Kuvaa jezi ofisini kupigwe marufuku

Kuvaa jezi ofisini kupigwe marufuku

Bora ingekuwa jezi smart inayofaa hata kwa mtoko mfano Gold fulani yellow au green imekaa poa, Ila utakuta jitu lina kitambi limepiga Tisheti Nyekundu na Nyeupe kama mganga wa kienyeji au raia wa Japan alafu unakuta kitambi kikubwa! Moja kwa moja unajua huyu mtu kichwani hamna kitu
 
Kwenye familia yangu tunajua kuvaa, hatuvai ili mradi mavazi tu, tunavaa kulingana na maeneo tulipo na tunakokwenda. Tunaangalia tunaenda kukutana na watu wa aina gani na kwa malengo gani. Mke wangu si kila mara mtandio na kanga tu wakati mwingine anaacha kichwa wazi nywele zake nzuri zionekane ni mrembo. Na watoto wetu tunawapigisha pamba kulingana na wapi wanaenda. Mavazi ya heshima na hadhi ni muhimu kuzingatia ulipo
 
Huu mtindo unapata kasi sana. Upigwe marufuku kwasababu ni aibu kwa taifa.

Ofisini ni sehemu ya heshima
nadhani ile jezi ya gold na ile ya buluu ya yanga inafaa my lady,
hata kwenye nyumba za ibada inafaa zaidi pia kwa maoni yangu lakini..

ila jezi za timu zingine mfano kuna moja kila mahali imeandikwa more mpaka imelalia upande moja kwa uzito wa maneno dad,🐒
 
Back
Top Bottom