Mkuu,
Katika picha ya juu,watanzania tunaonekana kama tuna tatizo kubwa la kiingereza na tunashindwa kupresent kwenye international platforms kwa sababu ya language barrier.
Ila deep down tatizo letu kubwa siyo kiingereza...Ni confidence.
Mbongo Hana confidence kwenye majukwaa ya kimataifa.
Hata hapa kwetu akija mgeni tunamu-overrate sana hasa akiwa anajua kiingereza. Anakuwa superior kwetu.
Nakupa mfano...
Siku Moja tulitoka na kampuni tukaenda kula bata kwenye 5 star hotel Pale DSM. Tuna kampuni tanzu Nairobi ,Kenya. Kuna wafanyakazi kadhaa walikuja kuwakilisha wenzao,walikuwa wanne.
Imagine,katika idadi yao ya watu wanne waliiteka show yenye watz zaidi ya 30!!!
Yani mbele ya wakenya waswahili wenzetu tunakuwa wanyonge kama tumemwagiwa maji!!
Angalau English medium za sasa mbali na kufundisha kiingereza, wanawafundisha watoto swala Zima la confidence mbele za watu.
Watoto wa sasa hivi ukiongea nao ni kama unaongea na mtu mzima mwenzio.
Kwa hiyo mkuu Fanyia kazi kwanza kazi swala Zima la confidence maana umesema lugha tayari unajua 7/10. Hapo ulipofika si haba.
Hata ukijua 10/10 kama huwezi kuongea mbele za watu,siku wakikupa maiki kiingereza chote kitapotea ukigongana na macho ya watu.