Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kauli za IGP Sirro zinamuelekeo na zinaviashiria kwa Jeshi la Polisi kuendelea k ( 344 X 640 ).jpg

Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika leo ametoa kauli kali ambayo ndio kauli halali ya Chama chake kuhusiana na Propaganda za kishamba zinazosambazwa na Jeshi la Polisi zikiongozwa na IGP Sirro mwenyewe kuhusiana na shambulizi alilofanyiwa Mh Mbowe na Watu waliotumwa kumdhuru .

Hakuna ushahidi wowote kwamba Mbowe alilewa kama Sirro na waliomtuma wanavyoropoka mitaani , tarehe 8 na 9 June Mh Mbowe hakuwahi kukanyaga Royal Village Hotel kama watunga uongo wanavyodai , na kama kuna anayebisha alete ushahidi wa Mh Mbowe kuwepo eneo hilo kwa tarehe zilizotajwa kama waongo wanavyodai, Hakuna mtu yeyote kati ya wapiga kelele akiwemo Ndugai au Sirro wanaoweza kuthibitisha jambo hilo , wala hakuna Daktari hata mmoja katika waliomtibu Mbowe aliyethibitisha hilo , bali uongo huu unaosimamiwa na IGP kwa kulishwa maneno na Ndugai umeletwa makusudi kwa lengo la kuzima uchunguzi wa kuvamiwa kishamba kwa Mh Mbowe, kama Sirro ana ushahidi auweke hadharani .

Natoa wito kwa Chadema kumchukulia hatua IGP Sirro kwa kujiingiza kwenye siasa tena kwa kutumia Mguu wa kushoto , ikiwa Sirro anahitaji uongozi wa kisiasa basi amuombe Mwenyekiti wake wa CCM amruhusu ili tupambane naye majukwaani, Asijiingize bila taarifa ili asitumbuliwe .
 
Wameshaanza kuweweseka kutoa kauli zao za ajabu, sadly enough mpaka IGP nae kaangukia kundi hilo, na yeye amekuwa mwanasiasa, wasubiri muda ufike wapate taarifa kamili toka Chadema, wao wamalizie uchunguzi wao kwanza.
 
Mbowe alilewa waache kumfichia aibu
Kila mtu anajua Mbowe ni mlevi wa kutupwa
Mwambieni huyo mseminari Mnyika aache kubwabwaja
Hata kama alilewa nyumba anayoishi ina CCTV ambazo zipo controled na serikali kwanini wasilete ushahidi wa video siku wakina siro watakapokuwa nje ya madaraka tutawashughulikia vibaya sana kwa upumbavu wanaofanya hawana kibali cha Mungu.
 
Polisi wataumbuka kwa Mara nyingine tena, Bahati mbaya wameshaongea wote, hawakuweka akiba, hakuna wa kusahihisha. Mbowe hakukanyaga 'Royal Village' siku hiyo na wameshatazama ushahidi wa camera za Royal Bila Shaka! Labda waje na zile CCTV za MO ambazo zinatoa picha za rangi!-Jon Mrema on twitter.

"RPC wa Dodoma kabla hajazungumza na vyombo vya habari, alfajiri ya tukio alikwenda hospitali pamoja na mazingira ya maumivu na matibabu aliyokuwa nayo Mbowe, alizungumza nae, alienda eneo la tukio, alijua undani wa tukio, ndio maana alikiri Mbowe amefanyiwa shambulio" -John Mnyika
 
Polisi wataumbuka kwa Mara nyingine tena, Bahati mbaya wameshaongea wote, hawakuweka akiba, hakuna wa kusahihisha. Mbowe hakukanyaga 'Royal Village' siku hiyo na wameshatazama ushahidi wa camera za Royal Bila Shaka! Labda waje na zile cctv za MO ambazo zinatoa picha za rangi!-Jon Mrema on twitter.
Mkuu ni aibu kubwa sana kuwa na polisi wa aina hii
 
Kuna viongozi wengine hukataa cctv camera nyumbani kwao na inasemekana na Mbowe alizima pia
Hata kama alilewa nyumba anayoishi ina cctv ambazo zipo controled na serikali kwanini wasilete ushahidi wa video siku wakina siro watakapokuwa nje ya madaraka tutawashughulikia vibaya sana kwa upumbavu wanaofanya hawana kibali cha Mungu .
 
Mbowe alipopiga kelele za kuomba msaada, majirani zake walijibu au wali mute ?
Inanikumbusha enzi za Omari Mahita alionyesha visu vyenye mipini ya rangi zinazofanana na bendera ya cuf, akiaminisha watanzania eti vimeletwa kwa ajili ya kuanzishia fujo kipindi cha kampeni. Lile contena hata leo halijaonyeshwa, hivi kweli karne ya 21 bado watz wanalishwa matango pori !!!!!!. Baada ya kustaafu akaenda kuomba ubunge na aliachwa mapema tu. Ma IGP muogopeni muumba
 
Nimejitahidi kusoma mara 2-3 lakini ata sijaona kauli ya maana zaidi ya taarabu tu! Headline kubwa kweli lakini hyo stori sasa! Bora ata taarabu za Hayati Bi Kidude
 
Inanikumbusha enzi za Omari Mahita alionyesha visu vyenye mipini ya rangi zinazofanana na bendera ya cuf, akiaminisha watanzania eti vimeletwa kwa ajili ya kuanzishia fujo kipindi cha kampeni. Lile contena hata leo halijaonyeshwa, hivi kweli karne ya 21 bado watz wanalishwa matango pori !!!!!!. Baada ya kustaafu akaenda kuomba ubunge na aliachwa mapema tu. Ma IGP muogopeni muumba
Omary Mahita nae alikuwa mhuni tu.
 
Back
Top Bottom