Lazima tukubali ukweli kwamba Waswahili na Wabantu hatuna historia kubwa kuu ya kale kihivyo na kwa hiyo hatuna mengi ya kujifunza, kuchangamsha na kuimarisha misuli ya bongo zetu kutoka kwenye historia yetu na tamaduni zetu wenyewe na kati yetu.
Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa tunahitaji kuchangamana zaidi na watu wa dunia nyingine huko nje za Wazungu, Wachina, Wahindi, Waarabu, Wakorea, Warudi, Waturuki na wengineo ili kujipatia maarifa mbalimbali kupitia historia kuu na filiosofia mbalimbali za maisha katika tamaduni za kale zilizokomaa (ancient cultures)
Kutokujua lugha kubwa kimataifa za Kingereza na Kifaransa zinatufanya kubaki kwenye chungu na mitazamo duni, uono hafifu na mdogo sana kuhusu Dunia kwa upana wake na mambo mbalimbali.
Waislamu japo wanajifunza Kiarabu ila ni kwa ajili ya kusomea Quran na dini tu kwa hiyo haiwasaidii chochote.