ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 754
- 1,478
Umewaza kitumwa Sana, yaani Taifa huru kama Tanzania liishi kwa kumuogopa boya mmoja anayeitwa Robert Amsterdam? Hivi anagalau unauelewa japo mdogo tu wa Case zinazoshughulikiwa na ICC na jinsi mashtaka yanavyofunguliwa huko? Au kwa vile umesikia Robert Amsterdam ni Wakili unajua anaweza anafanya kila kitu dhidi ya nchi hii?Ni swali muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Amani iwe nanyi wadau!
Usiku wa Jana, Wakili Robert Amsterdam ameitaarifu dunia kupitia Twitter yake kuwa amefikia hatua nzuri kupeleka mashtaka katika mahakama ya ICC Uholanzi dhidi ya Magufuli na Serikali yake.
Leo alfajiri, Magufuli akateua mawaziri wawili -- wa Mambo ya Nje, na wa Fedha.
Muda mchache uliopita kwa mara ya kwanza, wawakilishi wa nchi zinazoisadia zaidi Tanzania kifedha na kimisaada yaani Marekani, Uingereza, Sweden, Norway, Japan, Ujerumani, Finland, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya hawajaudhuria hotuba ya Rais Magufuli Bungeni.
Naomba mnaojua mtuelezee humu, kuna nini kinaendelea jikoni? Au ndo mambo yashakuwa mambo?
Naomba michango yenu!
Nasikitika kuona vijana wa Africa bado tupo kwenye utumwa wa kifikra wa kunyenyekea watu weupe.
Japo ana mapungufu yake kama Binadamu, lakini amini usiamini kama Africa itapata wakuu wa nchi 10 tu wenye Spirit kama ya JPM, Africa itakuwa imara na itaogopwa kama ile Africa iliyoongozwa na J.K. Nyerere, Kwame, na Haile Selassie.
Unajua Africa ni bara pekee linaweza kujitegemea yenyewe na kuwa na ziada ya bidhaa na huduma ikiwa itaamua kutumia ipasavyo rasilimali zinazopatikana kwa manufaa ya Africa yote?
Emancipate yourself from mental slavery, non but ourselves can free our mind~Bob Marley