Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 422
- 489
Uislamu ni mafundisho kutoka kwa Allaah kupitia mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.Hapo ndiyo ujenge hoja Sasa. Mimi nataka kuongeza ufahamu wangu kuhusu jambo hili na siyo kuanzisha mabishano.
1gb naye kaongezea jambo hapo kwenye bandiko lake msom
Allaah na mtume wakishahukumu jambo au kuliwekea utaratibu mwislamu hana nafasi ya kuuliza faida au madhara ya jambo husika.
Mwislamu anapokufa huwa ni lazima waislamu wenzake wamfanyie mambo manne.
1️⃣ Kumuosha
2️⃣ Kumvika sanda .
3️⃣ Kumswalia.
4️⃣ Kumzika.
Kati ya hayo manne wanawake wanaruhusiwa kumfanyia mambo matatu tu.
1️⃣ Kumuosha kama maiti ni mwanamke mwenzao, jukumu la Kumuosha maiti mwanamke ni la wanawake wenzake. Wanaume hawaruhusiwi Kumuosha maiti wa kike ila tu mwanaume anaruhusiwa Kumuosha mkewe aliyefariki.
Na wanawake hawaruhusiwi Kumuosha maiti mwanaume isipokuwa mwanamke anaruhusiwa Kumuosha mumewe aliyefariki.
2️⃣ Kumvika sanda kama ni mwanamke mwenzao.
3️⃣ Kumswalia akiwa maiti ni mwanamke au mwanaume.
Swala la kusundikiza jeneza na kuzika wanawake wamakatazwa na sisi waislamu tunatakiwa kufuata kilichoamrishwa na sheria na kuacha kilichokatazwa na haimaanishi kwamba wanawake hawajui kuwa maiti anazikwa kwenye udongo kwa kuwa dini haina mafundisho ya siri kwa wanaume ila kuna baadhi ya ibada ambazo ni maalumu kwa wanaume tu na nyingine ni kwa wanawake tu na nyingine ni za wanaume na wanawake.
KWA MFANO KATIKA IBADA AMBAZO NI MAALUMU KWA WANAUME TU NI IBADA YA KUADHINI/ KUTOA ADHANA ( Kuwatangazia waislamu kuwa muda wa kuswali swala fulani imefika ) DUNIA NZIMA ADHANA HUTOLEWA NA WANAUME TU NA HAKUNA NCHI HATA MOJA UTAKAYOKUTA MWANAMKE AKATOA ADHANA PAMOJA NA KUWA KAMA SHARIA YA DINI INGEWARUHUSU UWEZO WA KUTOA ADHANA AU KUADHINI WANAO NA ISINGESHINDIKANA HASA BAADA YA KUJA MAENDELEO YA KUTUMIA VIPAZA SAUTI.