Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, waislamu bado wanazo sababu za kuzuia wanawake kwenda kuzika?

Hapo ndiyo ujenge hoja Sasa. Mimi nataka kuongeza ufahamu wangu kuhusu jambo hili na siyo kuanzisha mabishano.

1gb naye kaongezea jambo hapo kwenye bandiko lake msom
Uislamu ni mafundisho kutoka kwa Allaah kupitia mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Allaah na mtume wakishahukumu jambo au kuliwekea utaratibu mwislamu hana nafasi ya kuuliza faida au madhara ya jambo husika.
Mwislamu anapokufa huwa ni lazima waislamu wenzake wamfanyie mambo manne.
1️⃣ Kumuosha
2️⃣ Kumvika sanda .
3️⃣ Kumswalia.
4️⃣ Kumzika.

Kati ya hayo manne wanawake wanaruhusiwa kumfanyia mambo matatu tu.
1️⃣ Kumuosha kama maiti ni mwanamke mwenzao, jukumu la Kumuosha maiti mwanamke ni la wanawake wenzake. Wanaume hawaruhusiwi Kumuosha maiti wa kike ila tu mwanaume anaruhusiwa Kumuosha mkewe aliyefariki.
Na wanawake hawaruhusiwi Kumuosha maiti mwanaume isipokuwa mwanamke anaruhusiwa Kumuosha mumewe aliyefariki.
2️⃣ Kumvika sanda kama ni mwanamke mwenzao.
3️⃣ Kumswalia akiwa maiti ni mwanamke au mwanaume.
Swala la kusundikiza jeneza na kuzika wanawake wamakatazwa na sisi waislamu tunatakiwa kufuata kilichoamrishwa na sheria na kuacha kilichokatazwa na haimaanishi kwamba wanawake hawajui kuwa maiti anazikwa kwenye udongo kwa kuwa dini haina mafundisho ya siri kwa wanaume ila kuna baadhi ya ibada ambazo ni maalumu kwa wanaume tu na nyingine ni kwa wanawake tu na nyingine ni za wanaume na wanawake.
KWA MFANO KATIKA IBADA AMBAZO NI MAALUMU KWA WANAUME TU NI IBADA YA KUADHINI/ KUTOA ADHANA ( Kuwatangazia waislamu kuwa muda wa kuswali swala fulani imefika ) DUNIA NZIMA ADHANA HUTOLEWA NA WANAUME TU NA HAKUNA NCHI HATA MOJA UTAKAYOKUTA MWANAMKE AKATOA ADHANA PAMOJA NA KUWA KAMA SHARIA YA DINI INGEWARUHUSU UWEZO WA KUTOA ADHANA AU KUADHINI WANAO NA ISINGESHINDIKANA HASA BAADA YA KUJA MAENDELEO YA KUTUMIA VIPAZA SAUTI.
 
Ndugu yetu Allaah akulipe kheri kwa darasa zuri ulilotoa.
Kwa mtu mwenye nia ya kuelewa ameelewa ama yule anayeendekeza ubishi hawezi kuelewa hata kidogo kama alivyosema sheikh Muhammad Naswirul diyn Albany Allaah amrehemu kwamba :
"طالب الحق يكفيه دليل، و صاحب الهوى لا يكفيه ألف
دليل. الجاهل يعلم وصاحب الهوى ليس لنا عليه سبيل"
( Mwenye kuitafuta haki dalili moja inamtosha ( kumuelewesha) na mtu wa matamanio dalili elfu moja hazimtoshi (hata umsomee Quran nzima ataendelea kubishana tu )
Mjinga ( anayejijua kuwa hajui) anaelimishwa , na mtu wamatamanio hatu njia kwa ajili yake ( hatuna uwezo wa kumuelimisha mtu anayetaka haki ifuate matamanio yake )).
 
JAWABU .Wanawake wa kiislamu kutokwenda makaburini ni maamrisho ya Allaah ( ambaye wewe unamuita mwenyezimungu ) Kupitia mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
 
Ndio ipo hivyo hakuna anayeshurutishwa kuzika au kuna mwenye kushurutishwa?
 
Hoja yangu ni huko kujiona kwamba mna akili sana kuliko watu wa dini, basi hivyo tu mkuu.
 
Kuoa hakujawai kuwa na maana nyingine zaidi ya kuoa.
Nchi za waarabu zimefungama na dini ya uislamu na zinafuata sharia (sheria za kiislamu). Chochote kitakachopitishwa na kuhalarishwa kimapewa baraka na mashehe, Maamuma, na maustaz kinafuata sharia za kiislamu Kama hakipo nje ya uislamu hawawezi pitisha
, Kama ni utamaduni na hakipo nje ya uislamu na kimepita, kwanini hawaruhusu watu wajenge makanisa? Kuuza pombe? Kucheza makamari? Migahawa kuuza chakula kipindi cha ramadhani?
Hapo wamepitisha sheria mtoto wa miaka 9 aolewe na siyo hiyo maana unayoeleza wewe
 
Kwanini hamuhoji wanawake kushughulika na mazishi mwanzo mwisho pasina uhitaji wa wanaume?
 
Kila kitu kinasababu zake na sababu ya wanawake kukatazwa kwenda makaburini ni iwe ni Ibada ya kumtii Muumba wao kwa kumtii kwa kutoenda. Hiyo ndio sababu yake kama unataka sababu.
Kwahiyo wanaume wanaoenda kuzika hawamtii muumba? Kama kutoenda ndiyo kumtii muumba
Eleza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika?
 
Kwanini hamuhoji wanawake kushughulika na mazishi mwanzo mwisho pasina uhitaji wa wanaume?
Hizi ni imani tu ambazo zipo.
1. Kwanini China anayeabudu dragon au mjapan anatengeneza bidhaa ambazo hakuna nchi yoyote ya kiislamu inayoweza kutengeneza?
2. Tuseme mungu wa wajapan au wachina ananguvu zaidi kuliko mungu wa waarabu?
 
👍
 
Hizi ni imani tu ambazo zipo.
1. Kwanini China anayeabudu dragon au mjapan anatengeneza bidhaa ambazo hakuna nchi yoyote ya kiislamu inayoweza kutengeneza?
2. Tuseme mungu wa wajapan au wachina ananguvu zaidi kuliko mungu wa waarabu?
Sijakuelewa.
 
Kichwa chako hakie
Kwahiyo wanaume wanaoenda kuzika hawamtii muumba? Kama kutoenda ndiyo kumtii muumba
Eleza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika?
Kichwa chako hakielewi na hutaelewa maandiko yanawazuia wanawake wewe unalzimisha kwa nini wanawake, na kwa nini wanawake wanazaa, hiyo ni Ibada wao wanakaa nyumbani inakuwa ibada, wanaume wanaenda makaburini inakuwa ni Ibada kwao، kama unataka dini iwe unavyotaka wewe haiwezekani na itaendelea kuwa hivyo, nimemalizana na wewe.
Kwahiyo wanaume wanaoenda kuzika hawamtii muumba? Kama kutoenda ndiyo kumtii muumba
Eleza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika?
 
Hoja yangu ni huko kujiona kwamba mna akili sana kuliko watu wa dini, basi hivyo tu mkuu.
Mkuu sio akili sana, ni common sense tu. Kuna kitu unaambiwa ni maagizo ya Mungu halafu hata ukiyaangalia unaona kabisa kwamba kunashida mahala.

Kwa mfano, Mungu anasema ufunge, usile ndio umuombe asikie maombi yako, unajiuliza chakula kua tumboni mwangu Mungu anaumia wapi ama anateseka na nini mimi kua nimeshiba na nikamuomba na akajibu maombi yangu?
 
Dini kwa sasa ni utahira unaokwepeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…