ya nje...kile mwigulu alichokiita urais wa mazoea!
 
Huyu sifa kubwa iliyomfanya autake urais ni kwakuwa ni waziri wa mambo ya nje...kile mwigulu alichokiita urais wa mazoea!

Yeah, kisa Mkapa na Kikwete wote walitoka katika wizara hiyo ndio wakaukwaa urais.
Ila sasa kilichotokea leo......basi tu.
 
Membe kanisikitisha sana badala ya kutangaza vipaumbele vyake na kuomba wana CCM wampendekeze apeperushe bendera ya CCM yeye kaishia kupambana na UKAWA utadhani Ukawa ndio wataingia kwenye NEC ya CCM, poor me.

Halafu kaanza kuomba kura za urais utadhani tayari yuko kwenye kampeni, anajuaje atapita kwenye chekeche lao kabla ya kuja kupambana na UKAWA?

Mambo kama haya ndo hunifanya nisijutie kuishia sekondari, huyo ni balozi wa kimataifa, hawezi kuzingatia terms reference, hiyo kazi anafanyaje? sikumbuki kama kuna mahali amesema tutarajie nini kwake, zaidi alionesha woga wake kwa upinzani...
 
Hiyo ni sentensi ya kichaa kichaa tu. Sasa kama serikali ya Kikwete ipo kwenye msitari sahihi, hiyo inayorudishwa "kwenye msitari huo" ni serikali ya nani?

Ni lazima tuone aibu kuwa na viongozi wa namna hii.
 
Atakuzaje? Nini maana ya huduma bora ama utawala bora ikiwa hazisemi sheria gani atazipitisha. Ndio hayo ya Cyberbill badala ya kutaja specific crimes, sheria inasema matumizi mabatya ya Mitandao.. Ni yapi hayo? oooh hapo tena utawasikia sijui Bulling! kwani walishindwa nini kuandika Bulling katika mitandao ndio crime! badala yake tunaona sheria inayotaka kumlinda Lowassa na mafisadi isiwe kigezo cha kuwabomoa.

Labda nikwambie ukweli, January Makamba nilimpenda kwa sababu ya exposure yake lakini ilipofika swala la kodi za simu, mara kaingia katika hii Cyberbill ili kumlinda Lowassa kiana huku tukiaminishwa ni team tofauti inanipa picha kwamba pengine he bet his chances as plan B itakavyokuwa japo EL anataka yeye tu na kama sio yeye basi hakuna mwingine..

Kwa hiyo, hii habari ya kutangaza sijui nitafanya hivi ama vile wakati unaomba nia ni kujaribu kuleta siasa za nchi za magharibi ambako rais ana wajibu mkubwa wa kujitofautisha katika Vipaumbele vyake akionyesha fedha zitatoka wapi na atakata mambo gani kutokana na bajeti inayotegemewa na wataalam wa mambo hayo wakayajadili.

Yani hakuna unachopindisha mkuu. Hongera sana kwa michanganuo iliyokwenda shule
 
Membe umeniangusha sanaaa yaan mwigulu,makamba wamekupta mbali xnaaa mi nasubr point we unacheza ngoma,mara unajulkana nje,mara usalama upo miaka mingi.mara ukawa wakt ujapta nec.
 
Membe sijaona kama anapointi. Miaka yote hiyo kama waziri kafanya nini? Safari hii hakuna kependeleana na nec hawahongeki
 
Nimekuwa nikisema kuwa Menbe hajui kitu wala kujieleza hawezi...kati ya siku ambazo hotuba za watangaza nia zimeniboa basi ni hii ya Membe yan hadi Mwigulu anamshinda? kwa ccm hadi sasa labda makongoro, prof. muhongo, na mwigulu kwa kujieleza na kujenga hoja.
 
Bila kuvutia upande wowote tuache boyoyo Lowassa amewafunika watangaza nia wooote ukweli unauma huo ndio uhalisia.
 
"nilijiunga Na Ccm Mwaka 1977 Nikiwa Na Miaka 22 Nafasi Ya Kwanza Uongozi Ndani Ya Chama Nilipata 2007"
This Is Foolish Inaonekana Hata Aliekupa Alikupendelea Kama Hata Mkapa Hakukuamini Leo Unakaa Mbele Ya Media's Eti Natangaza Nia Ya Kugombea Urais Haha Kagombee Kwenye Ukoo Wenu
 
Nasikitika kuwa jana moderator alifuta thread yangu iliyotaka wanaJF wajadili uhusiano wa fedha, mabepari na siasa (state capture/power and politics). Nilitaka watu waone ni kwa namna gani watawala wanatekwa nyara na mabepari mapema kabisa wakatiwakianza harakati zao za kusaka uongozi wa kisiasa. Nilitaka wathibitishe hilo kupitia uchambuzi wa presidential bid ya Membe. Kwa wanaotaka kutegua kitendawili cha jana juu uhusiano uliopo baina ya Sir George Kahama na presidential bid ya Membe tafadhali soma hapa
 
- Mwezi Machi mwaka huu nilikwenda Butiama kwenye sherehe za wazanaki,Nilialikwa na Chifu wa wazanaki (Wanzagi), Sikutaka kupoeza hiyo nafasi nilikimbilia haraka ili pia nikazulu kaburi la Baba wa Taifa.

- Nilisali sana kwenye kaburi la baba wa Taifa. Nilimuomba kuhusu kutia nia yangu ya kugombea Urais,kuna viatu ulivyovyiacha alivaa Mzee Mwinyi,Mzee Mkapa na Kikwete,wote hawa viliwatosha. Sasa naomba uniachie mimi nivivae.

- Pia nilimwambia mwalimu kama unaona hivi viatu havinitoshi,wewe na Mungu nipitishieni Mbali kikombe hichi.Lakini timu yangu niliyokuwa nayo iliniambia niombe,nikajiuliza mwalimu Nyerere kanisikiliza.


- Nimemtaja Mwalimu Nyerere kwasababu yeye ndio baba wa Taifa na aliyetuletea uhuru.


2969798700000578-3113860-The_inmates_left_a_note_with_a_smiley_face_reading_Have_a_nice_d-a-81_1433644955628.jpg

 
Back
Top Bottom