JF
Jana kwa !maranyingine tena tumeshudia kituko kingine kwa wanachama wa chama cha watia nia kutoka CCM wakiendelea kutuimbia nyimbo zisizona chembe chembe ya ukweli hata kidogo. Membe katika ubora wake alidai kutembelea kaburi la Mwalimu Butiama na kumuomba mwalimu amsaidie kuvaa vyatu v alivyomwachia Mwinyi, mwinyi kumwachia Mkapa na baadae JK. Sina hakika kama Mwalimu wetu mpendwa alimjibu au kumfukuzia mbali. AIBU!!!!.
Moja ya sababu alioitoa kwa nini anataka kuvivaa hivyo viatu nikwamba vyatu hivvyo bado ni vipyaaaaaa kama alvyoviacha Mwalimu.
Toka jana nimekuwa nikijiuliza kama kweli hvi viatu ni vipya au la. Anaposema viatu ni vipya basi tunategemea kuona vitu alivyoviacha mwalimu vikiendelea kwepo au vikiboreshwa na kuwa imara zaidi.
Kwangu mimi viatu kundelea kuwa vipya basi napata maana mbili; moja ni kwamba viatu havikutumika kabisaa toka mwalimu avivae mara ya mwisho na la pili nikwamba viutu vya mwalimu havipo tena bali viatu alivyoviona membe ikulu sio vilee vya mwalimu bali ni vingine vimeunuliwa vipya kutoka china, vikapakwa kiwi na kuwekwa kona moja hapo ikulu ili kuonyeshea wageni wa i***** kama membe ili kuwazuga.
Mh. Membe hivi uliviona vile vya mwalimu kweli???, siamini mimi!
Kama kweli viatu vya mwalimu vipo basi hatutegemei kuona mafisadi wakidunda mtaani.
Mwalimu hakuacha UFISADI ulokithiri kila kona na kila idara ya serikali, kuanzia magogini kwenyewe mpaka manyumbani kwetu. Kwa ufisadi huu hvi ni kweli viatu vya mwalimu bado vipya??au mheshimiwa haamini kwamba ufisadi umeshatafuna viatu hadi kamba za kufungia viatu.
Kingine kama viatu ni vipya basi tunategemea kuona Azimio la Arusha likiendelea au hata likiboreshwa na kuwa imara zaidi. Basi kwa hili nalo mheshiwa kawa kipofu kabisaaaa na haoni. Watu wamekuwa vipofu kiasi kwamba hawaoni hata aibu kudanganya saa sita mchana kweupeeeee. AIBU GANI HII!!!,
Viwanda alivyojenga mwalimu viko wapi Mh. Membe?? Au unaposema viatu vya mwalimu bado vipya unamaanisha vile vya na 9 vya Bata???, sijaelewa mimi!!. Kila kitu alichoacha mwalimu kimeharibiwa vibaya isipokuwa mipaka ya nchi.
Kwa imani yangu vile vya mwalimu kwanza havikutoshi labda uvikate katikati ili mvivae wawili wewe pamoja na mbuge wangu Wasira. Mkifanya collabo labda mtakaribia karibia namba ya mwalimu.
Nawasilisha