Kutoweka uzalendo kwa nchi: CCM haiwezi kuepuka lawama

Kutoweka uzalendo kwa nchi: CCM haiwezi kuepuka lawama

Kawe Alumni, Kwahiyo muko tayari kuwapiga watu risasi, kuwateka,kuwapa kesi za kuhujumi uchumi zisizo na ushahidi kama kweli unaipenda ccm na hii nchi yako uliyozaliwa kwanini musimshauri huyo bosi wenu kwanza muanze na kangi yule mzee wa ninja kule bungeni kwani yy ndie wakwanza aliyekua akiitetea hii nchi kushinda wewe na yy ndie aliyekua akikiabudu hichi chama na muda wote anatembea na ilani ya chama na yeye ndie aliyemkashifu na kumtukana alhaji Profesa asadi kule bungeni kwanini usimshauri mkuu kama huyo ninja anze kuwekwa ndani na avuliwe uwanachama ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Hapo sijaelewa inamaana umeandika mwenyew na kujijibu mwenyewe au sio?
Screenshot_20200224-143144.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wetu mpendwa Magufuli usicheke na wasaliti wa nchi, simama imara kama walivyosimama imara wazee wetu

Hii Nchi yetu ni muhimu kiliko mtu mmoja anaetukana Nchi yetu

Tumekukabidhi Nchi ili iwe salama

Angalia venuzuela ilivyofikia ni Kwasababu waliruhusu sana demokrasia
Kwahiyo unamshauri asiruhusu demokrasia kama Venezuela? Ndo ushauri wako?
 
Haiwezekani watu wanazurura duniani kuichafua Nchi yetu. Wamesoma kwa kodi za Watanzania
Wanaheshimika huko nje kwa siha njema ya Nchi yetu. Wakifika kule wanaanza kuitukana Nchi yetu

Hii Nchi yetu ipo kwa sababu kuna watu walijitolea maisha yao yote kuijenga hii Nchi
Kuna watu walimwaga damu.

Kuna watu walienda Uganda kuipigania Nchi wakarudi wamekatika miguu, wengine walirudi hawana mikono, wengine walirudi ni maiti.

Nchi hii ilikombolewa toka tukiwa tumboni mwa mama zetu

Anatokea mtu mmoja mropokaji, msaliti pengine hana hata dna na Tanzania yetu anaenda kwa Mabeberu kutukana Nchi yetu

Wanamtukana Rais wetu mpendwa Magufuli, Wanatukana Maendeleo anayotuletea
Wengine ni Wabunge wanaenda amerika kukutana na Mabeberu ati kuisema vibaya nchi yetu

Serkali watu kama hawa Kwanini mnawaacha huru? Kwanini wasihukumiwe kwa kusaliti wazee wetu waliopigania hii Nchi

Dawa ya usaliti hata huko kwa mabeberu inajulikana
Hao marikani haijawahi kucheka na msaliti wa Nchi adhabu yake inajulikana

China haijawahi kucheka na msaliti nenda popote msaliti wa Nchi zawadi yake inajulikana

Serkali acheni kuwachekea Wasaliti wa Nchi watatuharibia taifa letu

Kama kina kambona wenye heshima zao waliondolewa Uraia kwa manufaa ya Nchi Yetu mnaogopa nini kuwapokonya hawa wasio kuwa hata na historia ya ukombozi wa Nchi yetu!

Tumechoka kila siku Nchi yetu kutukanwa na wanasiasa wasaliti

Hatutaki tuwe kama Congo drc aliwachekea Wapinzani mwisho wake Wapinzani wakaiharibu Congo sasa ni machafuko kila siku huko Congo

Ni bora watu wawili au watatu waumie ili Watanzania milion 50 wawe salama

Tanzania tuna chama cha kizalendo kimoja tu ambacho ni Ccm na Tanu Hivi vyama vingine vimeletwa na Mabeberu kuja kuharibu Amani ya Nchi yetu

Naomba serkali ifutie uraia na kufunga wasaliti wa Nchi yote
Uingereza juzi imefutia uraia watu wengi kutokana na kusaliti Nchi yao

Serkali Kwanini inawaogopa hawa?
Hii nchi si Mali ya CCM...Lumumba mnajidanganya sana..
 
Kama demokrasia inazalisha Wasaliti ndani ya Nchi ina faida gani haswa?
Ni kivipi demokrasia inazalisha wasaliti? Nipe mfano wa usaliti unaosababishwa na demokrasia na mimi nikupe mifano ya kutosha ni kwa vipi ukosefu wa demokrasia unazalisha kusalitiana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Huko kwa Mabwenyenye mnapoenda kuwalamba viatu

Hovyo sana Wapinzani
Mbona juzi tu kule bungeni spika wa wanaCCM walikuwa wanamfokea Zitto kwamba anasababisha mkose misaada. Kwa nini mnalilia misaada toka kwa Mabwenyenye?
 
Huoni wanasiasa wa upinzani wanapishana angani kwenda kuitukana Nchi yetu kwa Mabeberu?
Ni kivipi demokrasia inazalisha wasaliti? Nipe mfano wa usaliti unaosababishwa na demokrasia na mimi nikupe mifano ya kutosha ni kwa vipi ukosefu wa demokrasia unazalisha kusalitiana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Back
Top Bottom