choupa moting
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 1,508
- 2,577
Mtu humjui unamrushia hela. Acha uibiwe tu.
SlopeMbona kuna mtu anauza bidhaa za nje ya nchi humu na ameshafanya business na watu wengi ikiwemo mimi, unaenda kwa hao makanjanja
Sent using Jamii Forums mobile app
Ile HP Envy ilinivutia kweli na Ile bei yake sasa ikafanya nianze jitihada za kuipata. Bahati nzuri nilikuwa na jamaa yangu huko Zenji ikabidi nimtume aende eneo tajwa kuhakikisha. Kufika huko hilo duka halipo. Kumbe anaenda dukani kwa watu anapiga picha kisha anaziupload.ndiyo mkuu
Duu hapo kweli nimekuwekea jumaa seriously yupo smart coz nimejaribu kutembela page yake nikashangaa likes nyingi Ila hamna comments yeyote coz nilitaka kujua kama kuna customers wengine labda ambao wanakuwa sastified na huduma zake!! Hamna comments hata moja!! HaiwezekaniYani huyo ana namba zaidi ya 20 za majina fake ya miamala na anatumia cm zaid ya moja na anatumia VPN pia kablock comments baada ya kuona watu wanacomments sana lawama na ukituma tu pesa anakublock kikubwa zaidi anajiamin sana kwenye wizi wake naweza kusema kua yuko smart kwenye hii idara ya wizi na teknolojia hapo tafuta mtu anaewezana nae na hana namba inayopatkana na ukipga whatsapp anakata na picha anazopost kwenye page anazitoa kwenye page moja duka ambalo lipo Lagos Nigeria
Dah we jamaa bei ya iPhone 7+ unaijua wewe?iPhone 7+ wao wanauza 450,000
Free delivery ata kama utaletea mfano simu wanachagua ile ambayo ni ya ovyo tu maana masimu yenyewe ni refubrished yan ig now kila mtu anabiashara akiwa na account tu ya kupost.khaaaaa....
Yaaani ukishaona Mtu anauza bidhaa hasa electronics Anadai ana Duka na ni nje ya Dar halafu haanzi kwa kutaja exact location Anajinadi kusema popote tunakutumia, Anza kutumia akili yako vizurii....
Wanatumia trick ya nje ya dar hasa zanzibar maana wanajua Ni ngumu kuifuata,
Na anajua wateja wengi wapo Dar, au Ana ndugu Dar, hivyo akikuambia yupo Dar ni simple tuu utahitaji kumuona au kutuma mtu.
Huyo ni tapeli, hauzi simu na Asilimia kubwa yupo Dar...
Ila vitu vingine ni kujiongeza tuu, sasa kweli mtu anakuambia Anauza simu, yupo Manyara, Tabora, Iringa(kupatana wamejaa hawa) Ukiangalia Mazingira ni bonge ya Duka, Bei nayo hata ya China haioni ndani....
Khaaa sasa kweli kweli kwelii mtanzania mwenzangu Duka la Simu bei chee tena iphones na Macbook za maana likose kote kwa kukaa likae Mara na sumbawanga?????
Halafu pia hii habari ya mjini ya sasa ya free delivery ndio inawaumiza watu..
Ni nzuri ila kiafrica wengi wana mlengo wao mwingine..
Na binafsi hata kama hamna utapeli, sio mpenzi wa biashara za free delivery hasa zile ambazo zinahitaji ukaguzi, bora hizi za kimataifa za kuagiza nje, ila bongo uaminifu bado sana
Raha ya biashara uone bidhaa, ukague, ulidhike, ulipe uchukue..
Sio ulipe uletewe, ulazimike kuchukua,
Ukienda dukani waweza ukutane na option nyingi quality tofauti tofauti uamue mwenyewe ya kuchukua.
Acha dharau sio kila anayetapeliwa ni msukuma, hata wewe ushawahi kutapeliwa but huwezi kusema hadharani, hiyo ni bahati mbayaWasukuma mtaendelea kupigwa kila siku
Sana sana wapenda kitongaMjini wajinga hawaishi
Dah ile pc ilikuwa bomba haiendeni na bei kabisaIle HP Envy ilinivutia kweli na Ile bei yake sasa ikafanya nianze jitihada za kuipata. Bahati nzuri nilikuwa na jamaa yangu huko Zenji ikabidi nimtume aende eneo tajwa kuhakikisha. Kufika huko hilo duka halipo. Kumbe anaenda dukani kwa watu anapiga picha kisha anaziupload.
Hili tangazo nilikutana nalo sana mitandaoni, nikacheka sana. Jamaa alikuwa anauza MACBOOK kwa 250,000/-. Alikuwa ansema yuko Ludea Njombe. Ukitaka umtume jamaa jyako aliyeko Ludewa hapohapo akaione anakuwa mkali na anaku block ama anasema kasafiri kidogo. Naye aliliza wengi sanaKuna mmoja alikua kupatana anauza mac book air au mac book pro kwa bei nyanya kweli kweli.
Mwenyewe alikua anaonyesha yupo Iringa.
I never thought atamnasa mtu mpaka siku nikakuta uzi humu eti jamaa katapeliwa na lile andazi.
Sasa wewe mtu anakwambia yupo Znz na bado unafanya naye business ya kumtangulizia pesa huku hana established trust yoyote kwako? Na kiukweli huyo mtu hayupo Znz. Atakua tu kijiwe fulani huku huku bara akiwapigia stori jinsi alivyomkamata mjinga wake.
Anyway, a sucker is born every second.