Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi ndiko kunakosababisha Magufuli aonekane Shujaa kuliko wenziwe

Kutokutunzwa kwa kumbukumbu za nchi ndiko kunakosababisha Magufuli aonekane Shujaa kuliko wenziwe

Kwa mfano tulikuwepo wakati Mkapa anapokea nchi toka kwa Mwinyi tulimuona kuna mambo makubwa sana kayabadilisha kwenye utumishi wa Umma kama ambayo Mwinyi alivyobadilisha mambo mengi sana kwenye uchumi au Mkapa ambaye alileta nidhamu ya ukusanyaji fedha za umma kwa kuunda TRA.
Wewe Mimi nilikuwepo mkapa Ni half JPM alileta Kodi ya kichwa na Kodi za baiskeli na kuitekeleza Ile Sheria ya uzembe na uzurulaji ili akusanye Kodi alipe Deni aliloliacha mwinyi ambalo lilifikia pabaya na kumbuka watu walikimbilia vijijini kulima mjini palikuwa pachungu kama una Kazi na sera ya ubinafsishaji ilisaidia kukusanya Kodi hivyo mkapa Ni HALF JPM.
 
Kimsingi magufuli alitaka watanzania wafanye mambo mengi wenyewe ili kujikomboa kuwa tegemezi wa ujuzi ndio maana alikuwa anasisitiza kufanya Kazi na miladi mingi ilijaa wazawa na akawa anawaandaa watanzania kujitegemea.
Hakuna anayekataa Magufuli kufanya watanzania kufanya mambo mengi wenyewe. Ila na wenzie walifanya hivyo pia.

Yule Binti Juliet Kairuki aliyetumbuliwa kisa hakuwa anachukua mshahara wake hakuwa Mtanzania??
 
Wannaomponda magufuli huwa siwaelewi kabisa mm nimeshuhudia vizuri utawala wa mwinyi na nlianza kupiga kura yangu kipindi cha pili cha mkapa. Kipindi cha nyerere pia nlikishuhudia japo sikuwa na akili ya kuelewa vitu. Kwangu mm magu alikuwa bora kuliko wote
Ubora wake unaupata kwenye nini??

Hebu sema kwa Mkapa unakumbuka alifanya nini tofauti na Mwinyi??
 
Wewe Mimi nilikuwepo mkapa Ni half JPM alileta Kodi ya kichwa na Kodi za baiskeli na kuitekeleza Ile Sheria ya uzembe na uzurulaji ili akusanye Kodi alipe Deni aliloliacha mwinyi ambalo lilifikia pabaya na kumbuka watu walikimbilia vijijini kulima mjini palikuwa pachungu kama una Kazi na sera ya ubinafsishaji ilisaidia kukusanya Kodi hivyo mkapa Ni HALF JPM.
Aisee!!

Aliyekusimulia amekupotosha sana.
 
Kaacha madeni makubwa vile vile na kuvuruga mfumo wa Hifadhi ya jamii. Miradi mingi aliiacha haijakamilika na inakamilishwa sasa. Kwa ivo ukiweka mradi kumbuka weka uliokamilika.

Ubungo interchange ulianza kutekelezwa tangu zama ya Kikwete na ndiyo maana zile nyumba za Ubungo zilibomolewa wakati Kikwete akiwa Rais.
Why haukujengwa hebu msijiondoe ufaham bana
 
Aisee!!

Aliyekusimulia amekupotosha sana.
Mkapa ndiye aliyewafumua mashekh pale mwembe chai Kwa Sababu za hovyo kama JPM alivyowafumua wale waliokuwa magaidi kule pwani wakaua Askari polisi 11 na wajinga kama zitto na lissu wakawatetea hivyo mkapa na JPM Ni wale wale tofauti Yao Ni ndogo ndio maana mkapa alimkubali sana JPM.
 
Mwenda zake SI shujaa kuna makundi Fulani ambayo ni
1.wajinga na wenye wivu
2.walio kuwa wanamfaidi na wanafiki
Hiyo namba Moja twaweza walisema wanao mpenda mwenda zake ni wajinga na wasio soma ndo wanao mwona shujaa
Pia jamaa alikuwa mwoga sanaa
Hatakuwa shujaa na hatawahikuqa shujaa
SI Bora mandonga tu

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Kwani nyumba za ubungo Kimara zimebomolewa mwaka gani?? Na jee zilibomolewa ili kifanyike nini kama siyo kujengwa kwa barabara??
Kwani Mladi WA JNHP na kuhamia dodoma ulipangwa au kuandaliwa Kwa kipindi gani huko nyuma lakini mwamba Mzee Wa matokeo amefanya Kwa vitendo hivyo ATA huo unaosema inaweza kuwa kweli ulikuwa kwenye mipango Ila aliyeufanya ukawa ni Nani?.
 
Nilikuwepo baiskeli ya baba ilikamatwa akalipa 500.
Hivi unajua thamani ya shilingi 500 wakati Mkapa akiwa Rais? Yaani Baiskeli iliyokuwa inauzwaa kwa shilingi 5000 - 7000 ndiyo kodi yake iwe shilingi 500?

Mambo ya Kodi ya Kichwa na baiskeli yalikomeshwa enzi Mkapa akiwa Rais ila wewe unasema yeye ndiye aliyeleta kodi hizo!!
 
Alifuta Kodi ya kichwa akaanzisha hiyo.
 
Hivi unajua thamani ya shilingi 500 wakati Mkapa akiwa Rais? Yaani Baiskeli iliyokuwa inauzwaa kwa shilingi 5000 - 7000 ndiyo kodi yake iwe shilingi 500?

Mambo ya Kodi ya Kichwa na baiskeli yalikomeshwa enzi Mkapa akiwa Rais ila wewe unasema yeye ndiye aliyeleta kodi hizo!!
Inawezekana nachanganya kiwango lakini ilikuwepo Kwa kuwa enzi hizo gari zilikuwa chache nyingi zilikuwa baiskeli .
 
Kwa mfano tulikuwepo wakati Mkapa anapokea nchi toka kwa Mwinyi tulimuona kuna mambo makubwa sana kayabadilisha kwenye utumishi wa Umma kama ambayo Mwinyi alivyobadilisha mambo mengi sana kwenye uchumi au Mkapa ambaye alileta nidhamu ya ukusanyaji fedha za umma kwa kuunda TRA.
Kwahiyo hapa ndio umejibu nilichokuuliza mkuu?
 
Back
Top Bottom