Kutokana na Maelezo ya Tundu Lissu, Mwalimu Nyerere ndio chanzo cha utawala mbovu unaoendelea Afrika Mashariki

Dennis: CCM iko njia panda sasa hivi, njia ya kwanza ni kuendelea kufanya kama walivyofanya miaka yote, nikiwa na maana ya kuizuia sauti ya Reform hata kwa gharama ya damu, njia hiyo ni mbaya kwao wenyewe na ina mwisho mbaya mno! Njia ya pili ni kukubali Reform na kukubali uhalisia wa sasa hivi, dunia imebadilika sana, na jamii ya Tanzania, na teknolojia si ile ya miaka ya 90.....Hivyo CCM ni kuubali ukweli huo mchungu, na kujua wazi unaweza kuiweka CCM pembeni, na hata Muungano pia. Ni ukweli usiokimbilika, ila hatujui CCM itachagua njia ipi.
Kama wana tatizo kubwa kwasasa ni kuwa na Mwenyekiti ambae anaweza kuwa easily targeted na wapinzani kwasababu ya ukanda (siasa za Tanganyika na zanzbari), jinsia na dini.

Hata kama wengi mnaweza msilione, ila Zanzbar imekuwa pilot ya CCM kunako ushindani wa kisiasa! Kama katiba ni hii, bado sijaona tishio la CCM mpaka sasa.
 
Unadhani wataishikilia Katiba hii?
 
Unadhani wataishikilia Katiba hii?
Ni vigumu ku-predict nini kitatokea kwakeli.

Shida hata hao wanao sukuma hio kete ya katiba wanaweza sahau tena jambo hili ktk hali isiyo elezeka japo wao wenyewe wataweza defend position yao hio mpya.
 
Na si kwamba Gen Z walikuwa hawajazaliwa.

Nyerere alienda na fimbo UDSM akawatandika fimbo, akafunga chuo.

Wakarudi kwa masharti makali ya Naapa Naahidi Mbele ya Chama, Mapinduzi ntakulinda mpaka kufa....

Akateka wakina Hanga, akatukana kina Kambona, akafukuza chamani kina Marsha.

Masha alikuwa Humfrey Polepole wa TANU, Katibu Mwenezi 1967, akafukuzwa TANU. Halafu akaagiza mtu yeyote atakaempa kazi atakiona cha mtema kuni.

Uzeeni Nyerere akajuta akasema, sikutegemea nimejenga Taifa la waoga kiasi hiki, Mungu nisamehe.
 
Sidhani uhitaji wa Katiba mpya utasahaulika, maana somo limewaingia atu wengi, na Internationa community, au wapatanishi wowote kutoka nje watasimamia hilo! Sidhani kabisa utafanyika uchaguzi mwingine bila kufanyia kazi hilo, kwangu naliona halikimbiki kabisa.
 
Sijui kabisa nia ya Adriz kuleta post yake, najua kuna ukweli ndani yake kuwa baadhi ya Waislamu wana chuki binafsi na Nyerere, lakini ukweli wa aliyoyafanya Nyerere yako wazi ! Aliweza kuujenga utaifa, nchi nyingi za Kiafrika baada ya Uhuru zilisumbuliwa na hilo, lakini katika kuujenga Umoja wa Kitaifa alitengeneza kitu kingine ambacho kina litesa taifa hili.

Narudia kusema sijui Adriz kaleta mada hii kumtweza Nyerere, au kaleta mada hii kwa nia safi. Naufahamu mno msimamo wa Adriz katika mada nyingi, hivyo inawezekana kabisa unalosema Mkuu.
Nyerere hakuwa na nia mbaya na taifa ...nilisha towaga elimu hapa JF kuhusu kukwama kwa siasa za nyerere kiuchumi na ukisoma post yangu ya kwanza niliyo mjibu adriz utaona hiyo mifumo minne niliyo onyesha nyerere alikosea kwa kufuata mfumo wa
1)SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIJAMAA (huu mfumo ni mbaya ila hauna sana stress, ila una sababisha taifa kuwa goi goi na slow lisilo na ushindani wa kimaendrleo ndani yake ...watu wote wanakuwa na mtindo wa maisha kama wa wazaramu ...wanakuwa awana haja ya haraka ya maendeleo)

mfumo tuliopo sasa ni mbaya na muovu kuliko ule wa nyerere nao ni

2)SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIBEPARI (huu mfumo unafanya serikali kuwa mali ya kikundi kidogo kwa maslai yao binafsi na familia zao na mara zote mfumo huu unachukia siasa za UZALENDO NA WAZALENDO ....mfumo huu umeanza kutumika na Rais Mwinyi na baadae Mkapa na baadae Kikwete na sasa Samia ....ni mfumo wa hatari sana wenye ufisadi mbaya sana ..

Mfumo sahihi uliopaswa kufuatwa ni huu wa

3)SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIBEPARI (Mfumo huu rais pekee aliye ufuata ni JPM )
 
Na si kwamba Gen Z walikuwa hawajazaliwa.

Nyerere alienda na fimbo UDSM akawatandika fimbo, akafunga chuo.

Wakarudi kwa masharti makali ya Naapa Naahidi Mbele ya Chama, Mapinduzi ntakulinda mpaka kufa....

Akateka wakina Hanga, akatukana kina Kambona, akafukuza chamani kina Marsha.

Masha alikuwa Humfrey Polepole wa TANU, Katibu Mwenezi 1967, akafukuzwa TANU. Halafu akaagiza mtu yeyote atakaempa kazi atakiona cha mtema kuni.

Uzeeni Nyerere akajuta akasema, sikutegemea nimejenga Taifa la waoga kiasi hiki, Mungu nisameh
Ni Kweli alitoa hayo maneno, ila sijui kama kweli alijuta, maana kama kweli aliona ni tatizo naamini alikuwa na influence ya kubadili hayo aliyo ona ni makosa.

Kuhusu katiba, Tume ya kwanza ya mambo haya ya kisiasa ilipendekeza mabadiliko ya katiba Nyerere akiwa hai, na wote walikataa mabadiliko hayo. Ukweli ni kuwa baba wa taifa alikusudia mfumo huo uwepo.
 
Na si kwamba Gen Z walikuwa hawajazaliwa.

Nyerere alienda na fimbo UDSM akawatandika fimbo, akafunga chuo.

Wakarudi kwa masharti makali ya Naapa Naahidi Mbele ya Chama, Mapinduzi ntakulinda mpaka kufa....

Akateka wakina Hanga, akatukana kina Kambona, akafukuza chamani kina Marsha.

Masha alikuwa Humfrey Polepole wa TANU, Katibu Mwenezi 1967, akafukuzwa TANU. Halafu akaagiza mtu yeyote atakaempa kazi atakiona cha mtema kuni.

Uzeeni Nyerere akajuta akasema, sikutegemea nimejenga Taifa la waoga kiasi hiki, Mungu nisamehe.
Nyerere alikuwa na utisho binafsi, he was a "mystic" figure mwenye utishio binafsi, kama madikteta wengi enzi za Ukomunist! CCM Haina mtu wa namna hiyo, na hatakuwepo! Na ni dunia nyingine kabisa! CCM wamebakiwa na Dola tu! Ungelitegemea licha vitisho vya Rais SAMIA kuna mtu angelitoka October 29? Angalau hata Mkapa alikuwa na utisho huo! Nakumbuka mitandao imepunguza mno ule utisho wa viongozi, nyuma ya keyboard kunaondoa woga na wasi wasi.....
 
Sidhani uhitaji wa Katiba mpya utasahaulika, maana somo limewaingia atu wengi, na Internationa community, au wapatanishi wowote kutoka nje watasimamia hilo! Sidhani kabisa utafanyika uchaguzi mwingine bila kufanyia kazi hilo, kwangu naliona halikimbiki kabisa.
Sawa, ila usisahau kuwa kama kuna kipindi katiba ilidaiwa kwa kasi na mchakato ukaanza ni miaka ya 2010 hadi 2015, na bado haikupatikana.
 
Nyerere alikuwa na utisho binafsi, he was a "mystic" figure mwenye utishio binafsi, kama madikteta wengi enzi za Ukomunist! CCM Haina mtu wa namna hiyo, na hatakuwepo! Na ni dunia nyingine kabisa! CCM wamebakiwa na Dola tu! Ungelitegemea licha vitisho vya Rais SAMIA kuna mtu angelitoka October 29? Angalau hata Mkapa alikuwa na utisho huo! Nakumbuka mitandao imepunguza mno ule utisho wa viongozi, nyuma ya keyboard kunaondoa woga na wasi wasi.....
Oktoba 29 ilikumbana na mambo mengi kidogo, kwa kifupi ni mchanganyiko wa dini + Siasa na harakati, sababu hizi hasa hilo la kwanza ilikuwa ni lazima watu watoke
 
Ni Kweli alitoa hayo maneno, ila sijui kama kweli alijuta, maana kama kweli aliona ni tatizo naamini alikuwa na influence ya kubadili hayo aliyo ona ni makosa.

Kuhusu katiba, Tume ya kwanza ya mambo haya ya kisiasa ilipendekeza mabadiliko ya katiba Nyerere akiwa hai, na wote walikataa mabadiliko hayo. Ukweli ni kuwa baba wa taifa alikusudia mfumo huo uwepo.

Hivyo Kwa Nyerere kukataa mabadiliko ya Katika akiwa hai, hawezi kukwepa dhambi ya kutuweka tulipo leo! Utaweza kuwa na mfumo wa vyama vingi, ukabakiwa na mfumo wa Katika wa chama kimoja? Kuna siku injini ya siasa ita kwama tu! Dunia inabadikika haraka mno!
 
Oktoba 29 ilikumbana na mambo mengi kidogo, kwa kifupi ni mchanganyiko wa dini + Siasa na harakati, sababu hizi hasa hilo la kwanza ilikuwa ni lazima watu watoke
Labda unifafanunulie kuhusi dini! Kuna chuki kubwa dhidi ya CCM naiona, maana hata zoezi la kupiga kura lilidorora kwa sehemu, utasemaje kuhusu hilo?
 
Kama wana tatizo kubwa kwasasa ni kuwa na Mwenyekiti ambae anaweza kuwa easily targeted na wapinzani kwasababu ya ukanda (siasa za Tanganyika na zanzbari), jinsia na dini.

Hata kama wengi mnaweza msilione, ila Zanzbar imekuwa pilot ya CCM kunako ushindani wa kisiasa! Kama katiba ni hii, bado sijaona tishio la CCM mpaka sasa.

Mkuu unaamini CCM ilipata 98% ? Kama hakuna tishio, Kwa nini Lisu yuko ndani, hakuwepo kwenye ulingo?
 
Hivyo Kwa Nyerere kukataa mabadiliko ya Katika akiwa hai, hawezi kukwepa dhambi ya kutuweka tulipo leo! Utaweza kuwa na mfumo wa vyama vingi, ukabakiwa na mfumo wa Katika wa chama kimoja? Kuna siku injini ya siasa ita kwama tu! Dunia inabadikika haraka mno!
Yes, mimi kwa maono yangu hata lile la kuwaambia kamati kuu ya CCM waende ktk siasa za vyama vingi licha ya kura ya maoni kuonesha 80% wanataka chama kimoja ilikuwa ni ujanja wa kuweza kufanya manipulation hii tuliyo ishi nayo miaka yote.

Nakusudia, kwakuwa watu hawakuwa tayari kuwa na vyama vingi ndio maana hawakuwa na attention yoyote juu ya ubovu wa katiba kuminya vyama vya upinzani, hata pale wapinzani walipo sema ni kama watu walikuwa wanawashangaa tu kwasababu wanaona vyama vipo tayari! Yote kwa yote Baba wa taifa alitimiza wajibu wake na taifa limefika hapa leo tulipo leo, kazi kwetu na viongozi wa sasa kutafuta hatma njema ya taifa ktk miaka ijayo! Tutambue historia yetu ila tusijikite ktk lawama kwa wafu.
 
Moja kwa moja.

Nilikuwa natazama kwa umakini YouTube hoja za Lisu wakati alipoalikwa kuongea katika kongamano Moja katika chuo cha Makerere Uganda.

Kutokana na Maelezo yake alimsifia Mwalimu kwa jitihada zake za ukombozi Afrika , kutopenda ufisadi na kujilimbikizia Mali Kisha akaenda kwenye point yake kuu kuwa Mwalimu kapanda mbegu mbaya sana ya utawala mbovu Tanzania na hiyo ikaota mizizi kwa vijana wake wa karibu aliowalea Museveni na Kagame nao wanatumia Misingi ya Mwalimu katika kufanya mabaya katika tawala zao.

Kutokana Maelezo yako amesema Mwalimu kaacha mbegu na Legacy hizi ambazo zinatumiwa vibaya na watala wa Afrika Mashariki.

1. Imperial Presidency (Uraisi Wenye mamlaka kupitia kiasi kama Mfalme ) .
Katiba ilimpa Rais mamlaka makubwa sana: kuwa Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, na pia uwezo wa kuteua Makamu wa Rais, Mawaziri, na kuvunja Bunge katika mazingira fulani. Sheria kama Preventive Detention Act zilimruhusu Rais kumweka mtu kizuizini bila mashitaka, na marekebisho ya baadaye yakaruhusu pia kuteua wabunge kadhaa, jambo lililoimarisha zaidi urais kuliko Bunge na taasisi huru.

2. Politicization of military ( Siasa kuingia jeshini ; jeshi kufanywa kama Chombo Cha siasa.

Badala ya kuwa taasisi huru ya kitaaluma. Hii ilimaanisha kuwa wanajeshi walichaguliwa na kulelewa kisiasa na CCM, hivyo siasa za chama zikapenya ndani ya jeshi na kuzuia uwezekano wa jeshi kuwa chanzo cha upinzani wa wazi kwa utawala.

Hivyo, jeshi na vyombo vya usalama vikawa sehemu ya uti wa mgongo wa chama na urais, jambo linalolinda utawala uliopo lakini pia linafanya taasisi za usalama zionekane kama chombo cha siasa badala ya chombo cha kitaifa tu.

3. Militarization of Politics : (Hii sijui kuichambua na kuelezea wataalamu nisaidieni) .

Summary : Nguvu ya watawala katika kufanya wanayotaka , kuendesha nchi kibabe , uminywaji wa demokrasia nk katika nchi za Tanzania , Uganda na Rwanda ni matunda ya mbegu aliopanda Mwalimu Nyerere.

#UziTayari
Kutaka rais mwenye mamlaka kidogo ni ujinga,lisu ana fikra/mentality ya kubishana,kuparurana, harakati
Duniani kote rais ndiye amir jeshi mkuu
 
Yes, mimi kwa maono yangu hata lile la kuwaambia kamati kuu ya CCM waende ktk siasa za vyama vingi licha ya kura ya maoni kuonesha 80% wanataka chama kimoja ilikuwa ni ujanja wa kuweza kufanya manipulation hii tuliyo ishi nayo miaka yote.

Nakusudia, kwakuwa watu hawakuwa tayari kuwa na vyama vingi ndio maana hawakuwa na attention yoyote juu ya ubovu wa katiba kuminya vyama vya upinzani, hata pale wapinzani walipo sema ni kama watu walikuwa wanawashangaa tu kwasababu wanaona vyama vipo tayari! Yote kwa yote Baba wa taifa alitimiza wajibu wake na taifa limefika hapa leo tulipo leo, kazi kwetu na viongozi wa sasa kutafuta hatma njema ya taifa ktk miaka ijayo! Tutambue historia yetu ila tusijikite ktk lawama kwa wafu.
Nakubali kabisa Mkuu, lakini CCM bila external pressure sidhan kabisa inaweza kufanya mabadiliko yoyote yale, ni kujitengenezea kitanzi! CCM wanalijua hilo.
 
Mkuu unaamini CCM ilipata 98% ? Kama hakuna tishio, Kwa nini Lisu yuko ndani, hakuwepo kwenye ulingo?
Shida ya msingi si asilimia ndugu yangu, asimilia 98 ingweza patikana hata kama wangepiga kura watu 50 tu.

Shida hapa ni wizi wa kura, na matokea ya uchaguzi ku-hodhiwa na tume, kifupi tume ndio inatuchagulia Rais si kura. Na hili hakuna mwana CCM hajalisemawazi, kuanzia Mwl Nyerere hadi rais wa sasa, wote ktk nyakati tofauti wamesema jambo linalo ashiria hilo au kulisema waziwazi.

Kuhusu Lissu, mimi naamini Lissu hajakaa ndani kwa kuogopa ushindani, Lissu amekaa ndani kwasabau za ki-usalama baada ya kutoa kauli ya tutakinukisha. Speech yake ilikuwa na clear threat kwa serikali na uchaguzi uliopita. Kwa katiba ya sasa huwezi ogopa ushindani.
 
Kutaka rais mwenye mamlaka kidogo ni ujinga,lisu ana fikra/mentality ya kubishana,kuparurana, harakati
Duniani kote rais ndiye amir jeshi mkuu

Kwa hiyo unaona ni sawa kuwa na Rais ambaye hatima nzima ya kuongoza taifa iko mikononi mwake? Akiwa Mwendawazimu...na hata akaisigina Katiba iliyomuweka madarakani utafanyaje?
 
Ataanza wazimu akiwa ikulu au kabla?
 
Nakubali kabisa Mkuu, lakini CCM bila external pressure sidhan kabisa inaweza kufanya mabadiliko yoyote yale, ni kujitengenezea kitanzi! CCM wanalijua hilo.
Ni kweli, lakini pia kwa njia mabavu kama tulivyo fanya juzi sioni kama yaweza kuwa rahisi ki-hivyo. Mabavu yanaweza leta tija kama Jeshi litawageuka CCM, na hilo ni almost impossible kutokea.
 
Back
Top Bottom