Kutokana na Maelezo ya Tundu Lissu, Mwalimu Nyerere ndio chanzo cha utawala mbovu unaoendelea Afrika Mashariki

Kutokana na Maelezo ya Tundu Lissu, Mwalimu Nyerere ndio chanzo cha utawala mbovu unaoendelea Afrika Mashariki

😁😁😁😁 wewe adriz akili zako finyu sana yani Tundu lissu ndiyo mwalimu wako 😁😁😁 Tundu lisu ana akili ndogo sana ...mambo hayo niulize mimi .....Matatizo ya tanzania ya sasa yanatokana na (Mfumo Siasa) wa
1)SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIBEPARI......huu mfumo Nyerere hausiki nao ulianza zama za mzee MWINYI na ndiyo chanzo cha haya yote ....

KUNA MIFUMO 4 TU YA UJAMAA NA UBEPARI NAYO NI

πŸ’₯1)SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIJAMAA (Nyerere system)

πŸ’₯2)SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIBEPARI (mwinyi mkapa kikwete na samia system)

πŸ’₯3)SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIJAMAA (huu hatujawai kuutumia )

πŸ’₯4)SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIBEPARI (huu mfumo Rais pekee aliye utumia ni JPM)

Leo watanzania tumwfanyiwa STATE CAPTURE kwa sababu ya UBEPARI WA KISERIKALI ....
MFUMO NO 4 NDIYO MFUMO SAHIHI KABISA.
Kabla sijakosoa maoni yako , wapi nimesema nasapoti maoni ya Lisu au kauli zake ? Mimi si nimeweka tu alichosema na kudai ?
 
Moja kwa moja.

Nilikuwa natazama kwa umakini YouTube hoja za Lisu wakati alipoalikwa kuongea katika kongamano Moja katika chuo cha Makerere Uganda.

Kutokana na Maelezo yake alimsifia Mwalimu kwa jitihada zake za ukombozi Afrika , kutopenda ufisadi na kujilimbikizia Mali Kisha akaenda kwenye point yake kuu kuwa Mwalimu kapanda mbegu mbaya sana ya utawala mbovu Tanzania na hiyo ikaota mizizi kwa vijana wake wa karibu aliowalea Museveni na Kagame nao wanatumia Misingi ya Mwalimu katika kufanya mabaya katika tawala zao.

Kutokana Maelezo yako amesema Mwalimu kaacha mbegu na Legacy hizi ambazo zinatumiwa vibaya na watala wa Afrika Mashariki.

1. Imperial Presidency (Uraisi Wenye mamlaka kupitia kiasi kama Mfalme ) .
Katiba ilimpa Rais mamlaka makubwa sana: kuwa Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, na pia uwezo wa kuteua Makamu wa Rais, Mawaziri, na kuvunja Bunge katika mazingira fulani. Sheria kama Preventive Detention Act zilimruhusu Rais kumweka mtu kizuizini bila mashitaka, na marekebisho ya baadaye yakaruhusu pia kuteua wabunge kadhaa, jambo lililoimarisha zaidi urais kuliko Bunge na taasisi huru.

2. Politicization of military ( Siasa kuingia jeshini ; jeshi kufanywa kama Chombo Cha siasa.

Badala ya kuwa taasisi huru ya kitaaluma. Hii ilimaanisha kuwa wanajeshi walichaguliwa na kulelewa kisiasa na CCM, hivyo siasa za chama zikapenya ndani ya jeshi na kuzuia uwezekano wa jeshi kuwa chanzo cha upinzani wa wazi kwa utawala.

Hivyo, jeshi na vyombo vya usalama vikawa sehemu ya uti wa mgongo wa chama na urais, jambo linalolinda utawala uliopo lakini pia linafanya taasisi za usalama zionekane kama chombo cha siasa badala ya chombo cha kitaifa tu.

3. Militarization of Politics : (Hii sijui kuichambua na kuelezea wataalamu nisaidieni) .

Summary : Nguvu ya watawala katika kufanya wanayotaka , kuendesha nchi kibabe , uminywaji wa demokrasia nk katika nchi za Tanzania , Uganda na Rwanda ni matunda ya mbegu aliopanda Mwalimu Nyerere.

#UziTayari
Nyerere alikuwa na nia nzuri bila kujua kuwA iko siku atakufa alijitaidi kuwa mungu wa Tanzania,,mwishowe akaambulia ubaba wa taifa
 
Ccm hawako tayari kwa katiba ya kweli. Wanajua kabisa ikija katiba ya kweli wao ndio watatolewa madarakani, kwani tayari kizazi hiki kimeichoka. Kama ww ni muumini wa ukweli unaweza kuona ile voters turnout ya juzi ilivyokuwa ndogo. Kiuhalisia ccm zile ndio huwa kura zake, lakini hupora za wapinzani na kusema ni zao. Na vyombo vya dola na tume ndio hulinda na kuwapatia ccm ushindi huo haramu. Na ccm ikipoteza kiti cha urais haitakaa inyanyuke tena na huensa ikawa historia. Rejea KANU ya Kenya.
Watatolewa madarakani na kushitakiwa pia kwa madhambi waliyoyafanya wakiwa watawala hiyo ndio hofu yao kubwa.
Maana wapinzani watakapochukua nchi hawataishis kwenye kutawala tu bali wataanza kupekua mafaili ya miaka ya nyuma kuangalia makosa yaliyotendeka ili kuwaadhibu wakosaji.
 
Naona kama uhuru ungepiganiwa na watu kama Lissu na Heche tungepata uhuru wa kweli kuliko wa Nyerere wa kutuuza kwa CCM.

TAasisi hazipo huru, jeshi halipo huru polisi hawapo huru, PCCB wala CAG wote wanapokea maelekezo. Sasa hiyo ni nchi au kituko?
 
Moja kwa moja.

Nilikuwa natazama kwa umakini YouTube hoja za Lisu wakati alipoalikwa kuongea katika kongamano Moja katika chuo cha Makerere Uganda.

Kutokana na Maelezo yake alimsifia Mwalimu kwa jitihada zake za ukombozi Afrika , kutopenda ufisadi na kujilimbikizia Mali Kisha akaenda kwenye point yake kuu kuwa Mwalimu kapanda mbegu mbaya sana ya utawala mbovu Tanzania na hiyo ikaota mizizi kwa vijana wake wa karibu aliowalea Museveni na Kagame nao wanatumia Misingi ya Mwalimu katika kufanya mabaya katika tawala zao.

Kutokana Maelezo yako amesema Mwalimu kaacha mbegu na Legacy hizi ambazo zinatumiwa vibaya na watala wa Afrika Mashariki.

1. Imperial Presidency (Uraisi Wenye mamlaka kupitia kiasi kama Mfalme ) .
Katiba ilimpa Rais mamlaka makubwa sana: kuwa Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, na pia uwezo wa kuteua Makamu wa Rais, Mawaziri, na kuvunja Bunge katika mazingira fulani. Sheria kama Preventive Detention Act zilimruhusu Rais kumweka mtu kizuizini bila mashitaka, na marekebisho ya baadaye yakaruhusu pia kuteua wabunge kadhaa, jambo lililoimarisha zaidi urais kuliko Bunge na taasisi huru.

2. Politicization of military ( Siasa kuingia jeshini ; jeshi kufanywa kama Chombo Cha siasa.

Badala ya kuwa taasisi huru ya kitaaluma. Hii ilimaanisha kuwa wanajeshi walichaguliwa na kulelewa kisiasa na CCM, hivyo siasa za chama zikapenya ndani ya jeshi na kuzuia uwezekano wa jeshi kuwa chanzo cha upinzani wa wazi kwa utawala.

Hivyo, jeshi na vyombo vya usalama vikawa sehemu ya uti wa mgongo wa chama na urais, jambo linalolinda utawala uliopo lakini pia linafanya taasisi za usalama zionekane kama chombo cha siasa badala ya chombo cha kitaifa tu.

3. Militarization of Politics : (Hii sijui kuichambua na kuelezea wataalamu nisaidieni) .

Summary : Nguvu ya watawala katika kufanya wanayotaka , kuendesha nchi kibabe , uminywaji wa demokrasia nk katika nchi za Tanzania , Uganda na Rwanda ni matunda ya mbegu aliopanda Mwalimu Nyerere.

#UziTayari

Adriz: Hauko mbali na ukweli, licha ya mambo mengi ambayo unaweza kumpa credit, Nyerere pia kwa sehemu kubwa ndio shina la matatizo tunayo hangaika nayo leo. Kwangu nayaona haya:

1.Katiba: Jinamizi la Katiba hii kandamizi inayotusumbua leo, ni zao la Nyerere, yeye ndiye aliyetengeneza Rais kuwa ni mfalme, na alipotuingiza kwenye mfumo wa vyama vingi, hakutoa hata wazo la kuibadilisha Katika iendane na mfumo wa vyama vingi. Hili ni tatizo kubwa mno ambali Nyerere ametuachia Watanzania, kwa kifupi amewaachia CCM mtihani mkubwa sana, Samia amejikuta ndani ya tatizo ambalo wala siyo yeye mwanzilishi, na anaogopa kuingia katika historia kwa kukubali kuibadili Katiba ya Tanzania, ambayo itatoa mwanya mkubwa ambayo unaweza hata kuiondoa CCM madarakani.

2.Muungano.: Nyerere altuachia kitu ambacho kitalisumbua taifa hili sana! In short Muungano hauna logic yoyote ile, na inaonekana hata CCM wenyewe ( upande wa bara) wanaogopa kuuzungumza, na visiwani ile political top class wanaukumbatia kwa sababu unawanufaisha! Sijui kama ukipitisha referundum leo Muungano utasimama.

Kwangu mimi, haya ndio matatizo makubwa mno ambayo Nyerere ametuachia, na tusipo yafanyia kazi yataendelea kututesa kwa muda mrefu, na kuudhohofisha mnao maendeleo ya taifa.
 
Mkapa hata elfu malim seif alikuwa ameshinda anaanda kutangazwa ghafla mkapa akaenda zanzibar kupindua matokeo alafu ghafla baadae anatuambia anatamani uchaguzi wa haki Tanzania kilikuwa ni kituko cha mwaka

Yote hayo ni mfumo aliotuachia Nyerere, Muungano ni vigumu kuwepo kama Visiwani watakuwa na Rais Nje ya CCM, na uchaguzi wa Huru na Haki ni vigumu mno kutokea ndani ya Katika hii, na Huwezi kabisa kurekebisha sheria za Uchaguzi bila kuuguza Muunganio na mamlaka hasa ya Rais!
 
Hata kama ni kweli, Nyerere alishakufa robo karne tayari ishapita, so tumeshindwa kabisa kurekebisha hayo unayosema ni chanzo cha utawala mbovu hadi leo? Au tusubiri afufuke aje arekebishe? Ina maana kizazi cha sasa hakina akili kabisa zaidi ya Nyerere hata tukiunganishwa wote milioni 70+. Basi tuna shida kubwa sana vichwani mwetu kama ndivyo

Common sense is not common
 
Nyerere alikuwa na nia nzuri bila kujua kuwA iko siku atakufa alijitaidi kuwa mungu wa Tanzania,,mwishowe akaambulia ubaba wa taifa

Adriz: Kosa kubwa alilolifanya ni kujaribu kuwa "mungu" wa Taifa....Hakuacha kabisa mfumo thabiti, na tatizo kubwa leo ni kuwa Rais wa Tanzania ni "mungu" ameshika hatima ya serikali nzima, inatisha mno!
 
Tunatumia saikolojia kutambua akili na nia za watu ..hasa waislamu wanapenda sana kumdunisha nyerere kana kwamba wao wangekuwa viongozi nchi ingekuwa tukufu sana kumbe wao ndiyo wahalibifu kamili na walio dhahili kabisa kwa vitendo vyao na nia zao mbovu na dhalimu
Kabla sijakosoa maoni yako , wapi nimesema nasapoti maoni ya Lisu au kauli zake ? Mimi si nimeweka tu alichosema na kudai ?
 
Hata kama ni kweli, Nyerere alishakufa robo karne tayari ishapita, so tumeshindwa kabisa kurekebisha hayo unayosema ni chanzo cha utawala mbovu hadi leo? Au tusubiri afufuke aje arekebishe? Ina maana kizazi cha sasa hakina akili kabisa zaidi ya Nyerere hata tukiunganishwa wote milioni 70+. Basi tuna shida kubwa sana vichwani mwetu kama ndivyo

Common sense is not common

Mkuu, ukweli tumeshindwa! Huoni kabisa kila attempt ya kubadili katika inakuwa ngumu! na kuujadili Muungano inakuwa ni kama kanuni ya dini...Na Ccm kwa vil;e inafaidika na mfumo huo, haiwezi kabisa kuubadili!
 
Tunatumia saikolojia kutambua akili na nia za watu ..hasa waislamu wanapenda sana kumdunisha nyerere kana kwamba wao wangekuwa viongozi nchi ingekuwa tukufu sana kumbe wao ndiyo wahalibifu kamili na walio fhahili kabisa kwa vitendo vyso na nia zao mbovu na dhalimu

Sijui kabisa nia ya Adriz kuleta post yake, najua kuna ukweli ndani yake kuwa baadhi ya Waislamu wana chuki binafsi na Nyerere, lakini ukweli wa aliyoyafanya Nyerere yako wazi ! Aliweza kuujenga utaifa, nchi nyingi za Kiafrika baada ya Uhuru zilisumbuliwa na hilo, lakini katika kuujenga Umoja wa Kitaifa alitengeneza kitu kingine ambacho kina litesa taifa hili.

Narudia kusema sijui Adriz kaleta mada hii kumtweza Nyerere, au kaleta mada hii kwa nia safi. Naufahamu mno msimamo wa Adriz katika mada nyingi, hivyo inawezekana kabisa unalosema Mkuu.
 
Hata kama ni kweli, Nyerere alishakufa robo karne tayari ishapita, so tumeshindwa kabisa kurekebisha hayo unayosema ni chanzo cha utawala mbovu hadi leo? Au tusubiri afufuke aje arekebishe? Ina maana kizazi cha sasa hakina akili kabisa zaidi ya Nyerere hata tukiunganishwa wote milioni 70+. Basi tuna shida kubwa sana vichwani mwetu kama ndivyo

Common sense is not common

Mkuu mfumo aliotuachia Nyerere hata kama aliutengezeza kwa nia safi uko outdated leo! CCM hawataki kabisa ubadilike, unaweza kuwekewa kosa la Uhaini, Kama tumeshindwa kuirekebisa Katiba, na kama ni kosa la jinai kuuzungumza Muungano huoni kua aina wehu katika akili za Watanzania!
 
Lisu huwa namuelewa sana anapoongea kuhusu madhara ya utawala wa Nyerere ndani ya nchi hii. Kwa mbegu hii aliyopanda Nyerere ni machafuko pekee yatamaliza kabisa laana ya kiutawala aliyoacha Nyerere ndani ya nchi hii. Kwenye hili lazima wengi tutamwaga damu ili kuondoa tambiko hilo.
Tindo: Tunaweza kumpa Nyerere sifa nyingi kwa taifa hili, lakini ukweli haukimbiliki, ametuachia mfumo mbaya mno wa kiutawala, na CCM wanalijua hilo kabisa, ukiubadili mfumo huu, anguko la CCM ni kubwa, ndio maana wanatumia njia zote kuutetea mfumo huu! Lakini ni mpaka lini? Je CCM watetea huo mfumo outdated kwa gharama kama tulizoona October 29! Watanzania tumekuwa kituko ulimwenguni kote!
 
Yote yanawezekana Tindo, hivyo waweza kuwa sahihi.

Ila ningetamani tukwepe fujo, fursa tunayo ya kufanya hilo including CCM wanayo option ya kuruhusu true election na bado wakabaki ktk siasa za Tanzania, Mfano wanaweza limit vyama vikawa viwili tu! Hio itakuwa gurantee ya wao kubaki ktk siasa.
WaTz na sio ccm, ndio waseme wawe na vyama vingapi, na hii iwe katika miongozo ya katiba mpya ya wananchi.
 
WaTz na sio ccm, ndio waseme wawe na vyama vingapi, na hii iwe katika miongozo ya katiba mpya ya wananchi.
Wazo la kutoa limit ya vyama ni kuiminya Demokrasia....Wache viwe vingi tu.....Ushindani wa haki utaviuwa tu!
 
Tindo: Tunaweza kumpa Nyerere sifa nyingi kwa taifa hili, lakini ukweli haukimbiliki, ametuachia mfumo mbaya mno wa kiutawala, na CCM wanalijua hilo kabisa, ukiubadili mfumo huu, anguko la CCM ni kubwa, ndio maana wanatumia njia zote kuutetea mfumo huu! Lakini ni mpaka lini? Je CCM watetea huo mfumo outdated kwa gharama kama tulizoona October 29! Watanzania tumekuwa kituko ulimwenguni kote!
Mimi haya hata sahivi yanayotokea Tanzania ni matokeo ya Nyerere na katiba yake ya 1977 na mbaya zaidi yeye Nyerere alijua wazi hii katiba ni mbovu ila hakutaka kubadilisha

Yaani kwenye katiba unaweka kipengele eti hatakiwi kushtakiwa sasa kwani Rais asifanye mambo ya hovyo kwa sababu ana-kinga tayari

Sijuagi kwanini watu wanamsifia Nyerere kwenye swala la uongozi amefeli sana kwenye uongozi wa Tanzania alitengeneza madikteta kupitia katiba

Sidhani kuna mtu wa ccm hata hawa wakina mpango wataweza badilisha hii katiba sababu wakibadilisha na kuwa nzuri, ccm ndo bye bye
 
Dennis: CCM iko njia panda sasa hivi, njia ya kwanza ni kuendelea kufanya kama walivyofanya miaka yote, nikiwa na maana ya kuizuia sauti ya Reform hata kwa gharama ya damu, njia hiyo ni mbaya kwao wenyewe na ina mwisho mbaya mno! Njia ya pili ni kukubali Reform na kukubali uhalisia wa sasa hivi, dunia imebadilika sana, na jamii ya Tanzania, na teknolojia si ile ya miaka ya 90.....Hivyo CCM ni kuubali ukweli huo mchungu, na kujua wazi unaweza kuiweka CCM pembeni, na hata Muungano pia. Ni ukweli usiokimbilika, ila hatujui CCM itachagua njia ipi.
 
Tunatumia saikolojia kutambua akili na nia za watu ..hasa waislamu wanapenda sana kumdunisha nyerere kana kwamba wao wangekuwa viongozi nchi ingekuwa tukufu sana kumbe wao ndiyo wahalibifu kamili na walio fhahili kabisa kwa vitendo vyso na nia zao mbovu na dhalimu
Hapo ndio mageuzi ya nchi yanapokuwa magumu!

Kifupi mna mchosha Tundu Lissu bure
 
Back
Top Bottom