Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, waislamu bado wanazo sababu za kuzuia wanawake kwenda kuzika?

Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, waislamu bado wanazo sababu za kuzuia wanawake kwenda kuzika?

Hapo ndiyo ujenge hoja Sasa. Mimi nataka kuongeza ufahamu wangu kuhusu jambo hili na siyo kuanzisha mabishano.

1gb naye kaongezea jambo hapo kwenye bandiko lake msom
Uislamu ni mafundisho kutoka kwa Allaah kupitia mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Allaah na mtume wakishahukumu jambo au kuliwekea utaratibu mwislamu hana nafasi ya kuuliza faida au madhara ya jambo husika.
Mwislamu anapokufa huwa ni lazima waislamu wenzake wamfanyie mambo manne.
1️⃣ Kumuosha
2️⃣ Kumvika sanda .
3️⃣ Kumswalia.
4️⃣ Kumzika.

Kati ya hayo manne wanawake wanaruhusiwa kumfanyia mambo matatu tu.
1️⃣ Kumuosha kama maiti ni mwanamke mwenzao, jukumu la Kumuosha maiti mwanamke ni la wanawake wenzake. Wanaume hawaruhusiwi Kumuosha maiti wa kike ila tu mwanaume anaruhusiwa Kumuosha mkewe aliyefariki.
Na wanawake hawaruhusiwi Kumuosha maiti mwanaume isipokuwa mwanamke anaruhusiwa Kumuosha mumewe aliyefariki.
2️⃣ Kumvika sanda kama ni mwanamke mwenzao.
3️⃣ Kumswalia akiwa maiti ni mwanamke au mwanaume.
Swala la kusundikiza jeneza na kuzika wanawake wamakatazwa na sisi waislamu tunatakiwa kufuata kilichoamrishwa na sheria na kuacha kilichokatazwa na haimaanishi kwamba wanawake hawajui kuwa maiti anazikwa kwenye udongo kwa kuwa dini haina mafundisho ya siri kwa wanaume ila kuna baadhi ya ibada ambazo ni maalumu kwa wanaume tu na nyingine ni kwa wanawake tu na nyingine ni za wanaume na wanawake.
KWA MFANO KATIKA IBADA AMBAZO NI MAALUMU KWA WANAUME TU NI IBADA YA KUADHINI/ KUTOA ADHANA ( Kuwatangazia waislamu kuwa muda wa kuswali swala fulani imefika ) DUNIA NZIMA ADHANA HUTOLEWA NA WANAUME TU NA HAKUNA NCHI HATA MOJA UTAKAYOKUTA MWANAMKE AKATOA ADHANA PAMOJA NA KUWA KAMA SHARIA YA DINI INGEWARUHUSU UWEZO WA KUTOA ADHANA AU KUADHINI WANAO NA ISINGESHINDIKANA HASA BAADA YA KUJA MAENDELEO YA KUTUMIA VIPAZA SAUTI.
 
Nimegundua kuwa wewe huna lengo la kujifunza. Nyuzi zako za zamani nilikuwa nadhani unataka kujifunza, lakini nimegundua hutaki kujifunza. Ulishawahi kuanzisha uzi (upo Jukwaa la Dini) ukauliza kuhusu Sunnah na ukajibiwa. Ila sijui why unauliza swali kama hili tena.

Wanawake kutokwenda kuzika sio kwa sababu walikuwa hawajui/hawajawahi kujua mazishi ya Kiislam. Unafikiri wanawake hawaendi kuzika kwa sababu hawajui mazishi ya Kiislam? Wanawake katika Uislam wanalazimika kuisoma Dini yao kama wanaume. Wanawake wanatakiwa kuisoma Dini yao, hakunaga kauli za "mwanamke hana Dini" katika Uislam. Wanawake pia wanakalifishwa na Shariah za Allah, na kuitekeleza Dini kunahitajika Elimu/kusoma, hivyo nao lazima wasome.

Ila hukmu hutofautiana baina ya wanaume na wanawake katika baadhi ya mambo ya Kishari'ah kwa Hikma ya Allah ambaye kawaumba wanawake na wanaume na anawajua vizuri zaidi. Mfano wote wanapaswa kuswali (wanawake na wanaume) ila kuna hukmu wanatofautiana.

Sio kwamba wanaonewa au kukandamizwa.

Na sio kwamba hawafanyi mambo fulani kwa sababu tu hawajui/hawawezi kujua. Kama unavyotaka kuashiria.

Kukutaarifu tu;
Wanawake wanaosha maiti za wanawake wenzao, bali Mwanamke anaruhusiwa kuiosha maiti ya mumewe, wanawake wanaweza kukafini wanawake wenzao (kuwavika sanda). Wanawake wanaswalia maiti (ya mwanamume au mwanamke), hawaendi tu kuzika makaburini.

Kutokwenda makaburini kuzika isikupe tabu. Kukatazwa wanawake kufanya jambo fulani wala sio ajabu. Hili hata kwa wanaume, kuna mambo wanakatazwa ila wanawake wanaruhusiwa. Mfano ni haramu mwanaume kuvaa dhahabu (hapa duniani) ila ni halali kwa wanawake, ni haramu wanaume kuvaa hariri (hapa duniani) ila ni halal kwa wanawake.

Kuna mambo wanaume wanalazimishwa ila kwa wanawake wamepewa hiari, mfano ni ni LAZIMA mwanaume kuswali Swala ya Ijumaa, ila mwanamke anaweza kuswali Swala ya Ijumaa au akitaka akaswali Dhuhr nyumbani kwake badala ya Swala ya Ijumaa, hiari hiyo hajapewa mwanaume, LAZIMA kwa mwanaume (labda awe na udhuru wa kishari'ah). Ni lazima mwanaume kuswali Swala za Faradhi Msikitini katika Jamaa (isipokuwa anapokuwa na udhuru wa kishari'ah utakaomfanya asiswali Jamaa msikitini) ila sio lazima kwa mwanamke kuswali Jamaa msikitini, ila anaweza kuswali msikitini.

Na mifano mengine mingi.

Hukumu zinaweza kubadilika si kwa jinsia tu, hata mtu mmoja huyo huyo, hukmu katika mambo ya Ibadah zinaweza kubadilika kwake kulingana na hali, mfano; mtu anawajibika kuswali Swala tano za Faradhi, ila anavyoswali akiwa katika hali ya kawaida (mzima na afya) ni tofauti kidogo na atakavyoswali katika hali za dharura kama ugonjwa na safari (kuna tahfifu kapewa), hukmu zinabadilika kulingana na hali yake atakayokuwa nayo na Shari'ah ishaweka bayana katika kila hali.

Uislam sio Dini ya Usawa. Ni Dini ya UADILIFU. Hakuna usawa katika Uislam, kuna Uadilifu.

So usitake kutaka kuleta mambo ya "usawa" yaliyotokana na fikra za watu nje ya Uislam (ambazo ni uongo mtupu na uharibifu).

Tunaridhia Shari'ah kutoka kwa Mola wetu. Na tunasikia na tunatii.

Na Allah ni Mjuzi zaidi.
Ndugu yetu Allaah akulipe kheri kwa darasa zuri ulilotoa.
Kwa mtu mwenye nia ya kuelewa ameelewa ama yule anayeendekeza ubishi hawezi kuelewa hata kidogo kama alivyosema sheikh Muhammad Naswirul diyn Albany Allaah amrehemu kwamba :
"طالب الحق يكفيه دليل، و صاحب الهوى لا يكفيه ألف
دليل. الجاهل يعلم وصاحب الهوى ليس لنا عليه سبيل"
( Mwenye kuitafuta haki dalili moja inamtosha ( kumuelewesha) na mtu wa matamanio dalili elfu moja hazimtoshi (hata umsomee Quran nzima ataendelea kubishana tu )
Mjinga ( anayejijua kuwa hajui) anaelimishwa , na mtu wamatamanio hatu njia kwa ajili yake ( hatuna uwezo wa kumuelimisha mtu anayetaka haki ifuate matamanio yake )).
 
Ndugu yangu Baljurashi unanisingizia. Sina lengo lingine ila kujifunza.

Pia Mimi huwa nauliza maswali ambayo wengine wanaona ni "taboo" kuuliza.

Sina nia ya kutaka usawa kwenye dini isiyo yangu bali nahusika nayo. Leo nazika ndugu yangu kitovu kimoja ambaye ni Muislamu. Je hapo uislamu haunihusu?

Hizi dini ni wachache wa mjini ambao hatuna mchanganyiko wa hizi dini mbili kwenye familia zetu.

Hata hivyo maelezo yako mareefu hayajajibu swali langu. Jee wanawake kutokwenda kuzika ni maamrisho ya mwenyezi Mungu ama ni mapokeo ya kitamaduni tu?
JAWABU .Wanawake wa kiislamu kutokwenda makaburini ni maamrisho ya Allaah ( ambaye wewe unamuita mwenyezimungu ) Kupitia mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
 
Kwa kila mfiwa wana haja tofauti,haziwezi fanana haja kwa wafiwa wote.
Hata hiyo hoja ya ufufuo inaweza ikawa haja kwa moja wapo ya wafiwa.
Ili mradi hakuna anaye shurutishwa kuzika.
Kila mmfiwa/wafiwa wanaweza kuamua lini wazike au wasafirishe.
Ili mradi hawavunji sheria wala si dhambi kufanya hivyo.
Ndio ipo hivyo hakuna anayeshurutishwa kuzika au kuna mwenye kushurutishwa?
 
Nikuulize, magizo kama hayo yasiyo na maana yoyote unadhani alieyatoa atakua ana akili timamu? Ama kwa mfano, Iraq limepitisha sheria ya kuruhusu watoto wa miaka 9 kuolewa na wanasema ni maagizo ya Mungu, wewe kwa kumuangalia mtoto wa miaka 9 wa kike kwa akili yako unaona ni sawa aolewe? Je unadhani maagizo kama hayo yaliyolewa na huyo Mungu akiwa na akili timamu kweli?
Hoja yangu ni huko kujiona kwamba mna akili sana kuliko watu wa dini, basi hivyo tu mkuu.
 
Naomba nikueleweshe Bro kuna dini na tamaduni ( dini ni mfumo wa maisha uishi vipi, ule vipi, uvae vipi, uamini kipi)Tamaduni ni namna jamii inavyo yakabili maisha..

Iran kuna tamaduni kama ilivyo nchi nyingine za kiarabu pia Africa tuna tamaduni tofauti na Asia au china..

Kwenye Mada kuoa mwanamke wa umri wa miaka 9.. waarabu iwe muislam au asiye muislam wanatamaduni ya kurithishana na kuoa ndani ya ukoo yan mtoto anaweza kuzaliwa leo ndani ya mwezi mmoja ukaambiwa huyu ataolewa na mtoto wa mpwa wako, unakuta binti Mpaka anakua msichana tayari anajua nani atamuoa

Neno kuoa wanavyo litafsiri sio kumuingilia au kushiriki tendo hapana... Ila ni kuwa halali ya mtu fulani kwa mantiki ya umestirika hauna sababu ya kushawishika na zinaa..

Kwa upande wa dini hiko kitu sijawahi kuona kama kipo ila ni tamaduni ya watu/jamii fulani..
Kuoa hakujawai kuwa na maana nyingine zaidi ya kuoa.
Nchi za waarabu zimefungama na dini ya uislamu na zinafuata sharia (sheria za kiislamu). Chochote kitakachopitishwa na kuhalarishwa kimapewa baraka na mashehe, Maamuma, na maustaz kinafuata sharia za kiislamu Kama hakipo nje ya uislamu hawawezi pitisha
, Kama ni utamaduni na hakipo nje ya uislamu na kimepita, kwanini hawaruhusu watu wajenge makanisa? Kuuza pombe? Kucheza makamari? Migahawa kuuza chakula kipindi cha ramadhani?
Hapo wamepitisha sheria mtoto wa miaka 9 aolewe na siyo hiyo maana unayoeleza wewe
 
Kwanini hamuhoji wanawake kushughulika na mazishi mwanzo mwisho pasina uhitaji wa wanaume?
 
Kila kitu kinasababu zake na sababu ya wanawake kukatazwa kwenda makaburini ni iwe ni Ibada ya kumtii Muumba wao kwa kumtii kwa kutoenda. Hiyo ndio sababu yake kama unataka sababu.
Kwahiyo wanaume wanaoenda kuzika hawamtii muumba? Kama kutoenda ndiyo kumtii muumba
Eleza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika?
 
Kwanini hamuhoji wanawake kushughulika na mazishi mwanzo mwisho pasina uhitaji wa wanaume?
Hizi ni imani tu ambazo zipo.
1. Kwanini China anayeabudu dragon au mjapan anatengeneza bidhaa ambazo hakuna nchi yoyote ya kiislamu inayoweza kutengeneza?
2. Tuseme mungu wa wajapan au wachina ananguvu zaidi kuliko mungu wa waarabu?
 
Nimegundua kuwa wewe huna lengo la kujifunza. Nyuzi zako za zamani nilikuwa nadhani unataka kujifunza, lakini nimegundua hutaki kujifunza. Ulishawahi kuanzisha uzi (upo Jukwaa la Dini) ukauliza kuhusu Sunnah na ukajibiwa. Ila sijui why unauliza swali kama hili tena.

Wanawake kutokwenda kuzika sio kwa sababu walikuwa hawajui/hawajawahi kujua mazishi ya Kiislam. Unafikiri wanawake hawaendi kuzika kwa sababu hawajui mazishi ya Kiislam? Wanawake katika Uislam wanalazimika kuisoma Dini yao kama wanaume. Wanawake wanatakiwa kuisoma Dini yao, hakunaga kauli za "mwanamke hana Dini" katika Uislam. Wanawake pia wanakalifishwa na Shariah za Allah, na kuitekeleza Dini kunahitajika Elimu/kusoma, hivyo nao lazima wasome.

Ila hukmu hutofautiana baina ya wanaume na wanawake katika baadhi ya mambo ya Kishari'ah kwa Hikma ya Allah ambaye kawaumba wanawake na wanaume na anawajua vizuri zaidi. Mfano wote wanapaswa kuswali (wanawake na wanaume) ila kuna hukmu wanatofautiana.

Sio kwamba wanaonewa au kukandamizwa.

Na sio kwamba hawafanyi mambo fulani kwa sababu tu hawajui/hawawezi kujua. Kama unavyotaka kuashiria.

Kukutaarifu tu;
Wanawake wanaosha maiti za wanawake wenzao, bali Mwanamke anaruhusiwa kuiosha maiti ya mumewe, wanawake wanaweza kukafini wanawake wenzao (kuwavika sanda). Wanawake wanaswalia maiti (ya mwanamume au mwanamke), hawaendi tu kuzika makaburini.

Kutokwenda makaburini kuzika isikupe tabu. Kukatazwa wanawake kufanya jambo fulani wala sio ajabu. Hili hata kwa wanaume, kuna mambo wanakatazwa ila wanawake wanaruhusiwa. Mfano ni haramu mwanaume kuvaa dhahabu (hapa duniani) ila ni halali kwa wanawake, ni haramu wanaume kuvaa hariri (hapa duniani) ila ni halal kwa wanawake.

Kuna mambo wanaume wanalazimishwa ila kwa wanawake wamepewa hiari, mfano ni ni LAZIMA mwanaume kuswali Swala ya Ijumaa, ila mwanamke anaweza kuswali Swala ya Ijumaa au akitaka akaswali Dhuhr nyumbani kwake badala ya Swala ya Ijumaa, hiari hiyo hajapewa mwanaume, LAZIMA kwa mwanaume (labda awe na udhuru wa kishari'ah). Ni lazima mwanaume kuswali Swala za Faradhi Msikitini katika Jamaa (isipokuwa anapokuwa na udhuru wa kishari'ah utakaomfanya asiswali Jamaa msikitini) ila sio lazima kwa mwanamke kuswali Jamaa msikitini, ila anaweza kuswali msikitini.

Na mifano mengine mingi.

Hukumu zinaweza kubadilika si kwa jinsia tu, hata mtu mmoja huyo huyo, hukmu katika mambo ya Ibadah zinaweza kubadilika kwake kulingana na hali, mfano; mtu anawajibika kuswali Swala tano za Faradhi, ila anavyoswali akiwa katika hali ya kawaida (mzima na afya) ni tofauti kidogo na atakavyoswali katika hali za dharura kama ugonjwa na safari (kuna tahfifu kapewa), hukmu zinabadilika kulingana na hali yake atakayokuwa nayo na Shari'ah ishaweka bayana katika kila hali.

Uislam sio Dini ya Usawa. Ni Dini ya UADILIFU. Hakuna usawa katika Uislam, kuna Uadilifu.

So usitake kutaka kuleta mambo ya "usawa" yaliyotokana na fikra za watu nje ya Uislam (ambazo ni uongo mtupu na uharibifu).

Tunaridhia Shari'ah kutoka kwa Mola wetu. Na tunasikia na tunatii.

Na Allah ni Mjuzi zaidi.
👍
 
Hizi ni imani tu ambazo zipo.
1. Kwanini China anayeabudu dragon au mjapan anatengeneza bidhaa ambazo hakuna nchi yoyote ya kiislamu inayoweza kutengeneza?
2. Tuseme mungu wa wajapan au wachina ananguvu zaidi kuliko mungu wa waarabu?
Sijakuelewa.
 
Kichwa chako hakie
Kwahiyo wanaume wanaoenda kuzika hawamtii muumba? Kama kutoenda ndiyo kumtii muumba
Eleza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika?
Kichwa chako hakielewi na hutaelewa maandiko yanawazuia wanawake wewe unalzimisha kwa nini wanawake, na kwa nini wanawake wanazaa, hiyo ni Ibada wao wanakaa nyumbani inakuwa ibada, wanaume wanaenda makaburini inakuwa ni Ibada kwao، kama unataka dini iwe unavyotaka wewe haiwezekani na itaendelea kuwa hivyo, nimemalizana na wewe.
Kwahiyo wanaume wanaoenda kuzika hawamtii muumba? Kama kutoenda ndiyo kumtii muumba
Eleza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika?
 
Hoja yangu ni huko kujiona kwamba mna akili sana kuliko watu wa dini, basi hivyo tu mkuu.
Mkuu sio akili sana, ni common sense tu. Kuna kitu unaambiwa ni maagizo ya Mungu halafu hata ukiyaangalia unaona kabisa kwamba kunashida mahala.

Kwa mfano, Mungu anasema ufunge, usile ndio umuombe asikie maombi yako, unajiuliza chakula kua tumboni mwangu Mungu anaumia wapi ama anateseka na nini mimi kua nimeshiba na nikamuomba na akajibu maombi yangu?
 
Back
Top Bottom