Kuvaa jezi ofisini kupigwe marufuku

Kuvaa jezi ofisini kupigwe marufuku

Sasa kama kuna mtu anachukulia mavazi poa anaweza kuvaa tu atakavyo kesho avae vazi la kijani na njano, bluu, nyekundu na nyeupe, na rangi ya zambarau halafu aende kupiga kura wale maofisa wa kura waone mavazi hayo, hakuna rangi ataacha kuona. Zingatieni sana mavazi ya kuvaa unakoenda
 
Hakika.
Ni kukosa heshima na busara kuja kwa muajiri wako ukiwa umevaa mavazi yanatangaza biashara na taasisi zingine.
Ufanisi wa kazi na matangazo kipi kiondolewe?
Ndio maana unakuta ofisini mtu ana vulunda kazi ila husikii akikemwa kisa tu anavaa mashati ya vitenge,kaunda suit imepauka mpaka imepoteza mvuto.
 
Jezi inapendeza zaidi pahala pake, uwanjani kunako michezo, vibanda umiza na huko vijiweni hasa vijiwe vya kahawa, drafti na vijiwe vya kuuzia magazeti mnasoma vichwa vya habari za michezo, simba, yanga, azamu, singida bs, tabora utd, mashujaa, namungo fc, coastal union, pamba jiji and alike
 
Vipi kama ofisi yako ni Uwanja wa mpira ? (Ground Caretaker) uvae Suti ? Nadhani kila ofisi zina taratibu zao na kama hizo ofisi unazosema zinataratibu au zina uniform basi kuvaa vinginevyo ni utovu wa nidhamu kama utovu mwingine wowote...
 
Back
Top Bottom