Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Membe Kuwa Rais ni Heri Tuendelee na Kikwete Maana Nionavyo Kwa Membe Maamuzi ni yale yale. Kituko Kingine..
 
Kiukweli Mwigulu ni jembe ukimlinganisha na Membe.
Aliongea kwa muda mrefu tena akiwa na mipango mizuri hadi huchoki kumsikiliza tofauti na leo hotuba fupi halafu hakuna kitu.

Hotuba ya Membe imekosa mipango.Haina plan B zilizojitosheleza elimu yake haitoshi sisi kumpa urais tunachotaka ni uwajibikaji.Kwa mwendo huu Muhongo na Nchemba wanaafadhali.
 
Hahaaaa kazidisha make up huyo. Badala aongee neno eti anacheza. Hivi January anatangaza saa ngapi nia. Huyu Membe hakujipanga.

Nimekua disappointed sana.Nilitegemea makubwa kutoka kwa Membe lakini nilichokiona ni tofauti.
Hivi ungekua mke wa mtangaza nia usingeongea japo jambo kidogo?
Hata kumsifia? Hawa wamama wanatia aibu sana.
 
Kiukweli Mwigulu ni jembe ukimlinganisha na Membe.
Aliongea kwa muda mrefu tena akiwa na mipango mizuri hadi huchoki kumsikiliza tofauti na leo hotuba fupi halafu hakuna kitu.

Mipango yote ya awa jamaa ni uongo mtupu, mipango ya mgombea wa ccm ipo kwenye ilani ya chama ambayo haijatoka bado. Kuhusu mipango ya uongo Mwigulu cha mtoto msubiri January Makamba lazima ukubali uongo wake alivyo nomaaa.
 
Namwona kuna mbunge wa chadema viti maalumu ameenda kujipendekeza kwa membe
 
Mbunge kupitia CHADEMA ameingia kuonyesha upendo...sasa sijui ataitwa msaliti?
 
Tunajua kuwa Mwanamke HISIA ... lakini baby gal hisia zako kwa Mwigulu ziko juu mbinguni ... Msikilize Makongoro labda atakusaidia kuona Upande wa Pili wa shilingi ..
Ngoja nimsubiri January,mka sasa hawa watoa nia aliyetoa speech ya kueleweka ni MWIGULU NCHEMBA PEKE YAKE
 
Uwanja umekuwa disko la wahuni sasa
Kamanda soma hii kiduchu.

Anawaonea huruma wenzao(Upinzani) kuwa tokea mfumo wa vyama vingi hawajawahi kushinda urais.

-Anawashangaa kuwa kila uchaguzi wanaweka mgombea yule yule ambaye anakuwa kama mfamle.

- Kila uchaguzi wanasingizia kuibiwa kura.

- Anasema kuwa wale wafalme hawataki kuachia ngazi na kubadilisha uongozi wa kifalme( Anaelezea sokosoko utakalopata kama ukitaka kugombea nafasi ya juu utafukuzwa kama panya).

- Anasema uongozi ule ule unaoshindwa miaka yote hawawezi kushinda,watachapwa asubuhi mapema.
 
Hapo nimempenda kwenye VETA/UFUNDI ana idea nzuri,kuongeza na kufufua viwanda kutaongeza ajira,pia vijana wataweza hata kujiajiri,ila je atayaweka kwenye VITENDO?

Mkuu Hawa jamaa wanakera halafu wanasikitisha, wanasifia awamu zilizopita kwa utendaji uliotukuka, lakini wana-ahidi kufanya kitu as if hakuna kilichofanywa na awamu hizo.
 
Jamaani hivi january saa ngap ataongea maana membe namuona hana jipya
 
Hotuba ya Membe imekosa mipango.Haina plan B zilizojitosheleza elimu yake haitoshi sisi kumpa urais tunachotaka ni uwajibikaji.Kwa mwendo huu Muhongo na Nchemba wanaafadhali.
Hotuba imejaa mipasho.
 
Hahahahaha
Kama panya...

Rutta yani huyu mtangazania wenu waleo ni sifuri kabisa. Inakuwaje anazidiwa na vitoto vidogo katika siasa kama Mwigulu Nchemba?
Wenda hao wapinzani wa UKAWA wakawa na mapungufu, lakini kwa jinsi alivyo deliver speech kwa kweli ni hovyo bora hata yule wa safarivya matumaini haki ya nani!
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa anajigamba sana, hii inatia wasiwasi juu ya uwezo wake. Nakwamba atalinda maslahi ya viongozi waliopita hata kama walifanya makosa??!

Sijaona tofauti na anayemaliza muda wake ni kuzozaaa to the max
 
You're right... watu wanachanganya mambo kweli kweli... wanadhani pale ni sehemu ya kutangaza sera kumbe ni kutangaza nia... hawafahamu ni mbwembwe tu zilizoibuka hivi karibuni lakini kwa kawaida, hata haya mambo ya kurusha LIVE wala sio lazima lakini bado kuna watu wanatega masikio kusikiliza sera sasa sijui ni sera za kumwahidi nani wakati wanachofanya ni kutafuta ridhaa ndani ya chama ambapo!!! Tusichojua ni kwamba, pale utangaze sera au usitangaze, haimaanishi chochote kwa kuwa sio pahala pake!

Kwa hiyo pale ni kwa ajili ya nini?
 
Back
Top Bottom