Tatizo la kufikiria kisiasa badala ya kufikiria kitaifa. Makonda siyo muda wenzetu wa Kenya watawakumbusha wageni kwamba huyu yuko kwenye list ya Marekani na Ulaya kama Muuaji na haruhusiwi kwenda nchi zao.
Hii haitasaidia wageni wetu wa Arusha na Mbuga zetu.
Wangempeleka huko Mwanza kwao.
Naunga mkono hoja, japo sio muuaji kwasababu hajashitakiwa popote!, ila ni kweli sio busara kumpeleka Geneva yetu mtu mwenye makandokando.
Huyu Makonda ana nyota kali sana!.
Wanabodi,
Ukiisikia simulizi za historia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, tangu kuzaliwa, alipotoka, mapito aliyopitia na hadi sasa alipo, na kuifikiria picha ya anapokwenda, baada ya kusoma makala hii na kusikiliza masimulizi haya, mtakubaliana na mimi kuwa, huyu Paul Makonda ni mpakwa Mafuta wa Bwana, hivyo safari yake na mapito yake ni kazi ya Bwana Mungu mwenyewe katika kuonyesha uweza wake kwa wanadamu, na anaweza kuikamilisha safari ya Makonda kwa kuufanya ule muujiza mkubwa wa "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni"!.
Kuna vitu kwa binadamu tuu wa kawaida haviwezekani, lakini kwa Mungu vinawezekana, hivyo kwa Mungu kunauwezekano kabisa wa "Jiwe walilolikataa waashi, likafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".
Huwezi jua jameni, Mwacheni Mungu aitwe Mungu!.
Paskali
Safari ya mafanikio ya huyu kijana, inaendelea..., sasa ni Arusha, soon atarejea DSM, 2025 atashika jimbo na kuingia mjengoni.
Nampongeza huyu Mwamba, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa yaani
RC, ila ilikuwa sio mkoa wa Arusha , ambao ni Geneva ya Africa!, kumpeleka mtu mwenye makandokando ya kunyimwa visa ya Marekani, kunaweza kusiwe na matokeo chanya kwa watalii wa Marekani ambao ndio watalii matajiri zaidi baada ya Waarabu!. Angeweza kurejeshwa DSM au mkoa mwingine wowote lakini sio Arusha!.
Ila kwa maoni yangu, hii teua, tengua, hamish, na tumbua ya Rais Samia, is not healthy at all!, it's a sign of weakness mahali!.
My honest opinion, CCM haina mtu mwingine yeyote ambaye ni the best kwenye uenezi zaidi ya Makonda!.
Ili Rais Samia afanikiwe, asiwasikilize sana wahafidhina wa CCM, sometimes
wanamuingiza chaka!, kama hili la kumuondoa Makonda kwenye uenezi na kumpelekea RChuga , kiukweli kabisa hapa wahafidhina wa CCM, wamemuingiza Mama chaka.
Japo siungi mkono hizi teua leo badilisha kesho, Waenezi 5, ndani ya miaka 5!
1. Polepole
2. Shaka
3. Mjema
4. Makonda
5. The upcoming one!.
Hi sio picha nzuri!, ila nasisitiza kuna tatizo kidogo mahali
Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda tuendelee kumpa muda, ata stabilize.
Hongera Paul Makonda kurudishiwa u RC, very soon itathibitika huyu aliyepo kwenye u RC wa Mkoa wetu hawezi!, soon utarudishwa RC DSM, jiji litanyooka!.
P
P