Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Wakuu kwema..

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala ...

Mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake.... Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa namba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndio maongezi yakaishia hapo...

Kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni....?? Naombeni muongozo karibuni
screenshot hiyo page tuletee hapa, tutairipoti insta mpaka ifungiwe, tuta comment mpaka insta wenyewe waifunge.
 
Kama ndio hivyo mbona wewe jamaa wa Ludewa hukumuamini?

rejea comment yako #162
Naona hujanielewa kamanda. Jamaa wa Ludewa alikuwa anakataa watu kwenda kuangalia bidhaa yake ya Macbook. Anataka atumiwe mshiko kwanza. Huo ni utapeli wa waziwazi. That is the difference bro. Huyu anayekuletea mpaka mlangoni bishaa sio tapeli kwa sababu unakuwa hujamlipa na una uwezo wa 100% kukataa kupokea na kulipia bidhaa kama iko tofauti na specification alizotangaza. Tuko pamoja?
 
Umetapeliwa au umetuma mwenyewe?Akisema alikuwa anakudai umeamua kumgeuzia kibao utajiteteaje? Akili za wabongo wengine wanazijua wenyewe tu.Ni hawa hawa ndio wanaoamini kila habari inayowekwa mtandaoni ni ya kweli, nadhani elimu sasa waipate kuwa siyo kila kitu cha mtandaoni ni cha kweli.Kiufupi ndugu,mfate tu diamondplatnumz akuimbie wimbo wa JIBEBE,hakuna namna hapo.
Hata akili zako zina shida kidogo
 
Ww unapenda maeneo yapi kwanza, ambapo ni tambalale sio juu ya jiwe
 
Jamaa awa wa Instagram ni matepeli hivyo hivyo na mimi nilitapeliwa 270K TZS nilikuwa nataka kununua laptop wakaniambia nitume pesa nusu kwanza nikatuma laki mbili na nusu.

Nilivyo tuma wakaniambia awawezi kutuma uwo mzigo kwa agent wao eti kwasababu ya corona wana avoid social distancing kwaiyo ni hatari kwa agent wao wakanitaka nimalizie kiasi cha pesa kilicho baki ndyo waitume mimi nikagoma. Then wakani block.

Nimesha potezea coz ni mda sasa lakini siyo mbaya coz nimejifunza kitu. Biashara mtandaoni imejaa utapeli jiahari
:-D Duh! eti social distance binafsi utapeli kwa hapa dsm hauwezi kuisha sababu kila siku vitu vinabadilika na watu huzidi kutumia mbinu mbalimbali kututapeli kwa hyo pale unapoliwa lazima upate akili.
 
Sitoisahau kipindi iPhones 6, 6+ zimetoka 2014 -2015, ulikuwa mwaka wa fundisho wa kutonunua vitu online.
 
We nae umeyataka mwenyewe, unalipia kabla ya kupata mzigo? Hizo biashara za kizamani sanaaaa umetaka mwenyewe kuibiwa.
 
Nakumbuka wakati naanza biashara ya kuuza simu 2015 nikiwa first year chuo nilikuwa natuma sana mikoani simu baada ya malipo kufanyika yaani huwez amini wateja wangu wengi walikuwa mikoani na walikuwa wanalipia kabla hata sijatuma simu na wengi nilikuwa hata siwafahamu kipindi iko kama ningekuwa tapeli basi ningeshalikuwa tajiri maana wateja walikuwa wanatuma pesa bila hata kuwaza matapeli wakasoma gepu Wakaanz kupost vitu kwa bei rahisi mno kuwaadaa wateja na wateja wakawa wanatuma pesa mizigo haitumwi wanaishia kublockiwa siku hizi watu washasanuka kukutumia pes sio tena kirahisi though wanatuma ila baada ya kujiridhisha muuzaji ni genuine.

Wadada wengi na watu wa mikoani ndio wahanga nambari moja wa hizi mambo.
 
Back
Top Bottom