Juni 12 ya mwezi huu,niliweka mada(mods waliiiunganisha) na kusema CHADEMA wameamua kuacha Polisi wafanye kazi yao ila wakifanya tofauti kwa maana ya kutoeleza ukweli wa tukio zima,basi CHADEMA watatoka hadhrani na kueleza kilichotokea.
Leo hii nafurahi kuona CHADEMA wanakusudia kuweka tukio hili hadharani kwa kutoa na ushahidi kama wengine tulivyotarajia.
CHADEMA ina watu smart sana.
Mada yangu ilikuwa ni hii:
Kwa mtazamo wangu,naamini mpaka sasa CHADEMA wameshakusanya taarifa za nini kilitpokea ila waliona kueleza kila kitu ingekuwa ni kuingilia uchunguzi wa Jeshi la Polisi, hivyo waliona ni busara watoe nafasi kwa Polisi kufanya kazi yao na kama maelezo ya Polisi yatakuwa tofauti na kilichotokea, basi watajitokeza kueleza kwa undani nini kilitokea na hiki ndicho binafsi nakitarajia kitatokea wakati wowote kuanzia kesho.
Kama kumbukumbu zangu ziko sahii, Mnyika alisema wakati tukio linatokea,Mbowe hakuwa peke yake bali kulikuwa na watu wengine ambao hawakuwataja hivyo naamini katika kujibu taarifa ya Jeshi la Polisi, CHADEMA watawataja waliokuwepo na pia na kama kuna ushahidi wa ziada,basi watautoa hadharani.
Naamini hata Mbowe mwenyewe atatoa maelezo ya nini hasa kilitokea.
Tusubiri.
Keep your fingers crossed.