Kutokana na mabadiliko ya kiutawala Arusha, serikali ikae makini ili jamaa asisababishe wazungu wakatoa travel advisory kwa raia wao

Kutokana na mabadiliko ya kiutawala Arusha, serikali ikae makini ili jamaa asisababishe wazungu wakatoa travel advisory kwa raia wao

Tatizo la kufikiria kisiasa badala ya kufikiria kitaifa. Makonda siyo muda wenzetu wa Kenya watawakumbusha wageni kwamba huyu yuko kwenye list ya Marekani na Ulaya kama Muuaji na haruhusiwi kwenda nchi zao.

Hii haitasaidia wageni wetu wa Arusha na Mbuga zetu.

Wangempeleka huko Mwanza kwao.

Atawanyoosha wenye kibri na jeuri
 
Lucas Mwashamba "Swahiba" wako anakuja Chuga omba appointment ya kuonana naye ofisini kwake upate hata posho ya uchawa wako hapa JF.
 
• Kumbe ni tuhuma 🤔🤔.. Nikahisi labda kuna ushaidi wowote????

• Hao wamarekani ni wanafiki tu, tangu lini wakaipenda Africa??
Kwa nini atuhumiwe yeye na sio Nape, Makamba au mtu mwingine yeyote!? Wamchukie yeye kwa kipi!?
 
Sasa asubiri, mawaziri wote alikiwa anawatukana, sijui nani atampa backup, pale kuna chuma emmanuel nchimbi, hawezi kuruhusu Rais ambaye hataruhusiwa kuingia marekani kwa kuwa ana tuhuma za mauaji, atahudhuriaje vikao vya umoja wa mataifa? Litakuwa linafukuzwa tu kila mahali walipo marafiki wa marekani
Chiembe huna hakili wewe, endelea kuwaza kupitia makalio.....
 
Sijui kwa nini raisi hakushauriwa kwenye hili. Makonda angeweza kupewa ukuu wa mkoa lakini sio Arusha. Yeye ana doa tayari la kuondoa haki ya watu kuishi na sio yeye Wala serikali waliowahi kukana hili. Hata Magu pamoja na kuwa kipenzi chake, hili alilichukulia kwa uzito na akamtoa Makonda kwenye executive. Mama ameingia mkenge ambao ni uchafu kwa hakika kwake.
Vingenvyo hii iwe ni exit door kwa huyu jamaa baada ya kuvurunda kule kwenye uenezi. Strategically, anaweza kuwa amepelekwa Arusha kama njia kuondokea moja kwa moja. Magu pia aliitumia ya namna hii alipomuacha akagombea ubunge na baada ya hapo akasema Kila mkuu wa mkoa aliyeacha ukuu wa mkoa na kwenda kuomba ubunge, akikosa ndio kwa heri hatarudi kuwa mkuu wa mkoa.
Unapigia Mbuzi gita.

Hakuna alichofanya ambacho Wakubwa hawajui.

Na ndio wanamwamini kama kijaana mtiifu kwenye mambo yao.

Sisi wenye maumivu ndio tunaona hafai
 
Sio tu kumpeleka Arusha bali kachemsha kumrudisha kwenye uongozi yule mtu hastahili kabisa kuwa kiongozi wa ngazi yoyote si kwenye chama wala serikalini.
 
Tatizo la kufikiria kisiasa badala ya kufikiria kitaifa. Makonda siyo muda wenzetu wa Kenya watawakumbusha wageni kwamba huyu yuko kwenye list ya Marekani na Ulaya kama Muuaji na haruhusiwi kwenda nchi zao.

Hii haitasaidia wageni wetu wa Arusha na Mbuga zetu.

Wangempeleka huko Mwanza kwao.
Naunga mkono hoja,huyo angeenda Mwanza then yule Mtanda ndio aende Arusha au abadilishane Kituo na RC wa Mbeya aje Arusha then Mtanda aende Mbeya na Makonda aende Arusha.
 
• Mda mwingine tujaribu kupunguza chuki..... Sioni faida yakumusema huyu jamaa kila sekunde..

• Ndani ya Siku mbili hizi, Ni Zaidi ya Threads 10, anajadiliwa makonda... ☹️☹️
Ana kashfa na inaweza kuathiri Utalii na image ya serikali
 
Naunga mkono hoja, japo sio muuaji kwasababu hajashitakiwa popote!, ila ni kweli sio busara kumpeleka Geneva yetu mtu mwenye makandokando.

Huyu Makonda ana nyota kali sana!.
Safari ya mafanikio ya huyu kijana, inaendelea..., sasa ni Arusha, soon atarejea DSM, 2025 atashika jimbo na kuingia mjengoni.

Nampongeza huyu Mwamba, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa yaani
RC, ila ilikuwa sio mkoa wa Arusha , ambao ni Geneva ya Africa!, kumpeleka mtu mwenye makandokando ya kunyimwa visa ya Marekani, kunaweza kusiwe na matokeo chanya kwa watalii wa Marekani ambao ndio watalii matajiri zaidi baada ya Waarabu!. Angeweza kurejeshwa DSM au mkoa mwingine wowote lakini sio Arusha!.

Ila kwa maoni yangu, hii teua, tengua, hamish, na tumbua ya Rais Samia, is not healthy at all!, it's a sign of weakness mahali!.

My honest opinion, CCM haina mtu mwingine yeyote ambaye ni the best kwenye uenezi zaidi ya Makonda!.
Ili Rais Samia afanikiwe, asiwasikilize sana wahafidhina wa CCM, sometimes
wanamuingiza chaka!, kama hili la kumuondoa Makonda kwenye uenezi na kumpelekea RChuga , kiukweli kabisa hapa wahafidhina wa CCM, wamemuingiza Mama chaka.

Japo siungi mkono hizi teua leo badilisha kesho, Waenezi 5, ndani ya miaka 5!
1. Polepole
2. Shaka
3. Mjema
4. Makonda
5. The upcoming one!.

Hi sio picha nzuri!, ila nasisitiza kuna tatizo kidogo mahali Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda tuendelee kumpa muda, ata stabilize.

Hongera Paul Makonda kurudishiwa u RC, very soon itathibitika huyu aliyepo kwenye u RC wa Mkoa wetu hawezi!, soon utarudishwa RC DSM, jiji litanyooka!.
P
P
Wangemfunda tuu na kumpa jadidu za rejea.
 
Kwa nini atuhumiwe yeye na sio Nape, Makamba au mtu mwingine yeyote!? Wamchukie yeye kwa kipi!?
• Kwenye masuala ya siasa, tuhuma ni kitu cha kawaida sana... Labda kama mgeni hapa Tz.

• hii nchi inahitaji viongozi gaidi.. Ila hawa wa kila kitu kupiga makofi kila saa, hawafai hata kwa bure.
 
Kama kuna mtu anawanyima raha wapinzani hapa bongo basi ni Makonda. Yaani hawa jamaa huwa hawependi mtu mchapakazi au anayependwa na wananchi yaani wana wivu wa ajabu na vijitabia vya kususasusa. Mpaka huwa najiuliza hivi hawa wanejiandaa kweli kushika dola au huwa wanaigiza, tu huwezi kuwatofautisha na wanaharakati yaani kutwa kulalamika na kudandia matukio pbadala ya kusema wakipewa dola watalifanyia nini taifa.
Kama unadhani upinzani hawampendi think again, ndani ya chama chenyewe ndio maadui zake wakubwa walipo, unajua kilichomtoa kwenye uenezi?
 
Ana kashfa na inaweza kuathiri Utalii na image ya serikali
• Kuna mwananchi yeyote amefaidika na huo utalii Zaidi ya viongozi wa CCM ??

• Au utaniambia waliojenga hotels ndo wanafaidikia(wananchi)??
 
• Mda mwingine tujaribu kupunguza chuki..... Sioni faida yakumusema huyu jamaa kila sekunde..

• Ndani ya Siku mbili hizi, Ni Zaidi ya Threads 10, anajadiliwa makonda... ☹️☹️
Hata mashuleni au mtaani wapo mademu wa namna hiyo ila ukitazama kwa makini hali hiyo uitaka wenyewe ujiona wao ndio wao hata akinunua kiatu anataka kiwe gumzo mtaa mzima.Sasa makonda wako yuko pele kwa matazamio baada ya kuvurunda uenezi kwahiyo akae pale huku akijifunza kwa wakuu wa mikoa wengine bila hivyo atafyekelewa mbali, mara ooh! sitaki kuona lubega mjini, mwende mkavae suruali, mara ooh! Kutembea na visu ni marufuku, nimsikia kwenye bomba.
 
Tatizo la kufikiria kisiasa badala ya kufikiria kitaifa. Makonda siyo muda wenzetu wa Kenya watawakumbusha wageni kwamba huyu yuko kwenye list ya Marekani na Ulaya kama Muuaji na haruhusiwi kwenda nchi zao.

Hii haitasaidia wageni wetu wa Arusha na Mbuga zetu.

Wangempeleka huko Mwanza kwao.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imemwekea vikwazo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Christian Makonda kwa madai ya kuhusika katika uvunjifu kamili wa haki za binadamu na tuhuma nyingine. Pia vikwazo hivyo amewekewa mke wake Makonda, Mary Felix Massenge.
Taarifa iliotolewa Ijumaa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeelezea tuhuma hizo ni uvunjaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa siasa za upinzani, ukandamizaji wa haki ya kujieleza na mikusanyiko, na kuwakandamiza watu ambao wanatengwa katika jamii.
Wizara ya Mambo ya Nje inasema ina taarifa zakuaminika kuwa Makonda alihusika katika uvunjaji wa amani katika nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Sheria ya Marekani inaagiza kuwa, katika hali ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ana habari za kuaminika kwamba maafisa wa nchi nyingine wamehusika na ufisadi mkubwa au ukiukaji wa haki za binadamu, watu hao na wana familia wa karibu hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani.
Marekani inasema ina wasiwasi kwa kuendeleakukosekana uzingatiaji wa haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania.
Hii ni pamoja na hatua ya serikali ya Tanzania inayochukua kukandamiza uhuru wa kujieleza, uhuru wa kujiunga na chama, uhuru wa mikutano ya Amani; kulengwa kwa watu wanaotengwa na vyama vya upinzani vya siasa, na hatarisho la maisha ya watu.
 
• Kuna mwananchi yeyote amefaidika na huo utalii Zaidi ya viongozi wa CCM ??

• Au utaniambia waliojenga hotels ndo wanafaidikia(wananchi)??
Wewe una upumbavu kuanzia kichwani Hadi matrakooo ,napoyeza mda kujadiliana na wewe
 
Tatizo la kufikiria kisiasa badala ya kufikiria kitaifa. Makonda siyo muda wenzetu wa Kenya watawakumbusha wageni kwamba huyu yuko kwenye list ya Marekani na Ulaya kama Muuaji na haruhusiwi kwenda nchi zao.

Hii haitasaidia wageni wetu wa Arusha na Mbuga zetu.

Wangempeleka huko Mwanza kwao.
Makonda ana kesi ya kutishia kuua
Hizo ndo sera za ccm Kuuana , juzi walitaka kumuua sendeka kisa anatetea wamasai wa ngorpngoro
 
Hata mashuleni au mtaani wapo mademu wa namna hiyo ila ukitazama kwa makini hali hiyo uitaka wenyewe ujiona wao ndio wao hata akinunua kiatu anataka kiwe gumzo mtaa mzima.Sasa makonda wako yuko pele kwa matazamio baada ya kuvurunda uenezi kwahiyo akae pale huku akijifunza kwa wakuu wa mikoa wengine bila hivyo atafyekelewa mbali, mara ooh! sitaki kuona lubega mjini, mwende mkavae suruali, mara ooh! Kutembea na visu ni marufuku, nimsikia kwenye bomba.
• Naona unatoa ya moyoni!

• Ebu nipe sababu za msingi kwa nini unamchukia makonda?? Pengine naweza kukuelewa unachotetea.
 
Back
Top Bottom