Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
(1) Prigozhin alikuwa rafiki mkubwa wa Putin tokea utotoni mwao huko St Petersberg na kuna wakati Putin alikuwa anatayarishiwa chakula na mgahawa wa Prigozhin tu; na mara zote Prigozhin mwenyewe ndiye aliyekuwa aneanda kutoa huduma hiyo ya chakula kwa Putin.
(2) Mwanzoni mwa mwaka 2022, shirika la ujasusi la Marekani lilitangaza kuwa Putin anajiandaa kuivamia Ukraine. Viongozi mbalimbali wa nchi za Magharaibi walimtembelea Putin kummwambia asifanye uvamizi huo. Putin aliwaambia kuwa hiyo ilikuwa ni propaganda ya marekani tu yeye hakuwa na mpando wowote wa kuvamia Ukraine
(3) Mwezi wa pili mwaka 2022, Putin aliishambulia Ukraine kinyume kabisa na vile alivyokuwa anawaambia viongozi wa nchi za Magharibi waliomuomba sana asifanye uvamizi huo kwa sababu za usalama wa dunia
(4) Prigozhin kwa kutumia kampuni yake ya Wagner alimsaidia rafiki yake katika uvamizi wa Ukraine kwa kupigana sana kule Bakhmut na kupoteza askari wake wengi sana akiwamo mtanzania mmoja. Kibaya zaidi kwa Prigozhin ilikuwa ni kwamba jeshi halisi la Urusi lilikuwa halitoi ushirikiano kwa jeshi lake la Wagner japo wote walikuwa wanapigana vita moja kwa ajili ya Putin. Prigozhin alilalamika sana kuhus kukosekana kwa ushirkiano huo
(5) Baada ya kukosekana kwa ushirikiano huo wa namba (4) hapo juu, Prigozhin alitishia kupeleka jeshi lake kwenda Moscow kuwabana waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi wa urusi. Tishio hilo lilionekana kama ni uasi akalistisha. Baada ya kulistisha, Putin akatangza kuwa mfarakano umekwisha na wale askari wote wa Wagner wanatakiwa waijunge na Jeshi, halafu Prigozhin aendelee na biashara zake nyingine lakini siyo ya PMC Wagner tena.
(6) Wakati Putin alipowakaribisha viongozi wa Afrika kwenye mkutano wake, alimruhusu Prigozhin akutane na viongzi wa kiafrika wa nchi ambako ana biashara zake. Hiyo ikionyesha kuwa hana mfarakano na bwana Prigozhin tena.
(7) Majuzi tu Prigozhin alikuwa anasafiri kwenda nyumbani kwake St. Petersrbeg; usafiri wake hutumia ndege mbili au tatu zinazofanana, na anaweza kuingia kwenye ndege yoyote kati ya hizo mbili/tatu bila kuulizwa atatumia ndege gani. Hata hivyo siku hiyo ya tukio, mamlaka zilitaka atamke ataondoka na ndege gani, akachagua ndege ya kwanza. Baada ya ndege hiyo kuondoka mamlaka zilichelewesha ile ndege yake ya pili kuondoka hadi ndege yake ya kwanza ilipokaribia na Tver ambapo kuna Air Defense system installation za jijeshi, ndipo ile ndege ya pili ikaruhusiwa kuondoka Moscow.
(8) Ndege ya kwanza ya bwana Prigozhin ilipoingia kwenye malengo mazuri ya Air Defense System ya Tver, ikatunguliwa; halafu ile ndege ya pili ambayo ilikuwa na mawasiliaono na ile ya kwanza iliposikia mlipuko wa ndege nyeza ya kwanza aikaamua kurudi Moscow; hata hivyo baada ya kuruhusiwa kutua Moscow, watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo ya pili wakatiwa nguvuni.
Matumizi ya zana za kijeshi Urusi yanahitaji kibali cha Putin tu; kwa hiyo utunguzi wa ndege ya Prigozhin ulikuwa na baraka za bwana Putin. Swali langu: Hivi kweli viongozi wa Afrtika tunajiamini nini kukubali maneno ya Putin ambaye hajaonyesha punje ya kusema ukweli siyo tu kwa viongozi wenzake wa nchi nyingine bali hata kwa marafiki zake wa karibu wa tangu utotoni?