Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Duh! Kwa halo waliyonayo magamba, mpaka sasa hakuna mgombea wa ccm kwenye majibu ya watanzania, ninachokiona mbele yao ni giza totoro.
Mpaka sasa sijaona Rais ajaye kupitia ccm.

Na wao hilo wanalijua kuwa urais mwaka huu sio wao
 
Kwa hiyo pale ni kwa ajili ya nini?

Pale ni kwa ajili ya kutangaza nia tu na kuomba ridhaa kwa chama. Zamani hayo mambo yalikuwa yakifanywa ndani ya chama ila kwa kuwa vikao kama halmashauri kuu inahusisha wana CCM wengi ndio maana wameweka huu utaratibu wa kujitangaza kupitia vyanzo mbalimbali. Hii inawahusu wana CCM tu. Huu mkutano sio wa kuwaomba kura kwa Watanzania....Watanzania tutawafuata baada ya kikao cha julai 12 na 13 kukaa.
 
Mipango yote ya awa jamaa ni uongo mtupu, mipango ya mgombea wa ccm ipo kwenye ilani ya chama ambayo haijatoka bado. Kuhusu mipango ya uongo Mwigulu cha mtoto msubiri January Makamba lazima ukubali uongo wake alivyo nomaaa.

Ndio namsubiria kwa hamu.Ila yule hata afanyeje hawezi kunishawishi aisee.
Ila akifanya poa tutampa sifa zake tu ila urais kwake ni ndoto.
 
nimemsikiliza ndugu membe nimegundu kwamba wagombea wa ccm ni weupe sana !
 
Tunajua kuwa Mwanamke HISIA ... lakini baby gal hisia zako kwa Mwigulu ziko juu mbinguni ... Msikilize Makongoro labda atakusaidia kuona Upande wa Pili wa shilingi ..

Makongoro wengi hawajamskia ndio maana wanatushangaa tukimzungumza na sielewi kwa nini ajitokezi watu wamwone. Kiukweli wa kuibadili hii nchi kupitia ccm ni mako peke yake wengine ni mwendelezo wa haya haya.
 
Wapinzani wake ndani ya chama watakuwa waliiba hotuba yake original, wakamuwekea aliyoisoma leo
 
Wote waliotangaza nia kupitia ccm ni Makongoro tu alieonyesha anajua anachokifanya kwa hatua aliyopo.
Membe kanisikitisha sana badala ya kutangaza vipaumbele vyake na kuomba wana CCM wampendekeze apeperushe bendera ya CCM yeye kaishia kupambana na UKAWA utadhani Ukawa ndio wataingia kwenye NEC ya CCM, poor me.

Halafu kaanza kuomba kura za urais utadhani tayari yuko kwenye kampeni, anajuaje atapita kwenye chekeche lao kabla ya kuja kupambana na UKAWA?
 
Steve nyerere naye yupo na kwa wassira alikuwepo.
 
Kama mtu katika dakika kama hii muhimu kabisa ktk maamuzi ya maisha yako na matumaini ya Watanzania unatoa speech nyepesi kama ile mtu huyu anafaa kuwa hata diwani?
 
Membe kanisikitisha sana badala ya kutangaza vipaumbele vyake na kuomba wana CCM wampendekeze apeperushe bendera ya CCM yeye kaishia kupambana na UKAWA utadhani Ukawa ndio wataingia kwenye NEC ya CCM, poor me.

hahahaaah yaani utafikiri ameshapata ridhaa ya chama
 
Kwa ufupi Bernad C Membe ni ndumilakuwili, muoga na mshirikina...!!
Hatakuwa tofauti na Mrisho.....

Kwa uzoefu anaosema anao hakutakiwa kutoa hotuba ya ulaghai na ya hovyo hovyo kiasi kile kile... Anyway inawezekana watu wa kusini na pwani ndo walivo.... Wanapenda soga!!

Nimeambulia tu kuhakikisha (tena kutoka kwa mwanausalama mzoefu) k
 
Mwenyewe kani disappoint sana Leo nilijua ataongea ya maana badala yake kachaganya madesa. Yani nilichotegemea tofauti kabisa.
Hawa wake za viongozi weupe mno hivi hawajifunzagi hata kuongea ili kuonekana wana support. Wanatia aibu hivi utakosaje cha kuongea kumu support mume.

Hivi hawaonagi wenzao akina Hillary Clinton na Michelle Obama? Wale wanawake nawakubali sana.
Walifight hadi waume zao wakashinda.
Hawa sijui wakoje kabisa.
Wanashindwa hata kuwasifia waume zao kua ni bora?
 
Amesema atapigania haki miliki za wanariadha....mwenye ufafanuzi asaidie haki miliki ya mwanariadha ni zipi ? au mmoja akishashinda mbio kwa dakika 10 sekunde saba apewe haki miliki ili mwingine asitumie tena muda huo.

Ah ah ah ah ah ah ah itakuwa ivyo
 
Back
Top Bottom