Kuuziwa chakula bei juu kwa Wasafiri ni kero kubwa

Zile hoteli mara nyingi zipo Pori , customer ni hao hao wasafiri , na wako limited , operation cost ni kubwa , ili kucover situation inabd bei iwe kubwa mkuu , mana maharage ya kilala, yanachacha wanamwaga , imagine umeyauza Kwa bukubuku
Na kwa nn ziwe pori??
 
Nunua mkate wako wa Buku jero Na soda ya take away buku Anza safari yako Njiani shindia mkate tu utanishukuru baadae
Enzi hizo tukisafiri na mabasi tulikuwa tunabeba chakula kama kawaida. Leo hii kila kitu kimekuwa issue
 
Mimi nawashangaa wanao safiri halafu wanakula njiani mimi siwezi kula kula njiani lazima nitaapike

Hata maji sinywi kuepuka kubanwa na mkojo
 
Hoja hizi zote ni mfu.
1. Kwani zamani kabla ya kujenga hizi hoteli za mbugani ilikuwaje? Ni kwamba magari yalikuwa yanasimama stendi za umma. Kwa mfano route ya Arusha to Dar, magari yalisimama Korogwe au Mombo.
2. Vyoo siyo tatizo kwa sababu magari yakisimama stendi za umma, kutakuwa na vyoo vya umma, na vyoo vya hotel. Abiria watakuwa na wigo mpana zaidi wa kuchagua.
3. Kuhusu ''hadhi'' ya hoteli nayo haina mashiko. Stendi za umma zamani zilikuwa na hoteli nzuri tu tena nyingi. Zilikuwa kwa sababu magari hayakuwa yanasimama tena. Wakirudisha utaratibu wa zamani watajitokeza wengi kujenga hoteli nzuri
 
sijawai ona hotel ya hadhi ya juu barabara zote za mkoa ambapo magari husimama kwa ajili ya vyakula ni upigaji tu wa madereva ili wapewe msosi wa bure
Hata mimi nimewaza kama wewe mkuu sijaona hizo hotel zenye hadhi wanazoongelea.
Kwa mfano ukisafiri kutoka Dar kwenda mikoa ya kaskazini kuna sehemu panaitwa Kabuku abiria hushuka na kununua vyakula kwenye vibanda na migahawa ya kienyeji lakini bado bei iko juu,sasa hapo ndio utaona kwamba sababu walizotoa hazina mashiko.
 
Ila acheni masihara kuna watu wanapenda kula safarini daah utafikiri viboko! unakuta ndo kwanza hata hamjatoka mtu kishapanga maandazi, bagia, vitumbua, sambusa. uko mbeleni ataongea sijui yogati, karanga, korosho,,,chaa! mm navyokuaga na stress ya safari vile hata sielewi mtu anapata wapi ujasiri wa kupakia kila anachokiona mbele yake.
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa mchana
Haya tumia akili ndogo tu kwa kununua biskuti na soda ya take awaye au maji

Wengine tunapenda hivyo vyakula vya buku 5
 
Hiyo biashara angefanya hata mwenye basi, wangeokoa muda na angepata faida,
Vyoo vimo kwenye yutong, friji ndani shida iko Wapi
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Hata Rukwa Kuna maduka yanauza chupa za chai na hotpot. Kama kweli umelala hotel au lodge ya heshima unaweza kuwaambia wakuwekee chai kwenye chupa yako na pilau au wali kwenye hotpot yako.
I am sorry for you Kama unalala gesti za buku jero ambazo Ni special for short time na hawana jiko.
Think in three dimensions young lady.
 
Shida ya wabongo tunapenda sana kula safarini, safari fupi tu ya Dar -Moshi/Dodoma/Iringa mtu anataka ale nyama choma kuku/mbuzi.! Wakati unaweza kukausha tu ukafika kwako ukapika ugali maharage ukashiba bila gharama
Eti Dar to Tanga gari inasimama njiani kula, tuchimbe dawa tusepe tu
 
Ubebe kutoka wapi..

Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Basi fungua mgahawa wako njiani

Ova
 
Mtandikiwe tu pia mikeka hadharani mswali kuwaringishia watu nyinyi ni watu wa dini
Nchi nyingi za africa ukisafiri,vyakula vya njiani huwa ni ghali
Wengine tukisafiri dar to bukoba njiani ni juice na karanga, biskuti, korosho
Sasa unakuta mwingine anataka safiri
Utafikiri anaenda honeymoon

Ova
 
Wabongo sahvi kutwa kulialia tu
Mkuu...
We ukiona bidhaa fulani gharama achana nayo

Ova
 
Hakuna mamlaka ya udhibiti hapa.
 
Kufunga siku moja bila kula ufi

Ila mm pia Ni mlaji hvyo jitaid tu utenge 15 kwa safari ya dar Arusha

Otherwise kausha ukifika dar ufakamie za buku 2

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…