Pole sana mkuu.
Ni vyema kwanza kuhakikisha authenticity ya muuzaji wa hio bidhaa. Kuna watu wanatumia advantage ya kujida wapo Zanzibar wakati hawapo Zanzibar, kusudi ili wewe uliopo nje ya Zanzibar ushawishike kutuma pesa ndio upate mzigo badala ya kwanza kwenda kuuona.
Vitu vya kuzingatia wakati unaangazi kwa bidhaa online kwenye mitandao ya zootanzania, kupatana, instagram and the likes, ni kutizama price kwanza. Ukiona it is too good to be true achana nayo. Nishakutana na watu wanajidai wanauza laptop, ambazo ni latest lakini wanauza cheap, nikaangaza angaza, nikagundua kuwa page za insta zinazotangaza izo laptop kuwa picha ndio zile zile, na ukichat nao hawana uhakika wa hata uwepo wa hio bidhaa. Nikajua hawa huenda wakawa madalali tu. Nimeamua kununua laptop kwenye duka la Epic computers, nilimtuma mtu aende akawacheki na kumtumia hela.
Jaribu kuelewa duka liko wapi, na kama una mtu, mtume aende akahakikishe kama kweli wapo, na mtumie huyo mtu wako pesa aende akanunulie yeye. Najua wengine hawana watu wa kuwatuma, na kama ni ivo, usibahatishe kununua kitu chochote kwenye mitandao kama hio maana hao ni individual sellers na hio mitandao unayotumia haiwezi kukulinda.
Kuna wakati nilitaka PS4 pro, nikaona jamaa zenjy anauza. Sasa mimi Zenjy ni kwetu. Nikaamuliza yupo wapi, akanambia Zanzibar Mjini West, Hii tayari ni RED FLAG. Hakuna anaeishi Zanzibar akakufahamisha kuwa eti anakaa Zanzibar mjini WEST! Nikawambia mimi pia nipo Zanzibar, duka lipo sehemu gani, Akasema Jambiani, Tayari hapa amejikoroga, Jambiani na Mjini West wapi na wapi? Nkaona isiwe tabu, kwa bahati mimi nafanya kazi Jambiani, nikamuuliza Jambiani kijiji kipi mana mi nafanyia kazi uko, akajibu kijiji cha kati, ata vijiji havijui. Nkampotezea.
Namba ya mshkaji ni 0624137621 huko Zoomtanzania na Kupatana jina lake ni John nafikiri.