Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Natoa wito kwa Chadema kumchukulia hatua IGP Sirro kwa kujiingiza kwenye siasa tena kwa kutumia Mguu wa kushoto , ikiwa Sirto anahitaji uongozi wa kisiasa basi amuombe Mwenyekiti wake wa ccm amruhusu ili tupambane naye majukwaani , Asijiingize bila taarifa ili asitumbuliwe .
Chadema wanatakiwa walete taarifa kinzani inayoonesha sultani alishambuliwa na wasiojulikana baada ya kulumbana na polisi
Iwe mbowe alilewa chakari au la,alienda kwa Joyce mukya au la,hatuhitaji kujua.Tunataka kujua alishambuliwa au aliteleza kwa bahati mbaya?
 
Wewe ndiye mpumbavu kwa sababu una hoja za kipumbavu!
Sikushangai maana akili zote ulishamkabidhi Mbowe!

Unafikiri kwanini Mbowe hajitokezi mwenyewe kujitetea? Watu wana hadi video wamehifadhi wanasubiri aropoke wamwage hadharani.

Wewe endelea kushabikia vitu usivyovijua
 
Inanikumbusha enzi za Omari Mahita alionyesha visu vyenye mipini ya rangi zinazofanana na bendera ya cuf, akiaminisha watanzania eti vimeletwa kwa ajili ya kuanzishia fujo kipindi cha kampeni. Lile contena hata leo halijaonyeshwa, hivi kweli karne ya 21 bado watz wanalishwa matango pori !!!!!!. Baada ya kustaafu akaenda kuomba ubunge na aliachwa mapema tu. Ma IGP muogopeni muumba
Shetani hana rafiki , baadaye alishitakiwa mahakama ya kinondoni kwa kumbaka house girl wake na kumtia mimba halafu akaruka matunzo ya mtoto
 
Nimejitahidi kusoma mara 2-3 lakini ata sijaona kauli ya maana zaidi ya taarabu tu!
Headline kubwa kweli lakini hyo stori sasa! Bora ata taarabu za Hayati Bi Kidude
mbumbumbu hawezi kuelewa
 
Kwani Mbowe hana mdomo?
Kwanini asitokee mwenyewe ajitetee badala ya kina Mnyika kutumia nguvu nyingi kumtetea mwenyekiti
Hili wangelipotezea lipite maana wabongo kama kawaida yao walishasahau wanasubiri tukio lingine wadandie. Kwa sasa wako na bilionea Laizer. Sasa hawa wanafukua tena wakati watu wazima tulishajiongeza, tukatulia. Jamaa atoke basi aongee mwenyewe.
 
Ila kwa hili la kuanguka Mbowe, kwakweli limeaibisha chama na uanachama wote. CDM ninavyowajua kama Mbowe angekua amepigwa wangeongea mpaka tungejuta hahaa ila kwa kuwa ni nguvu ya pombe aah wapo kimya wanarusharusha miguu tuu
hatutegemei lolote jipya kutoka kwa ngeleja , habari za chato mkuu
 
Kanusho kwamba Mbowe hakuwa Royal... Ni wazi kwamba waliosema hivo yawapasa kuthibitisha pasipo shaka. Otherwise wanapoteza uaminifu na ni aibu.
Mbowe anajivunia sana kuwa na watu Msioweza kufikiri kama nyie!
 
Back
Top Bottom