Kuunganishiwa separate mita ya umeme nyumba za kupanga

Haina haja ya kwenda tanesco kusajiri ili wakuungie mita,unanunua tu dukani unaita kishoka anakufungia na wala sio illegal.[emoji848][emoji848]
Hiyo kuiita sub meter siyo sawa maana kazi yake ni kusoma tuu units za umeme ulizotumia ili mpangaji akiambiwa achangie elfu kumi kwa mwezi asilete ubishi.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
tunaomba picha yake, ikikupendeza tutajie brand name ili tukanunue.
 
mmmh kujaza umeme tena. Nafikiri hiki kinasetiwa tu. Labda tuseme umelipia 5000 unit 12. So kitasetiwa ukimaliza hizo unit 12 kitajizima.
 
Anatakiwa aongee na mwenyenyumba wake ili amsaidie ku apply Tanesco apate mita nyingine ambayo akifika kwa watoa huduma ambao ni TANESCO TUU Aseme anahitaji kufanya meter separation kinyume cha hapo asije kurudi hapa kutoa ushuhuda wa kutapeliwa
 
Naomba niwape elimu kidogo juu ya submeter.Submeter si mali ya Tanesco.Tanesco inawateja wake wakubwa ambao anaitwa T2 na T3.Hawa wengi ni appartment au hoteli.Mita ya Tanesco ndo inaitwa T2 au T3 sasa unakuta wapangaji wanataka kujua huo umeme wanatumia unaendaje kwa kuhitaji kusoma unit au awe anapewa umeme wa 50,000 then afeed kwenye hiyo submeter.Tanesco haina huduma ya hiyo submeter.Be carefully great thinker
 
Nadhani tanesco wangewekeza kwenye mita ndogo ndogo zakujitegemea kwa nyumba za kupanga na frem wangepiga sana ela maana hapo kuna changamoto na kero kubwa.Hivi vimita walivyoleta vya kuhesabu unit ni ubabaishaji tu na havijatatua tatizo la msingi lakutumia mita moja watu wengi maana kuna nyumba utafikiri wana chomelea vyuma.
 
Ikikupendeza weka vizuri hili watu waelewe maana kwakweli umeme ni janga kwa watu wengi.
 
@ thedreamer thebeliever mwanzo nilijua anaongelea hizi,ni kweli zipo mkuu.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
#Zipo boss zinajizima automatically umeme wako ukiisha ,
#zipo zingine umeme wako ukiisha zinajizima ila unaweza kukopa umeme nyumba au chumba cha jirani ambayo mnashare mita kuu
#Pia unaweza konnekt hizi separating mita zikasoma umeme ,mtu akimaliza unit zake unamzimia manually switch ya kuzimia unaweka chumbani kwako
.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Anatakiwa aongee na mwenyenyumba wake ili amsaidie ku apply Tanesco apate mita nyingine ambayo akifika kwa watoa huduma ambao ni TANESCO TUU Aseme anahitaji kufanya meter separation kinyume cha hapo asije kurudi hapa kutoa ushuhuda wa kutapeliwa
Unaongea kitu ambacho haukijui separating mita mpk aende tanesco,au unacomment ukiwa kwa warden hapo block A ya bibo.
 
Habari zenu wanajukwaa!

Kuna mita fulani za umeme (third part vendor/siyo za Tanesco) niliziona Dar mwaka jana mwishoni, hizi mita ni tofuti na zile ambazo tunaita units counter ambazo zinahesabu matumizi yako lakini hazikati pale unapofikia ukomo wa units ulizolipia, mita hizo nilizoziona Dar utofauti wake na unit counter ni kwamba unaingiza token na zinakata pale umeme unapofikia mwisho wa units ulizolipia bila kuzima kwa wapangaji wengine.

Mita hizi hufanya kazi kwa kushirikiana na mita kuu ya tanesco unachofanya ni kununua umeme kama kawaida halafu tokeni unaingiza kwenye mita kuu na kwenye mita yako ya third part vendor baada ya hapo utakuwa umehuruhusu umeme kuingia kwenye chumba chako tu.

Mita hizi wakati naziona sikuzingatia sana kwakuwa sikuwa na wazo kama nitazihitaji kwa mbeleni na pale Dar nilienda kama dharura tu hata ukiniambia niende tena ile nyumba na mtaa siukumbuki, kama kuna mdau anatumia mita hizi naomba msaada wa namna wa kuzipata na kuwajua wauzaji.
 
Uingize umeme kwenye mita ambayo sio ya TANESCO, na hawa jamaa wakubali?? Umeme uishe usikate?? Naona maajabu
 
Mita inayofanana na hiyo unayoongelea niliiona uwanja wa nanenane Mbeya mwaka 2017. Nilivutiwa sana aisee. Yaani yenyewe unaifix kwenye nyumba ya wakazi wengi. Kila mtu ananunua umeme wake mwenyewe ingawa mita ya TANESCO ni moja. Na kila mtu anaangalia salio la units ambazo amebakiwa nazo. Umeme unaweza kuisha chumba kimoja vyumba vingine wanaendelea kuenjoy. Ukisafiri umeme wako unabaki vile vile hadi urudi unaukuta vile vile.

Halafu ile mita inaingizwa namba kulingana na idadi ya vyumba. Kama vipo 8, kwa mfano, inaingizwa namba 1 mpaka 8. Chochote unachofanya kama kuingiza umeme unaingiza kwanza namba ya chumba mfano 3 kisha unaingiza token. Kuangalia salio ni hivyo hivyo unaingiza kwanza namba ya chumba ndio uone salio la units.

Yaani ni safi sana. Wao walisema watawasiliana na TANESCO ili kuangalia uwezekano wa kujumuisha teknolojia hiyo kwenye mfumo wa umeme ila ndio nasubiri hadi leo sijui waliishia wapi.
 
Uingize umeme kwenye mita ambayo sio ya TANESCO, na hawa jamaa wakubali?? Umeme uishe usikate?? Naona maajabu
Unakata kwa mtu mmoja wengine wanaendelea na maisha. Yaani haukati nyumba nzima.
 
Ni kweli zipo aisee maana kuna mahali nilipanga fremu ya biashara tukawa tumefungiwa hizo kila mpangaji.

Uzuri wake zinasaidia kuondoa kelele za wapangaji wengine kudai wanalipa zaidi ya wengine au kuwakomoa wale wasiotaka kulipia umeme kwa wakati.

Usipolipa umeme unakaa gizani mwenyewe huku wapangaji wengine wakiwa na umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…