Kuvaa jezi ofisini kupigwe marufuku

Kuvaa jezi ofisini kupigwe marufuku

Dress Code kwa Watumishi wa Umma imeelekeza aina tatu za viwango vya mavazi:
1. Kiwango cha kawaida (Casual)
2. Kiwango cha kati (Casual Smart)
3. Kiwango cha juu (Smart)
Na katika hizo, nguo za michezo, fulana zisizo na kola na suruali za jinzi (jeans) katu haziruhusiwi. Watu huvaa kwa mazoea na pengine hakuna ufuatiliaji. Lakini baadhi ya taasisi wapo serious; mfano nenda pale Makao Makuu ya Jeshi (Ngome) na jeans yako kama utaingia, utakuja kusimulia...:KKalinka:
Kuna mambo mengine ya kipuuzi tu.
Jeans siku ya kuvaa casual Ina shida gani?
Ukivaa hivyo utakuwa unafanya kazi yako vibaya?
Mfano niambie sababu ya kulazimisha askari wanyoe ndevu Kama mademu!
Mbona tunaona wapo askari wa Uingereza wanaofuga ndevu wakati fulani?
Hao wakoloni ndio walituachia sheria nyingi za ovyo wakati sasa wao hawazifuati. Sisi tumebaki 1950 hadi leo.
 
Wanakataza jezi hukufuko wa kanzu wa mkeka wa betting(bet slip). Unafiki tu.
Kuna imamu mmoja wa msikiti fulani Ubungo alishinda milioni 100 na kitu.
Huo unafik ndio hautakiwi. Anaoufanya hiari yake na Mungu Wake na hisabu yake
Ikiwa fulani kakosea haitakiwi iwe ndio kiigozo cha sisi kufuata kwani pia itakuwa tunakosea
 
Ndo maana jezi za kwetu zinawekewa mpaka nakshi za vitenge maana huwezi jua mtu ataitumia vipi, sare za vikoba n.k
 
Huu mtindo unapata kasi sana. Upigwe marufuku kwasababu ni aibu kwa taifa.

Ofisini ni sehemu ya heshim
Adhabu kwa mtumishi avaae mavazi ya ovyo ovyo kazini.
1. Kufukuzwa kazi
2. Kushushwa cheo na mshahara
3. Kukatwa mshahara asilimia sijui ngapi nimesahau
4. Onyo
5. Karipio
6. Kunyimwa nyongeza ya mshahara
Waulizeni mabosi wenu wanajua
 
Back
Top Bottom