Kutumia Msalaba kama ishara ya ukristo na kanisa si sahihi

Sasa kwa nini tutumie msalaba kama alama?? Mungu mwenyewe amesema adhabu ile ni laana. AMELAANIWA AANGIKWAYE JUU YA MTI. Just a thought for the mind!
Alama ya msalaba wa Kikristo ina maana muhimu sana kwa Wakristo. Msalaba unawakilisha kifo cha Yesu Kristo msalabani na kufanikisha kwa wokovu wa wanadamu kupitia sadaka yake. Hapa kuna baadhi ya maana muhimu za alama ya msalaba:

1. Wokovu na Msaada: Msalaba ni alama ya wokovu na msaada wa Mungu. Yesu alikufa msalabani ili kutusamehe dhambi na kutufungulia njia ya kumwona Mungu.

2. Mapenzi ya Mungu: Msalaba unawakilisha mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili ya wokovu wetu, akionyesha upendo mkubwa wa Mungu.

3. Kifo na Ufufuko: Msalaba pia unakumbusha kifo cha Yesu na ufufuko wake. Kifo chake kilikuwa mwisho wa mateso yake kimwili, lakini ufufuko wake ulithibitisha ushindi wake juu ya mauti na dhambi.

4. Kumtambua Yesu: Wakristo hutumia msalaba kwa heshima na kumkumbuka Yesu Kristo. Ni alama ya imani yao na kumtambua Yesu kama Mwokozi.

5. Kuvumilia na Mateso: Msalaba pia unawakilisha kuvumilia na mateso. Yesu aliteswa na kufa msalabani, na hii inawaonya Wakristo kuvumilia mateso yao kwa sababu ya imani.

Kwa ujumla, msalaba ni alama yenye nguvu inayowakilisha mafundisho makuu ya Ukristo, ikiwa ni pamoja na wokovu, upendo, na ushindi wa Yesu Kristo juu ya dhambi na mauti.
 
Sawa kabisa. Nayajua hayo yote. Lakini kumbuka hata si madhehenmbu yote ya kikristo yanakubaliana kwamba Yesu alisulibiwa kwenye msalaba wa magogo mawili. Si kwamba sijasoma vitabu hivyo vya kimapokeo( Apocryphal books). Na hilo andiko la mtakatifu Yohana kusema kwamba kama yote aliyotenda Yesu yangeandikwa dunia isingetosha kuvihifadhi vitabu ni kichekesho kama likichukuliwa literally! Tuna mamilioni ya vitabu duniani na haijajaa vitabu!
 
Bado swali langu linakuja pale pale. Msalaba una structure ipi? Otherwise tutakuwa tunafanya ibada ya sanamu kuweka ishara ambayo haipo.
 
Hata kama yote aliyotenda na kufundisha Yesu yangeandikwa yote bado dunia haingejaa vitabu na kukosa nafasi ya kuviweka. Unatakiwa kujua mazingira ya mwandishi aliyeandika injili ya Yohana na siyo kutafsiri kila kila kitu literally. Duniani leo kuna mamilioni ya vitabu na wala dunia haijakosa nafasi ya kuviweka!
 
Bado swali langu linakuja pale pale. Msalaba una structure ipi? Otherwise tutakuwa tunafanya ibada ya sanamu kuweka ishara ambayo haipo.
Ile ni alama.
Logo ni kama ukiona bendera za taifa unajua ni taifa gani
 
Msalaba ni ishara ya wapagani toka zamani. Wanasema unawakilisha uchi wa wa mwanaume, viungo vya uzazi vya mwanamke au waabudu ng'ombe.
 
Nimeuliza msalaba una umbile gani? Mtume Paulo alipoongelea habari za msalaba alimaanisha lile gogo la kunyogea watu???? Mbona akili zetu wakristo kama zina kasoro?? Tuna doctoral degrees za Theology sijui hata ni nini tulichosoma huko!
Kwani reli ina umbile gani?
 
Mimi nafanya ishara ya msalaba nikianza kusali njoo unipige basi.
Ifike wakati tuache kulazimishana kwenda mbinguni aisee ukienda wewe inatosha.
 
Sawa kumbe tafsiri yake ni kwamba Yesu alitenda mengi mno na yaliyoandikwa ni machache tu. Mapokeo sio jambo baya kama watu walivyoaminishwa, hata Yesu aliishi mapokeo ya Kiyahudi. Cha msingi hayo mapokeo ni mazuri au mabaya?
 
wanadai ukiwaonesha mapepo hiyo zana ya kuulia wahalifu wananikimbia
 
Mimi nafanya ishara ya msalaba nikianza kusali njoo unipige basi.
Ifike wakati tuache kulazimishana kwenda mbinguni aisee ukienda wewe inatosha.
Mbinguni ni wapi? Isije kuwa kuwa unaamini mbinguni ni kule kwenye anga za juu. Hata Yuri Gagarini, mwanaanga (Astronaut ) wa Urusi alienda huko akasema I didn't find God. Mbinguni na outer space ni vitu viwili tofaouti kabisa
 
Two straight iron lines stretching parallel to each other. Au swali lako lilikuwa na maana gani?
A cross is a compound geometrical figure consisting of two intersecting lines, usually perpendicular to each other.
Bado swali langu linakuja pale pale. Msalaba una structure ipi? Otherwise tutakuwa tunafanya ibada ya sanamu kuweka ishara ambayo haipo.
Au unajibu lako? Jibu la msalaba hilo hapo juu.
 
A cross is a compound geometrical figure consisting of two intersecting lines, usually perpendicular to each other.

Au unajibu lako? Jibu la msalaba hilo hapo juu.
Hilo ni jawabu la lugha ipi? The new testament was written in Greek.
 
Hilo ni jawabu la lugha ipi? The new testament was written in Greek.
Unataka la lugha ya Greek ngoja ni kuwekee.

Ο σταυρός είναι ένα σύνθετο γεωμετρικό σχήμα που αποτελείται από δύο τεμνόμενες γραμμές, συνήθως κάθετες μεταξύ τους
O stavrós eínai éna sýntheto geometrikó schíma pou apoteleítai apó dýo temnómenes grammés, syníthos káthetes metaxý tous

Ukielewa ndio utajua maana ile ile,ukitaka ya kiyahudi niambie.
 
Wewe utakuwa ni Msagati kutoka Musoma, akili za kuambiwa na mzushi Hellen White
 
Mbinguni ni wapi? Isije kuwa kuwa unaamini mbinguni ni kule kwenye anga za juu. Hata Yuri Gagarini, mwanaanga (Astronaut ) wa Urusi alienda huko akasema I didn't find God. Mbinguni na outer space ni vitu viwili tofaouti kabisa
Njoo unipige
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…